SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKANA NA MASOMO NA MAOMBI.

SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKANA NA MASOMO NA MAOMBI.
Hizi ni baadhi tu ya shuhuda ambazo baadhi yao marafiki zangu ambao husoma masomo yangu na ambao baadhi nimewahi kuwaombea, kwa shuhuda hizo zote sifa, heshima, utukufu na adhama ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni tu anayetenda miujiza kupitia YESU KRISTO Mwokozi wetu.
Utukufu una yeye milele iliyopita na milele ijayo.
Amen Amen Amen
1. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi, ahsante mtumishi wa Mungu kwa maombi yako mtoto wangu ni mzima na anaendelea vizuri, ubarikiwe sana kwa maombi.
Mwanangu alikuwa anaumwa sana ila namshukuru Mungu nilikushirikisha mtumishi ukamuombea na Mungu amemponya.
Mungu akubariki sana.
2. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
yaani Mtumishi Mungu atakulipa kwa haya unayotutendea, wewe ni mmoja wa watumishi wa pekee, mwenye moyo wa upendo huruma na kumsikiliza mtu, yaani mtumishi nakupenda sana maana ni mtu ulionisaidia hadi nipo hapa, nilitaka kuuawa na wachawi lakini nilikupigia ukaniombea kwa Mungu na wao wachawi ndio wakanikimbia mimi, nilikuwa naumwa nikijua sitapona lakini Mungu akamponya, Mungu alikufanya uwe sababu ya kuwa mzima maana uliniombea kipindi nikijua lolote linaweza kutokea kwangu, nadhani unakumbuka, sina kitu chakusema kwakweli bali kila saa namuomba Mungu akuweke bado nakuhitaji yaani sio mimi ila wengi wanakuhitaji sina cha kukulipa ila Mungu atakulipa hapahapa duniani kwa wema wako.
Mungu akupandishe viwango kila itwapo leo
3. Bwana YESU asifiwe mtu, Namshukuru MUNGU sana maana sisi huku tunaendelea vizuri, na habari njema ni kwamba kidonda kinaelekea kupona kabisa, asante kwa maombi.
Pia yule mtoto wangu ambaye alikuwa hatembei baada ya maombi MUNGU alimfanya kutembea, sasa alitembea. MUNGU wetu ni mwema sana.
Muda si mrefu nitakutumia picha ya kovu la kidonda chenyewe.
Msalimie shemeji na MUNGU awabariki sana.
4. Bwana Yesu Kristo asifiwe mtumishi.
Kuna siku ulipost shuhuda na ushuhuda wa dada mmoja ulinigusa sana.
Nimejifunza kitu kwa shuhuda ya huyu dada kukosa kwenda kanisani kwa ajili ya sadaka kwa kukosa pesa.
Iko hivi jumanne ya week hii nilialikwa kwa ibada hapa nchini kwetu kwa kanisa yenye nashiriki kwakuwa niko na muda mrefu sijaenda kanisani kwa sababu zisizo eleweka. nilienda kwa ibada nilibarikiwa sana kwa mafundisho na baada ya mafundisho tuliambiwa wale hawakuja jana waje mbele nilienda pamoja na wengine tulipewa bahasha ya Thanks Giving kumtolea Mungu, jumapili tunapeleka bahasha hizo kanisani ikiwa na matoleo ya Shukrani, nilikua sina pesa lakini niliamini ifikapo jumapili nitapata pesa ya matoleo, jana nilisema sitaenda kanisani sababu sijapata pesa ya matoleo....nimesoma huo ushuhuda umenipa nguvu najua Mungu atatenda ata nisipopata iyo matoleo nitaenda....Mungu akubariki sana mtumishi peter
5. Mtumishi Bwana Yesu asifiwe ,asante kwajili ya masomo yako unayo tuandikia, mimi binafsi yamenibadirisha sana yamenifanya nikue kiroho, ndugu Peter mimi nipo mozambique ninaabudu Kanisa moja la kiroho huku . mara nyingi masomo yako huwa nakopi, huwa nikiwa nasali kuna roho inanisukuma nifundishe kitu watu kupitia masomo yako lakini napuuzia. Ndipo wiki iliopita nikiwa nimelala nilisikia sauti usingizini ikiniambia soma yeremia 1:6 nikaenda kumueleza mchungaji wangu .
6. BWANA YESU asifiwe mtumishi wa MUNGU.
Nina ushuhuda hua nakosa wakati wa kutuma, ni kwamba ule mfungo wa mwezi wa pili uliotuwekea masomo ya maombi kila siku ukielekeza nini cha kuombea, kuna siku tuliomba kufuta kalenda za kichawi. Usingizini nikaonyeshwa mdogo wangu alikuwa amekamatwa na watu watatu wakisema huyu nae yuko kwenye orodha nikajua ni kalenda za kichawi.
Mtumishi mwaka 2009 nilizika Mama yangu, 2013 nikazika mdogo wangu.
2017 nikazika tena mkubwa wa yule mdogo wangu aliyetangulia vifo, na vifo hivyo vyote ilikuwa ni utata tu.
Nashukuru MUNGU sana kwa yale maombi uliyotoa.
Naomba nikumbuke nami kwenye maombi ya picha kama ulivyofundisha kwenye audio, bado nina vita hapa na boss lady wangu havijaisha.
Ubarikiwe sana mtumishi wa MUNGU unasaidia kondoo wa MUNGU kiasi siwezi eleza.
Kupitia masomo yako nimejifunza mengi sana namtukuza BWANA kwa ajili yako nikiwa kwetu kwa kuzaliwa ni mimi tu niliyeokoka na kwa mume pia ni ibada tu za kawaida so nina vita sirahisi lakini MUNGU wetu ni mwema.
7. BWANA YESU asifiwe mtumishi wa MUNGU.
Ujumbe wa leo wenye kichwa POKEA UTU MPYA..nimesoma mda kama saa tano hivi ghafla nimepata nguvu ya kuomba.
Nikitumia ufunuo 5:9,10,DAMU ya mwanakondoo aliye chinjwa..imetoa kwenye lugha..imenitoa kwenye jamaa....na kadhalika na mara nyingi huomba kupitia masomo yako.
MUNGU akubariki utufundishaye kwa upako wa ROHO Mtakatifu.
8. Mtumishi mabula Bwana YESU asifiwe?
Napenda kutoa ushuhuda ulinifundisha somo lenye kichwa cha habari "BAADHI YA MAMBO YA KUJUA KUHUSU SAUTI YA ROHO MTAKATIFU
Sasa usiku wa Jana kuamkia Leo niliota ndoto nasoma kitabu Cha 1samwel1:20 "Naye Eli akambariki Elkana na mkewe,akasema BWANA na akupe uzao kwa mwanamke huyu,badala ya azimo aliloazimiwa BWANA. Kisha wakaenda nyumbani kwao.
Mtumishi mara tu baada ya kuamka nilimshukuru MUNGU Kwa sauti ya ROHO MTAKATIFU iliyonena nami kupitia ndoto maana nimewahi kukushirikisha juu ya changamoto yangu nayopitia katika ndoa yangu ni miaka miwili na nusu hatujapata mtoto.
Lakini tumekuwa na maombi kwa muda wote huo na kuishi maisha matakatifu ya wokovu tukiamini kabisa BWANA YESU KRISTO atatupa majibu kwa wakati na majira yake.
Ubarikiwe sana
9. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Namshukuru Mungu kwa kutuamsha salama Mimi na familia yangu ,bila shaka hata wewe pia umeamka salama.
Peter sikuelewa nini baada ya kusikiliza sala yako ya kufungua kamba na kupasua vifungo (Zaburi 2:3) nikairudia rudia Mara nyingi nyingi muda wa saa kumi na moja nilipitiwa usingizi wa asubuhi nimeota ndoto yaani Mimi mwenyewe nasikia raha ndani ya moyo wangu
Tukiwa mahali ambapo sikupajua kwa mama mmoja, wakati tunaondoka tukakutana na nyoka nikaita wenzangu nyoka ameingia hapa ,wakachimba udongo wa juu wakaonekana kuna nyoka wakubwa watatu na chini yake wamewekewa samaki tena sato wazuri. Mimi nilikaa pembeni kila nyoka anayetoka anapigwa hadi wote tukawaua
Ila mama mwenye nyumba hakufika lakini tulimfuata hakutoka alijifanya yuko bize.
Nimefurahi kwani nijua hawa maadui nimewapunguza wamekufa kwa jina la Yesu Kristo aliye hai.
Peter nakushukuru sana tena sana mafundisho yako na maombi yako hayapiti bila kunitoa pabaya yamenisaidia na kuniokoa, natembea kifua mbele kwa kiburi dhidi ya nguvu za giza ambazo zilikuwa nyingi sana zikiniwinda.
Nikihisi chochote nashika maandiko yako yote na kuanza kuomba, huwa nanakiri masomo yako.
Mungu akubariki sana akutie moyo usikate tamaa kwa watu kama sisi wenye taabu na shida ,tuombee na tusaidie
Nakutakia siku njema
Na Mungu akubariki
Amina

Comments