NINI UFANYE KUHUSU KARAMA YAKO AU HUDUMA YAKO.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Karama kwa kanisa ni nini?

✓✓Karama ni zawadi za neema ambazo mtu aliyempokea YESU KRISTO kama Mwokozi anapewa na ROHO MTAKATIFU ili amtumikie MUNGU.

1 Wakorintho 12:4-7 " Basi pana tofauti za karama; bali ROHO ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana(YESU) ni yeye yule.
Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali MUNGU ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa ROHO kwa kufaidiana."

◼️Huduma ni nini?

✓✓Huduma ni shughuli au kazi anazozifanya mtu kwa manufaa ya wengi.

✓✓Karama yako au huduma yako ni kitu cha thamani sana ambacho ROHO MTAKATIFU amekupa katika KRISTO ili umtumikie MUNGU.

✓✓Karama yako au huduma yako ni lazima ihusike kuwafanya watu kuwa wateule wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Warumi 1:5 -6 "ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa YESU KRISTO;"

✓✓Karama pia ndio kipawa cha kiroho.

Yohana 12:26" Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu."


◾Ushauri wangu kwako mteule wa KRISTO.

1. Itumie karama yako mbele za watu kumtambulisha YESU KRISTO anayeokoa.

2. Itumie karama kuwafanya watu wamwabudu MUNGU Baba katika roho na kweli ndani ya KRISTO.

3. Itumie huduma yako kuwafanya watu wawe wa YESU KRISTO na sio kuwafanya wawe wa kwako.

4. Itumie huduma yako kwa ajili ya KRISTO na sio kwa ajili ya kwako au ya dhehebu lako.

◼️Karama na huduma ni lazima zifanye kazi katika Kanisa la KRISTO.

1 Wakorintho 12:8-11 " Maana mtu mmoja kwa ROHO apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo ROHO yeye yule; mwingine imani katika ROHO yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika ROHO yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye."

◾Nini ufanye kuhusu karama yako au huduma yako?

1. Pambana ili kulinda huduma yako.
Huduma inalindwa.

2. Pambana ili kuiboresha karama yako au huduma yako.

3. Pambana ili kuikuza huduma yako.

4. Pambana ili umpendeze MUNGU.

✓✓Inawezekana unawaza utapambanaje ili kuikuza huduma Yako au utafanye ili Karama Yako ilete matunda safi mengi kwa MUNGU?
Mimi Peter Mabula nipo Leo hapa kukueleza njia za kufanya ili huduma Yako au Karama Yako ilete Matokeo makubwa .

◼️Njia za kupambana ili karama yako au huduma yako izae matunda.

1. Uwe mtu wa maombi.

1 Wathesalonike 5:17 "ombeni bila kukoma;"

2. Msikilize ROHO MTAKATIFU na ruhusu yeye akusaidie.

Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."

3. Uwe mtu wa kujifunza sana Neno la MUNGU.

1 Timotheo 4:15-16 "Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia."

4. Jifunze pia kwa watumishi wenzako waaminifu kwa KRISTO.

2 Timotheo 3:14-17 "Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika KRISTO YESU. Kila andiko, lenye pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
ili mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema."

◼️Lakini pia katika masuala ya huduma ni muhimu sana ukajua umeitwa kufanya nini katika huduma uliyopewa na MUNGU.

✓✓Je umeitwa kuanzisha huduma?

◾Kama hukuitwa kuanzisha huduma basi usianzishe huduma.

✓✓Inawezekana wewe umeitwa katika huduma ili kuiendeleza huduma ambayo ilianzishwa na wengine.

✓✓Inawezekana wewe umeitwa katika huduma ili kuitegemeza huduma kwa Mali zako, kama ni hivyo tembea kwenye huduma yako hiyo uliyoitiwa kwayo.

✓✓Inawezekana wewe umeitiwa huduma fulani, hakikisha unabaki katika huduma yako.

◼️Mtumikie Bwana YESU KRISTO.

Kumbu 10:12" Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;"

✓✓Kama huijui huduma yako basi omba MUNGU ili ujulishwe.

✓✓Kama huijui karama yako basi njia mojawapo ya wazi ya kuijua karama yako ni nini unapendelea sana kuvifanya katika kazi ya MUNGU.

◼️Hivyo ambavyo Moyo wako unapenda au unatamani sana kuvifanya katika kazi ya MUNGU hiyo ndio Karama Yako.

Unatamani nini katika kazi ya MUNGU?

Hapa sizungumzii vile unavyotamani kwa sababu umemuona mtu anafanya hivyo, hiyo sio njia ya kujua karama yako.

✓✓Nazungumzia vitu vile ambavyo sio kwa sababu ya kuona ila unavitamani tu.

✓✓Mfano kuna mtu anatamani kuimba sio kwa sababu ameona watu wanaimba.

✓✓Kuna mtu anatamani kuhubiri n.k

◼️Fanyia kazi karama yako kama umejiridhisha kabisa kwamba MUNGU amekuita katika karama hiyo.

Matendo 20:28 "Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo ROHO MTAKATIFU amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe."
MUNGU akubariki sana ukifanyia kazi.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.


Comments