UKIFUATA UOVU UMEFUATA UHARIBIFU WAKO.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu.

Karibu nikujuze Neno hai la MUNGU aliye hai.

Mtu anayefuata maovu huifuata mauti yake mwenyewe.

Mithali 11:19 "Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

■Mauti ni uharibifu hivyo mtu anayefuata maovu huufuata uharibifu wa maisha yake.

Je wewe unafuata uovu ili uvune uharibifu?

Yapo maovu ya namna nyingi na hayo maovu mtu akiyafuata anakuwa ameufuata uharibifu wake, ngoja nikupe mifano kadhaa kuhusu uovu mmoja tu uitwao  UASHERATI/UZINZI na namna kuifuata dhambi hiyo ni kufuata uharibifu wako.

1. Mfano mwanamke ambaye hujaolewa unapofanya dhambi ya uasherati kisha ukapata mimba na kuzaa huku aliyekubebesha mimba ameshakuacha siku nyingi, ujue wakati ukihitaji mume wa kukuoa kuna kundi la wanaume hawatataka kufunga ndoa na wewe kamwe, kundi hilo ni lile wasemao "Siwezi kuoa mwanamke mwenye mtoto", sasa kama anayetakiwa kufunga ndoa na wewe ndio mwanaume wa kundi hilo ujue hatakubali kamwe kukuoa, huo ndio uharibifu unaotokana na kufuata uovu.

Mithali 11:19b "Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

2. Mwanamke unapofanya dhambi ya uasherati kisha ukapata mimba na kuitoa kinachokupata ni laana ya kumwaga damu isiyo na hatia.

Na chanzo kimojawapo cha laana ni kumwaga damu isiyo na hatia, haijalishi ni damu ya nani.

Mwanzo 4:10-11 " Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;"

Laana ni nini?

Maana mojawapo ya laana ni adhabu za kiroho zinazotokana na kosa, adhabu hizo ndio uharibifu/mauti unaotokana na kufuata dhambi.

Mithali 11:19b "Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

3. Uasherati na uzinzi hutengeneza maagano ya kishetani, maagano hayo huzaa uharibifu/mauti.

1 Wakorintho 6:16 " Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? ....."

Kuna watu inabidi watumie nguvu nyingi sana katika maombi ndipo wapate wenzi wa ndoa, kutumia muda mrefu kuomba na kujifungua vifungo kwa sababu ya  uharibifu unaotokana na kufuata uovu, inabidi kuvunja maagano ya kipepo maana hiyo maagano ndio uharibifu wenyewe.

Mithali 11:19b "Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

4. Wachumba wengi wanaoanguka dhambini huishia kuachana kwa maumivu, huo ndio uharibifu unaotokana na kuifuata dhambi.

Mithali 11:19b "Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

5. Kuna watu kwa sababu ya kufuata uzinzi au uasherati hujikuta wamepata magonjwa ya zinaa, huo ndio uharibifu unaotokana na kufuata dhambi.

Mithali 11:19b "Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

6. Yuko mtu anaweza kuisaliti ndoa yake kwa kuzini na mke/Mume wa mtu na anakamatwa na kupigwa au kufanywa kulema, hicho kilema cha namna hiyo ni uharibifu unaotokana na mtu kufuata dhambi ya uzinzi.

Yupo mwanaume alikamatwa akizini na mke wa mtu na akapewa adhabu ya yeye na huyo mwanamke kutembea kijiji kizima wakiwa uchi na baada ya hapo ndoa zao kila mmoja zikafa, huo ndio uharibifu unaotokana na mtu kufuata dhambi.

Mama mmoja alifariki kwa mshtuko baada ya kumfumania mumewe akizini na rafiki yake, huo ndio uharibifu unaotokana na mtu kufuata dhambi, uharibifu huo ulitengeneza na mwanaume aliyeamua kuifuata dhambi, na ndoa yake ikaishia pale huku akisababisha kifo.

Mithali 11:19b "Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

7. Unaweza kuwa mwasherati kiasi ambacho hakuna mtu atataka kufunga ndoa na wewe, kukosa wa kufunga na wewe ndoa kwa sababu wewe ni mwasherati, huo ndio uharibifu unaotokana na mtu kufuata dhambi.

Mithali 11:19b "Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe."

Nimekujulisha dhambi moja tu na jinsi ambavyo dhambi hiyo inaweza kutengeneza uharibifu kwa mhusika.

Lakini Dhambi zote ni njia ya uharibifu.

Kama wewe labda unahusika na eneo mojawapo katika hayo 7 niliyokueleza kuhusu madhara ya uzinzi na uasherati basi tubu na acha dhambi hiyo kuanzia leo, fuata maombezi na ukawe muwazi kwa watumishi wa MUNGU ili wakuombee na utafunguliwa vifungo hata vile vilivyotokana na dhambi uliyoifanya.

Mwenye sikio la kusikia naamini amesikia na atatubu na kuachana na dhambi hiyo kuanzia leo, ataokoka na kufanyika kiumbe kipya kisichohusika na uzinzi wala uasherati.
MUNGU akubariki sana kama ukifanyia kazi.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments