MWANAMKE USICHOCHEE NGONO HADI TU SIKU UKIWA NA MUME WAKO NDANI YA NDOA.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote. 
Karibu tujifunze Neno la MUNGU. 

Wimbo Ulio Bora 2:7 "Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe."

Andiko hili ukilisoma Katika Tafasiri ya BHN Biblia inasema 

Wimbo Ulio Bora 2:7  "Nawasihi enyi wanawake wa Yerusalemu, kama walivyo paa au swala wa porini, msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi, hadi hapo wakati wake utakapofika."

✓✓Kumbe mwanamke haitakiwi kuchochea mapenzi hadi ukiwa na mume wako ndani ya ndoa yako.

Lakini leo wapo wanawake wanakiuka maagizo ya Neno la MUNGU, maana wao wanachochea ngono mitaani na njiani.

Siku moja Stendi ya basi nilikuta wanaume wanamchungulia binti mmoja aliyekuwa anasubiri gari akiwa amekaa uchi maana alivaa sketi fupi sana na katanua miguu baada ya kuchoka kuibana, na sina uhakika kama alikuwa amevaa nguo ya ndani maana wanaume wale walikuwa wanamwangalia kwa makini sana na mmoja anam-zoom kwa kamera ya simu huku akimrekodi, ni fedheha mbaya sana.

Katika jamii ya leo hadi mabinti wa Kanisani wanaendekeza ushetani huu, ni fedheha kwa Kanisa.

Ushauri wangu kwa wanawake.

■Mwanamke usichochee ngono kupitia uvaaji wako wa kikahaba.

■Usiwe unakubali kushikwashikwa na wanaume kwa sababu wanakuona kama Kahaba kwa sababu ya uvaaji wa kikahaba. 

■Nguo ya ndani ni siri yako, usikubali kila mtu aione na kuijua kwa sababu ya uvaaji mbaya.

■Kama wewe ni mwanamke uliyeokoka nakuomba usiwe tai unayetembea kama kuku.
Usiwe kondoo uliyevaa mavazi ya mbuzi.
Usiwe kondoo mwenye tabia za mbwa, hata hapo nazungumza kiroho kabisa.
Usiwe mwanadamu mwenye tabia za majini.

■Matiti yako ni kitu cha thamani sana, usiwe unawaonyesha watu mitaani kwa sababu umevaa nusu uchi.

■Mapaja yako  sio choo kiasi kwamba kila mtu anaingia chooni na kuona kukoje. 

Kwanza hakuna mwanamke asiye na mapaja, hivyo wewe unayeonyesha mapaja yako mitaani kwa kuvaa nusu uchi huna akili.

■Sehemu zako za siri ni za siri, usizifanye kuwa "sehemu za wazi"

Heshimu utu wako na mwogope MUNGU aliyeziumba Mbingu na Nchi.

Wimbo Ulio Bora 3:5 "Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe."

●Kumbuka kuvaa kwako nusu uchi kunaleta mitazamo hii kwa wanaume wengi wenye akili.

1. Wanaume wengi wanaokuona nusu uchi  wanadhani wewe ni Kahaba.

2. Hakuna mwanaume atakuheshimu kwa heshima sahihi kama wewe ni mtu wa kuvaa nusu uchi.

3. Kama hujaolewa ni vigumu sana kupata mchumba mwenye hofu ya MUNGU.
Utaambulia walevi tu na wazinzi watakaokutesa baadae

4. Wanaume wengi watadhani  kwamba umetokea  familia yenye malezi mabaya hivyo watakuepuka.

5. Watu wengi wakikuona unavaa nusu uchi watakuchukulia kama mwanamke Malaya na mpenda ngono.

6. Wanaume wengi wanapokuona unavaa nusu uchi watadhani kwamba wewe umeshachafuliwa sana kingono na wanaume wengi, au umeshaambukizwa magonjwa ya zinaa hivyo unatafuta wa kumwambukiza, hivyo wao watakuogopa.

Ndugu, nakuomba badilika kuanzia leo.

Vaa nguo za kujisitiri kama inavyowapasa wanawake wacha MUNGU Katika KRISTO YESU Mwokozi.

1 Timotheo 2:9 " Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa MUNGU."

Jitenge mbali na ubaya wa kila namna ikiwemo kuvaa kikahaba mbele za watu.

1 Wathesalonike 5:22 " jitengeni na ubaya wa kila namna."

Kama wewe ni Mteule wa KRISTO unayejiandaa kwa ajili ya uzima wa milele basi mtii KRISTO na Neno lake.
MUNGU akubariki sana kama ukizingatia.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi Katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 (Maombi, Ushauri, Sadaka ya kuipeleka Injili mbele na mawasiliano ya Whatsapp)
Ubarikiwe 

Comments