SHUHUDA MBALIMBALI.

SHUHUDA MBALIMBALI.
1. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Namshukuru sana Mungu maana somo lako liitwalo NJIA SABA ZA KUIACHA DHAMBI INAYOKUSUMBUA limebadili maisha yangu.
Somo hilo hakika limebadilisha maisha yangu. Ni muda mrefu nimesoma somo hilo na nilipozingatia tu njia hizo 7 sikunaswa kwenye dhambi hizo tena, maisha yangu yamebadilika kabisa, sio MTU wa dhambi tena.
Mungu akubariki sana Mtumishi.
2. Mtumishi wa Mungu namshukuru sana Mungu, mwanangu amepata choo.
Ilikuwa ni muda mrefu akisumbuliwa na kukosa choo ila Mungu ni mwema amemponya kwa maombi yako na najua hata tumbo amemponya.
Ubarikiwe
3. Bwana Yesu asifiwe mtumishi, namshukuru Mungu kwa maombi yako Bwana ametenda mengi, ndoto mbaya nilizokuwa naota sioni tena na pia kupitia maombi ya kufunga siku 28 nimekua sana kiroho tena nimepata amani moyoni, Mungu akubariki na akuzidishie.
4. Bwana yesu asifiwe!! Namshukuru Mungu Ameanza kutenda Miujiza katika biashara yangu!
Kwa sasa mambo yamekuwa mazuri sana.
5. Shalom mtumishi nimeamka vyema nadhani hata wewe umeamka mzima tumbo limeniachia toka saa tano usiku na hii asubuhi naliminya linaminyika jana kabla ya maombi tumbo halikuweza kuminyika kama kitovu kilikuwa chataka kutoka kabisa, kwa sasa niko vizuri na naamini nimepona kabisa asante mtumishi.
6. BWANA YESU apewe sifa Mtumishi wa MUNGU Peter Mabula napenda Leo hii kumshukru MUNGU kwa miujiza aliyonitendea kupitia kwa masomo yako na maombi yako pia yamenifanya niwe karibu na MUNGU na ninapo mwita anaitika na kunijibu hakika utukufu wake umetamalaki.
Siku chache zilizopita Bibi yangu alinipigia simu kuwa hali yake ni mbaya lakini kikubwa akaniambia kuna kitu kifuani kinamgonga kikubwa nilicho mwambia nilimwambia mimi kwasasa sina uwezo wakuja uko na wala hata nikija najua sitasaidia zaidi. Basi usiku ule nikafanya maombi kwa ajili yake lakini zaidi wakati nimelala usiku nilikuwa nimelala tu mwili lakini rohoni Roho Mtakatifu anazidi kuniongoza kuendelea kumwombea Bibi yangu usiku mzima siku hiyo ulikuwa usiku wa tofauti mno, Nilipoamka asubuhi nilimpigia kumjulia hali basi majibu aliyo nipa alinijibu naendelea vizur maana kilicho kuwa kikinigonga kifuani kimeisha nilijihisi mwenye furaha na kumtukuza MUNGU mno.
1kor 15:57 Lakina MUNGU na ashukuriwe atupaye kushida kwa Bwana wetu Yesu Kristo ndo neno napenda sana kutumia na siku hiyo ndio nililitumia katika maombi.
Jambo lingine ambalo pia napenda kumshukru MUNGU ilikuwa ni juzi usiku wa manane ambapo ndoto mbili ziliambatana pamoja ( sitazitaja) lakini ya kwanza ilikuwa ya ushindi lakini ya pili iliyofuatia ilikuwa ya shetani na mapepo wake wachafu wakati naenda kuangamiza katika hiyo ndoto Roho Mtakatifu akanitokea akaniambia acha na amka usali na Mimi haraka nikaamka nikaanza kukemea baadaye nikalala lakini baada ya muda fulani kikatokea kitu kama pembe kikaingia sehemu ya moyo kabisa nilipo kuwa na vuta hewa na kutoa hewa (kupumua) nilikuwa napata maumivu makali sana yasiyo ya kawaida nilikosa tu kulia na kupiga kelele nilikuwa naomba muda mwingine naishiwa ata na nguvu za kuomba kwasababu ya maumivu niliyo kuwa nayapata nilichosema nilisema (sitakufa) ata kama nikipata maumivu kiasi gani, takribani kama Masaa 3 kitu hicho kikapotea nikawa nasikia maumivu kidogo sana kwa mbali bado niliendelea kusema neno la 1kor 15:57
namshukru MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo kwa Utukufu wake mkuu na pia nimshukru jinsi anavyokutumia wewe Mtumishi Mabula kuinua roho zetu, MUNGU azidi kukufunulia zaidi na akuzunguke pande zako zote kama alivyo mzunguka Ayubu AMEN
7. Mtumishi BWANA YESU asifiwe sana. pia nashukuru kwa maombi yako. pia napenda kukupa ushuhuda huu. ilikuwa mwezi wa kwanza. ninakupa mahitaji ya wamama wawili. mmoja ambaye mume wake alietekwa na mwanamke wa nje ya ndoa yake.
sasa MUNGU wa mbinguni amejibu maombi yako ulio kuwa unamuombea. week jana jumapili mume wake alikuja kanisani nakutubu mbele za kanisa nzima. nakusema alikuwa hajui anachokifanya. sasa amemrudia MUNGU wake pamoja na mke wake wa ndoa. alimuunguzia yule mwanamke wa pili vitu vyote nakusema anarudia kwenye ndoa yake. so MUNGU apewe sifa sana.
8. Shalom Mtumishi, Mimi naishi Kilimanjaro nafuatiliaga sana mafundisho yako facebook, kweli yananibariki sana. Niliwahi kuugua saratani ila kwa jinsi nilivyokuwa nafuatilia masomo yako yananitia moyo hakika niliuona mkono Wa Mungu ukininyanyua kitandani. namshukuru Mungu sasa naendelea vizuri na nimepona kabisa.
Ombi langu ni moja naomba uniombee nipate mume mwema na pia Mungu anipe watoto naamini Mungu ni mwamimifu kama aliweza kunitoa kitandani basi atanipa mume na familia bora.


1. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi Mabula, namshukuru Mungu nimepona kabisa, mimi ni yule niliyekuwa na tatizo la kusumbuliwa na ziwa pia nimefunguliwa kwa namna mbalmbal hakika nimemuona Mungu na akutumie zaidi kuwaponya watu,Mimi binafsi nina mengi ya kushukuru lakini barikiwa Mtumishi wa Yesu.
2. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi, asante kwa maombi yako ninaona mabadiliko ndani yangu , naweza kufunga sasa,
Haikuwa hivyo kabla, Mungu akubariki sana.

3. BWANA YESU asifiwe,mtumish mabula, yaani tangu umeniombea kuhusu ndoto mbaya,sijaota tena.
MUNGU akubariki sana.
4. Bwana Yesu asifiwe mtumishi, namshukuru Mungu naendelea vizuri kwa maombi yako naona Bwana ametenda mengi katika maisha yangu. Nina rafiki yangu anapitia mapito magumu Mno nimempatia namba yako atakupigia leo nakuombea sana Mungu akupe kibali cha kumsaidia. Anaitwa MWANAIDI.

Comments