![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote.
Katika maombi yako ya leo omba kwa kufuata ufunuo huu ambao umekaa rohoni mwangu kwa siku kadhaa.
Yeremia 15:21" Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha."
MUNGU Baba anasema atakuokoa katika mikono ya watu wabaya na atakukomboa katika mikono ya maadui zako wenye kutisha.
●Kwenye ulimwengu wa roho watu au vitu hushikiliwa kwa mikono ya kiroho, inategemea tu aliyekushikilia kwa mikono ni nani.
Mikono ya maadui zako inaweza kukushika na kukushikilia ili wakuonee watakavyo.
■Kuna watu afya zao zimeshikiliwa na mikono ya wachawi ndio maana watu hao wanaumwa kila wakati.
■Kuna watu ndoa zao zimeshikiliwa kwa mikono ya majini mahaba au zimeshikiliwa na watu wabaya ndio maana ndoa hizo hazikosi vita, migogoro,usaliti na uonevu.
■Kuna watu biashara zao au kazi zao zimeshikiliwa na mikono ya mawakala wa shetani ndio maana japokuwa wako katika eneo zuri kikazi au kibiashara lakini hakuna mafanikio, kuna wako Katika nafasi nzuri kikazi lakini hakuna mafanikio wayatakayo.
■Kuna watu akili zao zimeshikiliwa kwa mikono ya majini/mapepo ndio maana maamuzi yao yote ni ya kipepo na sio maamuzi ya ki MUNGU.
■Kuna watu uzao wao na uchumi wao vimekamatwa na mikono ya wakuu wa giza, kuna watu afya zao au uchumba vimekamatwa na mikono ya nguvu za giza, kuna watu hawana kibali popote kumbe ni roho za nyoka zimeshikilia kibali.
■Kuna watu baraka zao za namna nyingi zimeshikiliwa na mikono ya mawakala wa shetani.
Ndugu, ndio maana leo tunafanya maombi haya muhimu ili mkono wa mchawi au mkono wa jini au mkono wa mkuu wa giza au mkono wa mizimu ukuachie.
Kumbuka kazi za mawakala wa shetani wakija kwako siku zote ni ili tu kuiba baraka zako na haki zako na kazi yao nyingine ni kuleta roho ya mauti na kuleta uharibifu, hiyo ndio kazi ya shetani na mawakala zake.
Yohana 10:10" Mwivi(shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; ............"
Ashukuriwe MUNGU maana YESU KRISTO alikuja ili kuzivunja kazi zote za shetani na mawakala zake, ndio mana leo tuna ujasiri wa kuomba katika jina la YESU KRISTO na tunashinda.
1 Yohana 3:8" ............ Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi."
■■Hakikisha unaishi maisha matakatifu ya Wokovu na ni omba, Kama kuna mahali unatakiwa kutubu tubu na tengeneza na MUNGU katika KRISTO YESU.
■leo omba katika jina la YESU KRISTO ili utolewa katika mikono ya maadui zako na utatoka hakika.
■Omba kuwatoa ndugu zako katika mikono ya shetani au baraka zako zitoe katika mikono ya wakuu wa giza.
Hakika MUNGU atakukomboa leo wewe na baraka zako na watu wako utakaowaombea.
Zaburi 18:3 "Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu."
Nini ufanye katika maombi yako leo?
1. Tubu kwa kilichosabanisha maadui zako kukushikilia au kushikilia baraka zako kwa mikono yao ya kiroho(Taja eneo waliloshikilia mfano mwili,afya,ndoa uchumba,ufahamu, akili, kazi, biashara n.k)
Zaburi 107:6 "Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao."
2. Omba MUNGU akuokoe kutoka mikononi mwa watu wabaya (Wataje ; mfano wachawi, waganga wa kienyeji na kila mtu anayetumika kipepo dhidi yako)
Yeremia 15:21a" Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, ...."
3. Omba MUNGU akukomboe wewe na akomboe baraka zako (zitaje; mfano ndoa,uchumi,familia,mke/mume wako, nyumba yako,uzao wako n.k)
Yeremia 15:21b"..... nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha."
4. Omba maombi ya vita ukiweka ncha ya upanga wa MUNGU kwenye nyumba za maadui zako kwenye ulimwengu wa roho.
Ezekieli 21:15" Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje."
5. Omba mkono wa MUNGU wa kuangamiza uwe juu ya nguvu za giza zilizokufunga au kukutesa.
Kumbu 2:15" Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa kati ya marago, hata walipokoma."
6. Ita ukombozi wa damu ya YESU KRISTO kwenye kila eneo ambalo mawakala wa shetani walikuwa wameshikilia kwa mikono yao ya kiroho.
Waefeso 1:7 "Katika yeye(YESU) huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake."
7. Mshukuru MUNGU kwa ushindi aliokupa kutokana na maombi yako ya leo uliyoomba kwa imani.
Marko 11:24 "Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu."
■■Hakika kama unaomba maombi katika jina la YESU KRISTO na unaomba kwa imani hakika MUNGU atakuokoa dhidi ya maadui zako wenye kutisha na wenye nguvu.
Zaburi 18:16-17 "Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi."
Omba ndugu na Bwana YESU KRISTO atakushindia.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments