MUNGU ANAWEZA KUWAZIMA KAMA UTAMBI MAADUI ZAKO WEWE MUOMBAJI.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

✓✓Mwezi uliopita tulipokuwa katika maombi ya mwezi mzima, moja ya nilivyofunuliwa ni maandiko, leo ngoja nikupe hili ili liimalishe nguvu zako za maombi ili uombe na kushinda katika jina la YESU KRISTO Mwokozi.

Siku moja katika siku hizo za maombi nilipewa Isaya 43:17, nakuletea hapa nikianzia na mstari wa 15 ili uelewe zaidi.

Isaya 43:15-17 " Mimi ni BWANA, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu. BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu; atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa mfano wa utambi."

✓✓Waisraeli ni uzao wa  Kimwili wa Ibrahimu na Kanisa hai la KRISTO ni uzao wa kiroho wa Ibrahimu.

Wagalatia 3:29" Na kama ninyi ni wa KRISTO, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi."

✓✓Wewe  Mteule wa KRISTO ndio Mwisraeli unayezungumziwa sasa.

◼️Sasa katika andiko la Isaya 43:17 MUNGU anasema kwamba atafanya njia hata baharini ili watu wake wapite.

◼️MUNGU anasema kwamba atawatoa jeshi la adui za watu wake, hilo jeshi la adui litalala halitaamka.

Wewe unapambana na jeshi gani la nguvu za giza? 

✓✓MUNGU wa Mbinguni ana uwezo wa kuwalaza hao jeshi la shetani na hawataamka tena kukufuatilia wewe, kinachohitajika ni maombi yako katika Jina la YESU KRISTO.

✓✓MUNGU anasema kwamba jeshi la adui zako litazima kama utambi, kinachohitajika ni maombi yako tu katika jina la YESU KRISTO.

MUNGU atawazima adui zako kama utambi.

Kama ambavyo Mtu anaweza kuzima mshumaa au taa ya utambi kwa kupuliza tu mara Moja Basi kwa MUNGU ni zaidi akiamua kuwazima wachawi wanaokutesa, mizimu wanaokutaabisha, majini wanaokuhangaisha n.k

Najua kwenye ulimwengu wa roho tuna Maadui wengi, mfano ni hapa ambapo Biblia inaweka wazi.

Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,"

Ndugu, ukiishi Maisha matakatifu katika Wokovu wa KRISTO YESU unaweza kuomba na MUNGU akawazima kama utambi adui zako.

◼️Falme za giza zinazokutesa zinaweza kuzimika kama utambi ukiomba katika Jina la YESU KRISTO.
Ndugu omba katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.

◼️ Mamlaka za kishetani zinaweza kutoweka kwa Maombi omba katika Jina la YESU KRISTO ili hizo mamlaka za kishetani zizimike kama utambi sawasawa na Neno la MUNGU.

◼️Wakuu wa giza wanaokutesa wanaweza kuzimika kama utambi kwa Maombi Yako katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.

◼️Majeshi ya pepo wabaya wote wanaweza kuzimika kama utambi ukiomba katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
Mimi Peter Mabula Niko hapa kukuambia rafiki yangu unayesoma somo langu hili kwamba ipo Nguvu ya ajabu katika Maombi katika Jina la YESU KRISTO.

✓✓Adui zako unapambana nao kiroho hata kama wakiwa ni jeshi kubwa  watalala bila kuamka tena kwa Maombi Yako katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi.

✓✓Wachawi wanaokutesa ukiomba wanaweza kuzimwa kama utambi unavyozimwa, yaani kama mshumaa unavyozimwa ndivyo MUNGU atawazima mawakala wa shetani wanaokutesa au kukuwinda.

✓✓Ukiwa muombaji hakika waganga wa kienyeji na tunguri zao na majini yao watazima kama utambi uzimwavyo, watazimwa kama mshumaa katika Jina la YESU KRISTO.

✓✓Ukiwa muombaji, leo unaweza kuomba maombi ukitumia andiko hilo hapo juu Mwanzo na kila anayetumika kipepo dhidi yako, dhidi ya kazi yako, dhidi ya mwili wako au afya yako, huyo adui atazima kama utambi, hatakufuatilia tena.

✓✓Inawezekana nguvu za giza zimevamia ndoa yako au baraka yako, leo kwa maombi unaweza ukawazima kama utambi hao mawakala wa shetani wanaokutesa.
Omba katika Jina la YESU KRISTO na utamuona MUNGU wa Miujiza.

✓✓Inawezekana wakuu wa giza wanawinda kazi yako au familia yako au uzao wako " MUNGU wetu anasema kwamba atawazima kama utambi hao maadui zako wewe unayeishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU na ni muombaji.

Ndugu yangu, nguvu za giza zitazima kama utambi, majini yao yatazima kama mshumaa, katika jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.

◼️"Eee Bwana YESU KRISTO Mwokozi wangu ninaomba mawakala wa shetani wanaopambana nami wazimwe kama utambi sawasawa na Isaya 43:17"

Ndugu, Mimi  nilipofunuliwa andiko hili niliomba sana kwa ajili yangu kisha nikawaombea sana marafiki zangu ambao huwa nawaombea, niliomba hadi furaha ya rohoni ikawa ndani yangu na wakati mwingine nikajikuta naomba huku nacheka maana niliona  ushindi mkuu dhidi ya nguvu za giza.

◼️Ndugu unao muda wa kuomba leo kupitia jina la YESU KRISTO na wakuu wa giza wanaokuwinda watazima kama mshumaa, hawatakuwa na uwezo tena wa kukufuatilia au kukufunga vifungo.
Leo omba ndugu.

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments