![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu.
◼️Mimi sikai katikati ya waliookoka bali nataka siku zote za maisha yangu niwe sehemu ya waliookoka.
Hata Wewe rafiki yangu Inakupasa kuwa namna hii.
✓✓Sitaki niwe Mtumishi wa MUNGU tu bali nataka siku zote nimtumikie MUNGU huku nikiishi maisha matakatifu katika KRISTO.
Hata wewe rafiki yangu Inakupasa kuwa namna hii.
1 Wakorintho 9:26-27 " Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa."
✓✓Wako watu wako katikati ya waliookoka ila wao hawajaokoka.
✓✓Unaweza kukuta familia ya Mchungaji aliye safari ya mbinguni ni Mchungaji tu lakini mwenzi wake na watoto hawana mpango wa kwenda Mbinguni, wao huenda Kanisani kwa sababu wanakaa kwa Mchungaji, wanaweza kuimba Kwaya n.k lakini huwa wanasali kwa sababu tu ya Mchungaji, hao ni watu walio katikati ya waliookoka ila wao hawajaokoka.
✓✓Yuko mtu anaweza kuwa Kanisani miaka hata 7 lakini yeye haishi maisha matakatifu, huyo yuko katikati ya waliookoka ila yeye hajaokoka.
◼️Kumbuka waitwao ni wengi ila wateule ni wachache.
Mathayo 22:14 "Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache."
✓✓Unaweza kabisa kukuta Kanisa lina watu 700 lakini ni watu 50 ndio waenda mbinguni maana ndio wanaishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi, waliobaki wote wao wapo katikati ya waliookoka ila wao hawajaokoka.
✓✓Inawezekana kabisa kuna mahali katika Kanisa unaweza kukuta aliyeokoka ni Mchungaji na Mama Mchungaji peke yao maana ndio wanaishi maisha matakatifu, waliobaki wote wao wapo katikati ya waliookoka ila wao hawajaokoka, wamekalia tu uzinzi,wizi na uongo na dhambi zingine.
1 Wakorintho 5:1-2 "Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo."
◼️Ndugu unayesoma somo hili nakuomba sana kuanzia leo usiwe katikati ya waliookoka bali okoka.
✓✓Ndugu usikae katikati ya kundi au katikati ya Kanisa tu bali fanyika Kanisa safi na takatifu la KRISTO YESU.
1 Wakorintho 1:2 "kwa kanisa la MUNGU lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika KRISTO YESU, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu YESU KRISTO kila mahali, Bwana wao na wetu."
Ndugu, nini nataka kusema kwako?
✓✓Usiishi na watu waliookoka huku wewe mwenyewe hujaokoka.
✓✓Usiwe mtu wa ibada na kumbe huendi ibadani kumtafuta MUNGU.
✓✓Usiwe tu miongoni mwa wanaosema "Bwana YESU asifiwe" huku wewe mwenyewe
YESU KRISTO sio Bwana na Mwokozi wako.
✓✓Ndugu usiwe mhubiri mtenda dhambi.
✓✓Usiwe mwanakwaya mtenda dhambi.
✓✓Usiwe mwimbaji mtenda dhambi.
✓✓Usiwe Mchungaji mtenda dhambi.
✓✓Usiwe Nabii mtenda dhambi.
✓✓Usiwe Mtume mtenda dhambi.
✓✓Usiwe Mwalimu mtenda dhambi.
✓✓Usiwe Mwinjilisti mtenda dhambi.
✓✓Usiwe Mshirika Kanisani ila mtenda dhambi.
✓✓Usiwe Mkristo asiyemtii KRISTO na injili yake.
◼️Ndugu usiwe katikati ya waliookoka huku wewe mwenyewe hujaokoka.
✓✓Usiwe katikati ya waliookoka huku wewe mwenyewe huishi maisha yawapasayo waliookoka.
✓✓Kuna mtu yuko miongoni mwa wanakwaya mashuhuri Kanisani ila hajaokoka.
✓✓Kuna mtu ni miongoni mwa waimbaji mashuhuri wa Nyimbo za Injili na inawezekana yeye huimba nyimbo zenye ujumbe sana ila yeye sio miongoni wao waliookoka.
1 Wakorintho 3:3 "kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?"
◼️Ndugu, Wokovu sio wa kundi bali Wokovu ni wa mtu binafsi.
✓✓Mnaweza kuwa Kanisani watu 100 na walioamua kuokoka na wanaishi maisha matakatifu ni 10, waliobaki hawajaokoka, wao wanaishi katikati ya waliookoka ila wao hawajaokoka, ndugu naomba usiwe wewe bali wewe okoka na ishi maisha matakatifu ya Wokovu.
Ndugu nasema usiseme tu "Bwana YESU asifiwe" huku YESU bado hajawa Mwokozi wako, bali okoka ndipo YESU KRISTO atakuwa Bwana na Mwokozi wako.
Mwenye sikio la kusikia na asikie leo.
Mathayo 13:9 "Mwenye masikio na asikie."
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments