![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Uovu na dhambi husafishwaje?
Mithali 16:6 "Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu."
Biblia inatoa majibu ya namna ya kusafishwa uovu au dhambi.
1. Uovu na dhambi husafishwa kwa rehema.
✓✓Yaani kwa kutubu mbele za MUNGU katika KRISTO YESU na kuomba msamaha na kuamua kuwa mtii na mwaminifu kwa MUNGU.
MUNGU siku zote Yuko tayari kumrehemu Mtu anayeomba rehema kwake.
Isaya 55:7 "Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa."
◼️Rehema ni Neema anayopewa Mtu na MUNGU, rehema ni msamaha wa MUNGU bila kuangalia ubaya uliotendwa na Mwanadamu anayetubu.
✓✓Toba ya kweli ni kutubu mbele za MUNGU kupitia YESU KRISTO.
Kwanini ni toba katika KRISTO YESU tu ndio inapokelewa na MUNGU hata mtu anasamehewa na kuwa safi?
Ni kwa sababu ni kwa sababu ni damu ya YESU KRISTO pekee ndio inayoweza kufuta dhambi za mtu na kumtakasa mtu huyo.
1 Yohana 1:7" bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."
2. Kweli husafisha uovu.
Uovu na dhambi husafishwa na kweli ya MUNGU.
◼️Kweli ni Neno la MUNGU.
Yohana 17:17 " Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli."
◼️Neno la MUNGU linatakasa kupitia mtu binafsi kuamua kulisoma kisha kulitii na kisha kuliishi.
3. Kwa kumcha MUNGU hupelekea mtu kusafishwa uovu.
✓✓Kumcha MUNGU kunaanzia na kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi kisha unaanza MUNGU na Neno lake.
Kumb 13:4 " Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye."
4. Kujiepusha na uovu.
Zaburi 34:14 " Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie."
Ndugu Naamini umeelewa lakini rohoni mwangu naambiwa nimwambie Mtu mmoja maneno haya hapa chini.
"Wewe ulikuwa mtumishi wa MUNGU ila kwa sasa umekuwa mtumishi wa shetani, umekuwa wakala wa shetani. Umemsahau MUNGU wa wokovu wako, umemwacha YESU KRISTO Mwokozi wako, wewe unaona ni sawa tu lakini si sawa hata asilimia moja, dhambi ya uzinzi kwako ni jambo dogo tu na umeshawahi hata kunywa pombe, umesahau YESU alikuokoa?
umesahau YESU alivyokusaidia usifukuzwe kazi?
kwa sasa kwa sababu unapokea mshahara mzuri huna haja tena na YESU?
Lakini kumbuka kwamba unamhitaji YESU zaidi ya unavyoihitaji kazi yako, ndugu tubu haraka na rejea kwa upya kwa YESU KRISTO Mwokozi, mimi sijui lolote kuhusu wewe hata kama nimewahi kukuombea kwa MUNGU ili akuepushe na mabaya na akakuepusha. Nimepewa ujumbe huu juu yako usiku saa tisa usiku , unaweza kuchagua uzima au laana, mimi nakuomba chagua uzima ili ukaishi,
Kumbu 30:19 "Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;"
Mchague YESU kuwa Mwokozi wako, ishi maisha matakatifu na mtumikie yeye daima.
Nisamehe kama nimekukosea ila nimefunuliwa hayo kuhusu wewe na nakushauri tengeneza na MUNGU haraka sana maana sijui ni nini kiko mbele yako.
Tengeneza maisha yako, hutakufa, utapona, mkaribishe Bwana YESU KRISTO atawale maisha yako.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments