SHUHUDA MBALIMBALI.

SHUHUDA MBALIMBALI.
1. Bwana asifiwe Mtumishi Mabula!.
Namshukuru Mungu kupitia masomo yako uliyotoa mwanzoni mwa mwaka huu nimepata haki yangu kwa uwezo wa Mungu,kuna baba nilimpa pikipiki yangu aendeshe kama boda boda, akaamua kutokomea na kuhama kabisa, kupitia masomo ya kuchana kalenda za kipepo na matukio ya kipepo mwaka huu nikawa natumia hizo points ulizotoa katika maombi hatimaye leo nimeipata kwa msaada wa Mungu! Bila Mungu nisingeipata aiseee maana alijificha mbali mno ila Mungu kammulika na haki yangu nimeipata,.
Mungu azidi kukutumia.

2. Shalom Mtumishi wa Mungu
Kwanza kabisa napenda nimshukuru Mungu sana kwa ajili yako, pia napenda nikushukuru kwa mafundisho yako mazuri kwenye ukurasa huu ambao kiukweli umenifundisha mengi Sana na kunijenga kiroho.
Mwezi uliopita mke wangu alikuandikia meseji kuwa yeye Ni mjamzito na anaitaji maombi.
Ulikuwu bize ukamwambia tuombe jioni na jioni ilipofika simu yako ilikuwu bize muda wote.
Nilimkumbusha mke wangu kuwa Mtumishi alikuwa anataka akuombee na kwa wakati huu simu yake iko bize Na huduma ,basi Ni vyema uamini tu nawe utajifungua salama maana kama uliamini kuwa akikuombea utaponywa hakika na hata Sasa itatokea kwa jna la Yesu.
Kweli aliamini na namshkuru Mungu alijifungua salama mtoto wa kiume
Jina la BWANA lihimidiwe milele na milele yote
Amen.
3. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu,nimekuandikia historia ya familia yangu kwa sehemu kwa njia ya message
Pia mtumishi nilivyofunga maombi ya siku saba,nikamwambia Mungu ,naomba uniinulie mtumishi atakae nitoa hapa nilipo yaani atakaeniingiza kwenye ndoa takatifu,tena siku hiyo nikawa nadeki nikawa naongea mwenyewe nasema Mungu naomba uniinulie mtumishi uliyemkusudia atakesema neno juu yangu katika swala la ndoa,ili niweze kufunga ndoa takatifu,na rohoni nikawa nasikia sauti inaniambia nikupigie simu,mimi nikawa nakasema siku ya saba nitakavyomalizia maombi ndiyo nitakupigia simu,siku hiyo hiyo niliyokuwa nawaza hayo,ukaniandikia message nipigie simu nikuombee,nikapata jibu langu hapohapo nilikuwa nimeongea na Mungu,la kuniinulia mtumishi wa kunitoa hapa nilipo,hakika Mungu ni mwaminifu sana ,na yuko karibu sawasawa na neno lake katika Yeremia 23:23 huo ni ushuhuda Mtumishi wa Mungu
Maana nilikaa mahali nikasema mwaka unaisha,sioni matokeo,mwaka mwingine hivyo hivyo,nikasema hapana,mwaka huu 2019 sitaenda nao kwa mazoea,Ninataka Mungu aniinulie Mtumishi atakaenitoa hapa nilipo mpaka nifunge ndoa takatifu,namwamini Mungu huu mwaka 2019 Mungu atanitendea matendo makuu,na nitasema hakika ni Yeye Mungu aliye Mkuu aliyenitendea,Amina
4. BWANA YESU APEWE SIFA MTUMISHI naendelea kumtukuza Mungu hali ya mume wangu inaimarika kesho au kesho kutwa anaweza kuruhusiwa kutoka hospital asante kwa maombi mtumishi, ninaanda shukrani mbele za Mungu nikishaituma nitakupigia pia tuombe maombi ya kushukuru.
Ninamshukuru Mungu maana hali ya mume wangu ilikuwa mbaya kupita kawaida.


SHUHUDA MBILI.
1. Shalom Mtumishi. Nashukuru Mungu Lile Tatizo Nililokuambia Uniombee Limekwisha, Unakumbuka Nilikuambia Nina Vita Kali Sana Kiroho, Kuna kuna roho ya kupinga nisimuabudu Mungu, Kila Nikisoma Bibilia Au Nikiomba Kuna roho ilikua inataka nimkane Mungu Ilinisumbua Sana, Mungu Amenisaidia,
Ubarikiwe Sana, Ahsante, BWANA Akuinue Zaid, Jina la YESU KRISTO LIHIMIDIWE.
2. Shalom Mtumishi.
Nakumbuka Nilikupa Hitaji La Mwanangu,ambae Alikuwa Anamaliza Form 4 Mwaka Jana,alikuwa Anasumbuliwa Usingizi Kila Akisoma,na Kukataliwa Na Wenzie Katika Study Group,hayo chini Ndio Matokeo Yake.Namshukuru Sana BWANA,Nakushukuru Sana Wewe Ambae Ulinibeba Katika Maombi Kwa Ajili Ya Kijana Wangu.Sina La Kukulipa,yuko BWANA,atakulipa.
Usichoke Katika Kunibeba Hata Kwa Mengine.
Matokeo amepata division two ya 20
CIV - 'C' HIST - 'C' GEO - 'C' KISW - 'C' ENGL - 'C' PHY - 'D' CHEM - 'C' BIO - 'B' B/MATH - 'F'
Ubarikiwe Sana na BWANA.

Comments