SHUHUDA MBALIMBALI.

SHUHUDA MBALIMBALI.
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote.
Hapa chini ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki zangu walinitumia, hata na wewe kama una ushuhuda wa kweli ulioupata kupitia masomo yangu au maombezi unaweza ukanitumia ili kumtukuza MUNGU wetu pamoja.
Kuna faida kubwa katika kushuhudia kile YESU KRISTO Mwokozi amenitendea.
Ubarikiwe sana.
1. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu, nakumbuka nilikushirikisha maombi ya kumuombea mchumba wangu ili asifukuzwe kazi, lilikuwa ni tukio gumu sana na wafanyakazi wenzake walijua lazima afukuzwe kazi, hata yeye alikata tamaa kabisa ya kuendelea na kazi, nipo hapa leo mtumishi nikimshukuru Mungu maana mchumba wangu hajafukuzwa kazi amehamishwa tu kituo cha kazi.
Asante sanaa kwa Mungu na asante kwa kutuombea na sasa mambo ni mazuri.
Ubarikiwe Mtumishi.
2. Bwana Yesu asifiwe mtumishi, baada ya wewe kunitumia hiyo audio ukielezea jinsi picha ya mtu inavyoweza kutumika katika madhabahu za giza kumfunga kipepo mtu huyo kuna kitu kimetokea hapa. Ni kwamba huu ujumbe nimeusikiliza usiku wakati wewe unaomba ndani ya audio mwanangu amelia ghafla hadi akaamka ni kama kuna MTU kamfinya nikagundua ni kifungo kinamwachilia ninaamini wengi wamefunguliwa kupitia somo hilo.
Mungu akubariki sana.
3. BWANA YESU apewe sifa Mtumishi Mabula
Leo nishuhudie kidogo juu ya shida nilizo pitia zikanifanya niendelee kumwamini Mungu kuwa yupo. nilipo maliza chuo mwaka Jana nilikosa kitu cha msingi cha kufanya ili niweze kujikimu kimaisha kuna muda nilipitia wakati mgumu sana, nilikuwa nakosa Pesa mwezi mzima unapita bila hata sh mia mfukoni hapo naishi na Dada yangu mtoto wa bamdogo, ikafika hatua shetani akanidanganya niache ata kwenda kanisani kwasababu sina sadaka nitamaliza kama mwezi bila kwenda kanisani wakati mimi kawaida yangu ni kila Jumapili kwenda kanisani, na cha ajabu kanisani hapakuwa mbali natumia dakika 1 _2 kufika kanisani.
Mwisho wa siku Roho Mtakatifu alinijia kupitia kwa wimbo wa BONY MWAITEGE (maisha ni foleni) kuna sehemu anasema "NDUGU YANGU USIACHE IBADA KWASABABU YA KWAMBA UNATAFUTA MAISHA" nikaona kweli na mimi nimeacha ibada kwasababu ya kukosa sadaka hivyo ikanifanya nianze kwenda kanisani bila ata ya sadaka, kama majuma mawili naenda kanisani bila sadaka, majuma mawili yalipoisha Mungu akafungua mlango wa kupata pesa ya kujikimu mimi na kumtolea sadaka mpaka leo ninaposhuhudia sijawahi kukosa kanisani wala kukosa pesa ya matumizi wala pesa ya sadaka
Nitarudia tena Neno hili 1kor 15:57 Lakini na Mungu ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo hakika alinishindia na ashukuriwe Mungu aliye kupa wewe Mtumishi peter Mabula karama hiyo na upendo huo unaotuonyesha kupitia kutuombea na kutufundisha, na aliyenikutanisha na wewe katika WhatsApp hii ilikuwa kama muujiza siwezi kukwambia kwamba namba yako niliipataje wala sio Facebook lakini kaa ukijua mtumishi kwamba na mimi ni mojawapo ya matunda yako na ni wewe uliniongoza sala ya toba nufaikika, TOBA ulioniongoza kipindi kile ndio imekuwa mzizi mkuu kuliko yote ya wokovu wangu, mengne ni kama maji au udongo au mbolea nasitawishwa na huo mzizi mkuu
Mungu akuzidishe zaida na kubariki kazi ya mikono yako unayo Fanya katika SHAMBA lake MUNGU.
4. Bwana Yesu asifiwe mtumishi , ahsante mtumishi wa Mungu kwa maombi yako mtoto wangu ni mzima anaendelea vizuri kabisa.
Ubarikiwe sana mtumishi kwa maombi yako na namshukuru sana Bwana Yesu Kristo kwa kumponya mwanangu.


FAIDA 10 ZA KUMTUMIKIA MUNGU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Karibu ujifunze kitu cha kutusaidia katika maisha yako ya wokovu huku ukimtumikia MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi.
Kutoka 23:25-29 ''Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.''
Faida 10 za Kumtumikia MUNGU.
1. Atabariki Chakula Chako.
2. Atabariki Maji yako.
3. Atakuondolea ugonjwa katikati yako.
4. Hapatakuwa na Mwenye Kuharibu Mimba.
5. Ataondoa Utasa.
6. Hesabu za siku zako ataitimiza.
7. Atatuma Utiisho wake mbele yako ili kuwadhibiti adui zako.
8. Atawafadhaisha maadui wote wakufikirio.
9. Adui zako watakuonyesha maungo yao yaani watadhalilika.
10. Atapeleka mavu mbele yako; watakao mfukuza Mhivi, na Mkaanani na Mhiti wote watoke mbele yako(Mhivi,Mkaanani na mhiti ni tawala za shetani)
Je unamtumikia MUNGU kwa nini?
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuhubiri.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuishi maisha matakatifu.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa matoleo yao kwenye kazi ya MUNGU.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuombea watumishi na Kanisa n.k
Je wewe unamtumikia MUNGU kwa nini?
Mwisho tambua kwamba Ukimtumikia YESU KRISTO hakika MUNGU atakuheshimu.
Yohana 12: 26 ''Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba(MUNGU) atamheshimu. ''
MUNGU akubariki sana kama hujampa YESU maisha yako basi fanya hivyo leo maana saa ya wokovu ni sasa na Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu pia zingatia kwamba hakuna uzima wa milele kwingine nje na kwa BWANA YESU { Yohana 14:6 }
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.


BAADHI YA SHUHUDA.
1. Ubarikiwe sana Mtumishi,kwa maombi yako,niliyokushirikisha kwa ajili ya mama yangu ambaye ana tatizo la moyo kupanuka kwa mujibu wa madaktari,miguu ilivimba sana,alikuwa amepoteza fahamu,Asante YESU leo ana ufahamu,anajitahidi kutembea japo kwa kushikiliwa,maana alikua ananyanyuliwa,ingawaje hajaruhusiwa Hospital naamini ameruhusiwa kwa imani,hatakufa bali ataishi,na moyo wake utarudi kama alivyoumbwa maana yanaona matokea baada ya maombi.
MUNGU JEHOVAH akubariki kwa kubeba mzigo huu nami kwa maombi,naamini ukimtamkia kuishi huyu Mama yangu,ataishi.
Ubarikiwe sana.

2. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi Peter,
Asante sana kwa ujumbe mzuri.
Mtumishi nimemwambia mwanangu akutafute ili unisaidie maombi yake ,nimuda upi au siku ipi anaweza kukupata yuko hapo chuoni dar nitampatia na namba yako,
Nashukuru kwa maombi yako maana umeyafanya maisha yangu kuwa na amani na furaha ambayo ilikuwa imeishapotea siku nyingi, hadi leo imebaki historia midomoni mwa watu,kila mtu ananishangaa , Namshukuru sana MUNGU kwa ajili yako na sijui nitakulipa nini sitahahidi ila BWANA atatenda nipate kutoa shukrani kwako ,asante sana Mungu akubariki na kulinda na akupe nguvu ya kutuombea usichoke.
Namshukuru YESU kwa ajili yako leo na Mimi nasoma Biblia bila shida basi nami siku moja naomba nisimame mbele za watu nihubiri neno la Mungu
Amina
3. Namshukuru Yesu.
Asante pia Pastor Mabulla kwa kutuongoza katika mafundisho na njia sahihi katika uzima wa milele,kutuombea na kutufariji,hatukupungukiwa kitu katika familia.
Nimeona baraka nyingi zikitendeka kwangu ,zilikuwa zikimiminika za uponyaji,afya njema,mafanikio,ushindi,nimefunguliwa,nimepata ufahamu wa neno la Mungu kwa undani zaidi,zaidi ya yote baraka tele zinaendelea kumiminika,Mungu amenifungua na kunifanyia wepesi katika kila jambo ninalogusa,Barikiwa Pastor Mabulla,Mwenyezi Mungu ainue huduma yako,akumiminie mvua za baraka kwa kila unachogusa kwa utukufu juu ya utukufu,Ameen!!
4. Bwana YESU KRISTO apewe sifa milele Mtumishi wa MUNGU Peter. Habari ya asubuhi. Namtukuza sana MUNGU kwa ajili yako kupitia maombi ya kufunga mwezi mzima wa Februari, 2019 ambapo nami nilishiriki kuomba na kufunga siku zote. Ni kwa neema ya MUNGU tu, haikuwa rahisi sana kibinadamu kwa sababu ulipotushirikisha ndio tu nilimaliza kufunga siku saba ya maombi yangu binafsi hivyo nikaunganisha, lakini MUNGU aliniwezesha kufunga siku zote 28. Hakika nilimuona MUNGU kwa namna ya ajabu sana! Pamoja na shuhuda nyingi nilizonazo, nimebadilika sana kiroho kwa kiwango kikubwa... MUNGU amenibadilisha. Heshima, Utukufu na Sifa ni kwa KRISTO YESU pekee aliyeniwezesha. Nimetuma sadaka yangu ya shukrani Mtumishi wa MUNGU.
Nakutakia Huduma njema na MUNGU wa mbinguni aendelee kukutunza. Asante sana.

Comments