PAJUE UNAKOELEKEA.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

✓✓Mkristo aliyeamua kuokoka anatakiwa ajijue kwamba anatoka wapi na anakwenda wapi.

Ni kazi yako mwenyewe Mteule wa KRISTO kujua ulikotoka na sasa inakupasa ujue unakokwenda.

✓✓Ulikotoka ni kwa shetani, kwenye dhambi, kwenye mambo ya kidunia.
Umetoka kwenye njia pana ila inakwenda jehanamu.
Mathayo 7:13 " ........... maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo."

Ulikokuwa kabla ya kumpokea YESU kama Mwokozi ni kwenye njia pana ila njia ya upotevuni.

Njia ya upotevuni/jehanamu ni pana na huwafurahisha sasa watu wengi wa dunia, ni wengi mno wako katika njia hiyo wakielekea upotevuni.

 ◼️MUNGU amekupa neema ya ajabu(Amazing Grace) ukaiona njia nyembamba ya kwenda mbinguni/uzima wa milele.

Mathayo 7:14" Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache."

✓✓Njia hii ya uzima wa milele wanaoiona ni wachache sana.

✓✓Njia hii ni Kuokoka/Kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu katika Wokovu wake.

✓✓Njia hii unaweza ukakuta ukoo mzima ni watu wachache tu ndio wameiona.

✓✓Njia hii unaweza kukuta ofisi nzima ni mtu mmoja tu au wawili ndio wameiona.

✓✓Njia hii unaweza kukuta familia nzima ni watu wawili tu ndio wameiona na wanaifuata.

Njia hii imesonga hivyo watu wa njia pana wanaweza kukuona mshamba au umepungukiwa ukiwa katika njia hii nyembamba, lakini njia yako nyembamba ni ya uzima wa milele na wanaoiona njia ya uzima wa milele ni wachache maana mtu mtenda dhambi hatapenda kupita njia hiyo, mpenda mambo mabaya ya kidunia hawezi kutamani kupita njia hiyo japokuwa ni njia ya uzima wa milele, mzinzi na mwasherati haipendi njia hiyo ya uzima wa milele, mchawi na mnajimu na mganga wa kienyeji na washirika wao hawawezi kuipenda njia ya uzima wa milele, mwizi na tapeli na msaliti wa ndoa hawezi kuipenda njia hii japokuwa ndio njia ya uzima wa milele ambayo wasio safi hawawezi kupita katika njia hiyo.

Isaya 35:8 "Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo."

✓✓Sasa hakikisha unajua ulikotoka na jua pia unakokwenda.

✓✓Ulikotoka ni kubaya sana na kamwe usitamani kurudi huko kubaya, ukilijua hilo hutatamani kurudi huko.

◼️Tambua sasa kwamba unakokwenda ni uzima wa milele, njia ya uzima wa milele ni kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi, njia uliyopo inaitwa njia ya utakatifu.
Kama uko sasa katika njia ya utakatifu maana umeokoka tambua sasa unakoelekea.

✓✓Aliyeokolewa na YESU KRISTO anakoelekea ni uzima wa milele kwenye makazi yaliyoandaliwa kwa ajili ya wateule wa KRISTO waaminifu na wanaoishi sasa maisha matakatifu ya Wokovu.

◼️Bwana YESU KRISTO Mwokozi anathibitisha juu ya makazi aliyotuandalia sisi tuliompokea kama Mwokozi wetu.

Yohana 14:2-6 "Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia.
Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."

◼️Sisi tuliokolewa na Bwana YESU KRISTO tunakokwenda ni mbinguni kwenye uzima wa milele, inatupasa kuishi maisha matakatifu siku zote.

Wale wa njia pana ya upotevuni wao wanakoelekea ni nje ya uzima wa milele.

Ufunuo 22:15 "Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya."

Je unataka uelekee nje ya uzima wa milele au unataka uelekee uzima wa milele?

✓✓Ndugu nakushauri elekea uzima wa milele ambao uko pekee katika MUNGU kwa njia ya Wokovu wa YESU KRISTO pekee.

✓✓Ndugu, usikubali mtu yeyote au kitu chochote kikakutenga na YESU KRISTO.

Warumi 8:33-35 " Ni nani atakayewashitaki wateule wa MUNGU? MUNGU ndiye mwenye kuwahesabia haki.
Ni nani atakayewahukumia adhabu? KRISTO YESU ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa MUNGU; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?"

✓✓Usikubali kazi au Mali au pesa au ndoa au uchumba au dhehebu au dini, usikubali vikakutenga na YESU KRISTO.

✓✓Usikubali chochote kikakutenga na Wokovu wa KRISTO YESU.

◼️Kwa sababu umeamua kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako basi MUNGU anakuhesabia haki.

✓✓Hata kama watu wa dunia watajaribu kukuhukumu kidunia lakini ukweli ni kwamba YESU KRISTO ndio Mwokozi wako ana alilipa deni la dhambi zako pale msalabani, amekusamehe na sasa u huru, kazi yako sasa ni kuishi maisha matakatifu katika Wokovu wake.

✓✓Usikubali chochote kikutenge na utakatifu katika KRISTO.

◼️Uko mahali salama kwa YESU KRISTO.

Naamini hakuna kitakachokutenga na Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments