SHUHUDA 8 MBALI MBALI KUTOKANA NA MASOMO NA MAOMBI.



1. Bwana Yesu Asifiwe Mtumishi
Namshukuru Mungu Amenisaidia Kupata Nafasi Ya Kusoma Baada Ya Wewe kuniombea, Japokuwa Sikuwa Na Sifa Za Kuruhusiwa Kusoma Kulingana Na Kazi Yangu. Ili Niwe Na Sifa Za Kuruhusiwa Kusoma Ilibidi Nikae Kazini Miaka 3,halafu Ndiyo Niombe Kusoma,lakini Nilipokushirikisha Uniombee Hakika Nimepata Nafasa Ya Kusoma Nikiwa Na Mwaka Mmoja tu Kazini.
Namshukuru Sana Mungu Kwa Muujiza Huu Kwangu.
2. Bwana Yesu apewe sifa mtumishi. Namshukuru sana Mungu maana toka uniongize sala ya toba nimejisikia amani sana. Naandaa sadaka yangu ya kusindikiza maombi yangu ya kufunga ambayo nimeamua kuomba.
Mungu akubariki sana na ukipata neno juu yangu tafadhali uniambie.
3. Bwana YESU KRISTO asifiwe Mtumishi Mabula, hivi mtumishi haya masomo yalikuwa yamefichwa wapi? kweli mimi binafisi yananijenga sana. alafu nikuambie mimi hapa nilishabarikiwa kuwa mzee wa kanisa nahata sasa ni mzee wa kanisa. lakini masomo yako sijui kama MUNGU ameanza kuyauumba tena! yaani huwa najiuliza kumbe ndiyo hivi. sasa mtumishi hapa sasa baada yakuanza kupata masomo yako pamoja na uzee wa kanisa. nilianza hatua mpya kabisa kabisa. na pia naomba BWANA WETU YESU KRISTO anisamehe dhambi zangu na makosa yangu yote. nimejikuta bado niko na dhambi japokuwa ni mzee wa kanisa. kweli naomba uniombee toba ya kweli ili nisiwe mtu wa kuachwa siku ile. nina andika haya nasikia uchungu mwingi sana moyoni. kwa muda niliokuwa nafurahisha wanadamu. so naomba BABA wa mbinguni anisamehe. asante sana kwa masomo unayoendelea kufundisha. MUNGU akubariki.
4. Mtumishi ubarikiwe sana.
Ni hivi tangu ulivyofundisha somo la maombi ya vita kusema kweli nimeona tofauti kubwa ijumaa nilitumia niliingia Kwenye maombi ya vita kweli Niliamka mwili wote unauma kama nina homa kubwa lakini ndio uponyaji wangu maana sikuumwa tena, Namshukuru Mungu sana na asante pia kwani masomo yako yamenitoa kwenye hatua moja na kuingia kwenye atua nyingine , Mungu wa Mbinguni akubariki na aendelee kukutumia mimi sitaacha kukwambia Kile ntakachokuwa nakiona na ninapoitaji msaada wako nakuomba usisite kunisaidia kwani natamani nifikie viwango vyatofauti na hapa.
5. Amina Mtumishi! Na ubarikiwe sana.
Umenipa mwanga sana Mafundisho yako yananisaidia sana pale nilipokuwa nimekata tamaa nikikutana na mafundisho yako napata tena nguvu! Maana nina vita sana ninashambuliwa baba'angu wee acha tu!
Kwenye biashara ndo usiseme! Nyumbani nipo namuuguza mama yangu mzazi niko na vita, wanamtumia roho za mauti namuomba Mungu na mama yangu wa kiroho ananisaidia sasa tunapogeuza hizo roho mashambulizi yanarudi kwangu yaani dukani
Mwezi mzima siuzi hata 50'000 yaani baba! Lakini najua IPO siku Mungu ataona na kusikia kilio changu na kunijibu! Alafu ile silaha ya moto wa Yesu uliyofundisha ilinisaidia sana nilipiga Nayo adui mpaka akaniachia akaanguka sikujua Alikopitia!
6. Kristo Asifiweee!!!
Asante sana Pastor Mabulla,kwa kweli unatujuza mengi,kila siku nabadilika,nakuwa kiumbe kipya,Ya kale yamepita sasa yamekuwa mapya hakika,mambo niliyokuwa siyafahamu sasa hivi nimekua kiimani,hakika hatabaki mtu hapo alipo baada ya kusoma kwa makini,kuyafanyia kazi na kuomba kwa Imani kupitia masomo yako.
Jambo moja tu mimi ningefurahi sana ikiwa utaniombea na mimi nipate karama ya kuongea na Roho mtakatifu moja kwa moja kama vile wewe unavyosikia sauti toka ndani mwako ,unajulishwa na unajibu,mbona mimi sina?ni mara mbili hivi nilisikia sauti toka ndani,ikisema ,Niite nami nitaitika basi haijarudia tena,nilijitahidi kuomba ili niwe nijibiwe ,hapana haikutokea,sasa sijui ilikuwa yatoka huko?
Hata hivyo asante sana kwa masomo unayofundisha. Nimejifunza na nimekuwa nami natumia huo upanga mkali ukatao kuwili,upanga unaotembea wenyewe(Mwanzo 3:24)
Nimejifunza pia kuhusu aina nyingi za malaika na jinsi wanavyoweza kuja ,wakati mwingine kama upepo(Zaburi 104:4),kwa kweli Yesu Kristo ni wa kipekee,upendo wake ni mkuu mno
Nimejifunza pia Namna ya kutumia damu ya Yesu katika maombi.Maombi ya vita katika ulimwengu wa Roho!
Nimegundua Kila kitu,kila kitu kipo kwenye Biblia,kila sekta imeguswa katika Biblia,Hii ni ajabu na kweli,nimejifunza kuwa ukianza kusoma Biblia na yenyewe inakusoma wewe,kwa sababu ni kamili!Hili ni jambo la ajabu sana,mambo mengine naona mapya,naanza kujiuliza hili nalo lilikuwa wapi?
Asante sana Pastor Mabulla,Mungu unayemtumikia ni Mkuu,Barikiwa daima Milele,Mungu akulinde,Mungu akupe maisha marefu,Akutane na mahitaji yako,Upande kwa Viwango vya juu katika Utumishi!!!!!
7. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi.
Namshukuru sana Mungu kwa alivyonitendea.
Nashukuru Sana pia kwa maombi yako maana Yale maumivu ya upande wa kushoto yamepungua Sana Sana na ile Hali ya gesi upande huohuo imeachia naamini itakwenda kuisha kabisa siwezi kuadithia maumivu yalikua makali likini baada ya kuniombea naendelea vizuri kabisa nilikua kuinama kwangu Ni shida Sasa nafanya kazi zangu vizuri kabisa Mungu akubariki Sana Sina Cha kukulipa Mungu mwenyewe anajua.
Mungu akubariki
8. Shalom Mtumishi Ninamshukuru Mungu sana kweli ninaendelea vizuri maumivu yale kwenye mgongo yameisha, naomba uzidi kunikumbuka nina vita kali ninaamini nitashinda hata hiyo vita.

Comments