![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu.
Leo ngoja nikuletee funuo chache za ki maombi zilizonitokea Mimi mwenyewe Peter Mabula.
Siku moja nilipata ufunuo huu nikiwa katika maombi.
Kwa sauti nilipewa maandiko haya.
ZABURI 104:4. OBADIA 1:18,MWANZO 3:24
Kwa sauti nilipewa maandiko haya.
ZABURI 104:4. OBADIA 1:18,MWANZO 3:24
✓✓Nilipoangalia maandiko hayo nilijifunza mambo kadhaa ya kunisaidia katika maombi yangu dhidi ya nguvu za giza nilizokuwa napambana nazo.
Baadhi ya niliyojifunza ni haya.
1. MUNGU huwafanya Malaika wake kuwa kama upepo, hivyo unaweza kujikuta unalindwa sana wewe Mteule wa KRISTO, hata kama huoni anayekulinda ila unaona tu upepo.
Zaburi 104:4 "Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali."
✓✓Hao adui zako ukiwa muombaji mzuri,hao adui zako wanaweza kupigwa na silaha zao za kichawi huku hawajui ni nani anawapiga,
✓✓Kumbe wewe unaomba katika jina la YESU KRISTO na Malaika wanaoonekana kama upepo wako eneo la tukio kuharibu nguvu za giza zinazopambana na wewe.
2. MUNGU huwafanya watumishi wake waaminifu kuwa kama moto au Mwali ya moto mbele za adui zao.
Zaburi 104:4 " ......... Na watumishi wake kuwa moto wa miali."
✓✓Unaweza ukaomba MUNGU akakufanya kama mwali wa moto mbele za nguvu za giza wanaokuwinda.
Nina shuhuda nyingi katika hili.
Dada mmoja alihamia Kanisani kwetu na kumbe ni mchawi gwiji aliyerithishwa uchawi na Bibi yake.
Baada ya kuhamia Kanisani jumapili iliyofuata Mchungaji wakati anaombea watu yule Dada alianguka mapepo na kisha kuanza kufanya ishara za kichawi, ilibidi Mchungaji aniambie Mimi na baadhi ya watumishi tumpeleke ofisini ili tukamuombee wakati ibada ikiendelea, tulienda na kumwombea kisha akafunguliwa, baada ya kufunguliwa nilimuuliza kuhusu uchawi akasema mambo mengi sana ya ajabu, akasema kweli yeye ni mchawi na hadi alishaua kichawi watu wengi na hasa watoto wakiwa tumboni amewahi kuwaua na kuwala nyama kichawi. Kisha nikamuuliza kuhusu hapo Kanisani akasema yeye huwa anakuja ibadani na dawa zake za kichawi ila huwa haingii nazo ndani ya jengo la Kanisa, akasema alipofika Kanisani alianza mbinu za kuwaroga baadhi ya watu lakini alipojaribu kumroga Mchungaji na baadhi ya watendakazi alishindwa maana alimuona mchungaji na sisi watendakazi tukiwa tumezungukwa na moto mkali sana ambao hautuunguzi ila unatulinda dhidi yake, alipojaribu zaidi akawa anapata mapigo hivyo akaacha.
Binti mwingine ambaye naye alikuwa mchawi anayesimamia misukule ya Babu yake siku moja alisema kwamba alijaribu kuniroga Mimi ila akashangaa kwamba aliponijia tu aliniona nimezungukwa na moto mkali wa ulinzi wa MUNGU ambao alipojaribu kupambana kichawi aliishiwa nguvu, mwingine alisema kwamba alipomjaribu Mtumishi mmoja aliishiwa nguvu hadi za kuondoka hivyo alijikuta yuko hapo hadi kunakaribia kukucha yaani kunakaribia asubuhi ndipo akaondoka kama mgonjwa.
Nina shuhuda nyingi sana katika hili, baadhi ya shuhuda ni zangu mwenywe na nyingine za watumishi wa MUNGU wengine ila ninachotaka ujifunze ni kwamba MUNGU anaweza kumfanya Mtumishi wake kuwa kama moto mkali ambao mchawi au jini hawezi kusogea, ndugu inakupasa kuomba leo ili MUNGU akufanye kuwa mwali wa moto mbele za mawakala wa shetani wanaokufuatilia, inawezekana kuwa kama mwali wa moto katika jina la YESU KRISTO Mwokozi.
3. MUNGU anaweza kuifanya nyumba yako kuwa mwali wa moto mbele ya nguvu za giza.
✓✓MUNGU anaweza akaifanya familia yako kuwa moto mbele za mawakala wa shetani wanaojaribu kuiroga au kuiharibu familia hiyo.
Obadia 1:18 "Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo."
4. MUNGU anaweza kuweka ulinzi katika eneo fulani.
✓✓MUNGU anaweza kumfukuza mtu katika eneo, anaweza hata kumfukuza adui.
◼️MUNGU anaweza kuweka Malaika ili kulinda eneo fulani,wanaweza wakalinda Kanisa au mtu au familia, hakikisha tu una sifa za kulindwa na Malaika wa MUNGU yaani umeokolewa na YESU KRISTO na unaishi maisha matakatifu ya Wokovu huku ukimtumikia MUNGU na ni muombaji.
Mwanzo 3:24" Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima."
✓✓Kama kuna kitu kilinishtua katika ufunuo wa andiko hili ni "Upanga wa moto unaojigeuza huko na huko ili kulinda"
✓✓Kwa kusoma kwangu Biblia niligundua kuna panga nyingi za MUNGU ambazo kwa hizo zinaweza kuharibu na kuangamiza nguvu za giza.
✓✓Kuna upanga mkali mkubwa wenye nguvu(Isaya 27:1)
✓✓Kuna upanga unaokata haraka kama umeme(Ezekieli 21:15)
✓✓Na panga zingine nyingi kulingana na maandiko na ufunuo unaotokana na maandiko lakini upanga wa Mwanzo 3:24 ni moja ya panga hatari sana, ni upanga wenye moto unaotembea huko na huko kumkabili adui.
Ni upanga ambao hauhitaji kubebwa kwani hata wenyewe unaweza kutembea na kuzunguka huko na huko ili kumkabili adui.
Baada ya ufunuo huo niliomba sana ili niwe mwali wa moto mbele ya wachawi, waganga, wanadamu wanaotumika kipepo,majini,mizimu na kila nguvu za giza.
Niliomba familia yangu izungukwe na moto wa MUNGU ili nguvu za giza zisivamie.
Nikitumia upanga wa MUNGU ulio katika Mwanzo 3:24 ili kuwafekelea mbali maroho wa kuzimu.
Namshukuru sana MUNGU maana niliona ushindi dhahiri.
Nimetamani kukushilikisha leo ufunuo huu wa sauti inayotaka katika maandiko ili yamkini kuna kitu utajifunza, utatiwa moyo, utaongezewa imani, utapata mbinu mpya za maombi unapokabiliana na mawakala wa shetani na ujumbe huu utakuimalisha kiroho na inawezekana kabisa ujumbe huu utafanya kazi kubwa kwako hadi siku moja utanipa ushuhuda mzuri.
Inawezekana una msukumo wa maombi leo na hujui utaomba nini, ila kupitia ujumbe huu umejua uombe nini ili adui aliyekuzoea asikuzoee tena, akuogope sana maana atakutana na moto wa MUNGU na huku silaha za MUNGU za vita ya kiroho zikimpinga huyo adui katika kiwango ambacho hatakufuatilia tena,hatafatilia familia yako tena, hatafuatilia uzao wako, hatafuatilia kazi yako,uchumi, afya yako na kila baraka yako.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments