![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Natamani kila mtu asome somo hili mwanzo hadi mwisho maana kuna kitu chake ROHO MTAKATIFU amemuandalia kupitia somo hili la ufunuo wake.
Neno la MUNGU la Leo linasema "Usipobarikiwa mjini utabarikiwa mashambani."
Tuanze na maana ya neno"Baraka"
◼️Baraka za MUNGU ni nini?
1. Baraka za MUNGU ni mambo mema akupayo MUNGU.
Wagalatia 3:14" ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika YESU KRISTO, tupate kupokea ahadi ya ROHO kwa njia ya imani."
2. Baraka za MUNGU ni matokeo mazuri ya jambo jema ulilolifanya katika MUNGU.
Tito 2:13" tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu;"
3. Baraka za MUNGU ni hali ya ustawi na mafanikio anaokupa MUNGU katika jambo fulani kutokana na Neema ya MUNGU.
Waefeso 1:3 "Atukuzwe MUNGU, Baba wa Bwana wetu YESU KRISTO, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake KRISTO;"
4. Baraka za MUNGU ni uwezeshaji wa MUNGU unaokupatia wingi wa vitu.
Ufunuo 7:12 "wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina MUNGU wetu hata milele na milele. Amina."
◼️Sasa kwanini nimesema Usipobarikiwa mjini utabarikiwa mashambani?
Maana yake ni hii
✓✓Usipopata baraka mjini hamia mashambani utabarikiwa.
Inawezekana ni Neno gumu sana kwako ila nisikilize itakusaidia.
Kumbu 28:3 "Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani."
◼️Maana yake MUNGU anaweza kuachilia baraka popote iwe ni mjini au vijijini kwenye mashamba.
✓✓Maana yake ukiona jambo moja limeshindikana kukuletea baraka uitakayo hamia jambo lingine.
Mfano kama biashara yako haikulipi hamia kwenye kilimo.
Kama kilimo hakikulipi hamia biashara, kama biashara haikulipi hamia ufugaji.
✓✓Kama ajira haikulipi basi jiajiri, baraka za MUNGU hazijaachiliwa katika eneo moja tu bali zimeachiliwa maeneo mengi sana.
Ilimradi ni unafanya kazi halali mbele za MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi.
◼️Na njia mojawapo ya kufanikiwa kama wewe ni muombaji basi ni kumsikiliza ROHO MTAKATIFU anakupa amani katika jambo gani la kufanikiwa kwako.
✓✓Sina maana kwamba lazima ukaishi vijijini tu ila nina maana kwamba baraka za MUNGU ziko katika maeneo mengi, sio eneo moja tu.
Kama sio ofisini kuna kilimo, kama sio kilimo kuna biashara.
✓✓MUNGU anaposema kwamba atakubariki mjini na atakubariki mashambani ina maana ya kwamba baraka za MUNGU zimeachiliwa maeneo mengi tu, sio eneo moja tu.
✓✓Kumbuka pia ROHO MTAKATIFU anakusaidia kuliendea eneo ambalo utakuwa salama, utakuwa na muda wa kumwabudu MUNGU Baba, utakuwa na muda wa kumtumikia Bwana YESU KRISTO na utakuwa na mafanikio ya kiroho na kimwili.
Kumbu 28:8 "BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako."
◼️MUNGU anaweza kuiamuru baraka ije kwako haijalishi uko wapi au uko katika ardhi ya eneo gani.
✓✓Andiko lina kumb 28:8 lina maana pia kwamba "MUNGU atakubarikia katika ardhi akupayo" hivyo husika na maombi ya kuombea ardhi unayoishi.
Mawakala wa shetani wakati mwingine huifunga ardhi kipepo hivyo kama unaishi juu ya ardhi hiyo huwezi kufanikiwa.
Unaweza kuwa mjini na umefungua duka, na ardhi ya eneo hilo imefungwa kishetani na mawakala wa shetani, usipoombea ardhi hiyo na kuikomboa kwa damu ya YESU KRISTO ujue utasumbuka sana kufanikiwa.
✓✓Unapoombea baraka zako kumbuka sana kuombea ardhi ya eneo lako la kazi ndipo utaiona baraka yako.
✓✓Pamiliki hapo kwenye ulimwengu wa roho ili adui asipafunge ili wewe usifanikiwe.
Kumbu 11:24 "Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu."
Kila mtakapopakanyaga patakuwa penu maana yake mtamzuia adui kupafunga hapo wala kupateka.
Inawezekana wewe unafanya kazi ofisi Fulani na ardhi ya hapo imefungwa kipepo na adui, ndio maana hufanikiwa.
Inawezekana wewe unalima katika ardhi iliyofungwa.
Inawezekana wewe unaishi katika ardhi iliyofungwa.
Kumbuka mafanikio yako yote haijalishi upo wapo, hayo mafanikio yanategemea ardhi iwe kwa ofisi, biashara, kilimo, usafirishaji, uchuuzi n.k
✓✓Kumbuka tu pia kwamba baraka zako zinaambatana na kufanya kazi halali, kisha uwe mtoaji wa fungu la kumi, uwe muombaji na unayeishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU.
✓✓Najua ndugu unazihitaji Baraka za MUNGU hata Mimi Peter Mabula nazihitaji sana Baraka za MUNGU wa Mbinguni.
Sasa Ninachoweza kukuambia ni kwamba jiweke wakfu kwa MUNGU ili upokee baraka za MUNGU.
Kutoka 32:29 "Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa BWANA leo, naam, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo."
✓✓Jiweke wakfu kwa wewe kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU.
✓✓Jiweke wakfu kwa maombi hasa maombi ya toba na utakaso.
✓✓Jiweke wakfu kwa kutokufuata machukizo ya kidunia.
✓✓Jiweke wakfu ili upokee baraka ya MUNGU kutokana na maombi yako na kazi yako njema unayoifanya katika MUNGU Baba.
◼️Ni furaha kuwa na baraka ya MUNGU maana baraka ya MUNGU huwa haiambatani na huzuni.
Mithali 10:22 "Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo."
✓✓Watu wengi sana wanahitaji baraka lakini wengi hutafuta baraka za shetani na sio za MUNGU.
Ukiona mtu anaenda kwa mganga ujue mtu huyo anatafuta baraka ya kishetani, hata huyo mganga mtoa baraka hana hizo baraka hivyo kinachofuata ni kuwaunganisha watu na nguvu za giza ili kuwatenga na MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi.
✓✓Ndugu, wewe zihitaji baraka za MUNGU na sio za shetani.
✓✓Baraka za MUNGU huwa haziambatanishwi na huzuni, ni baraka safi katika mazingira salama na ya kitakatifu.
✓✓Baraka za MUNGU ziko katika makundi matano ambao ni baraka za ndoa, afya, uchumi, uzao na baraka za kibali.
Nini ufanye kwenye maombi?
1. Tubu kwa ajili ya ardhi ya eneo lako la kazi.
2 Nyakati 7:14" ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao."
Kuiponya nchi yao maana yake kuiponya ardhi yao.
2. Tubu kwa ajili ya nafasi uliyopo ambayo kuna mtu au watu walishawahi kukaa katika nafasi hiyo.
Matendo 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"
Ngoja nikupe mfano hai.
Mimi Peter Mabula kuna kipindi niliteuliwa kuwa Mzee kiongozi wa Kanisa, Kanisani kwetu.
Baada ya kupewa nafasi hiyo kwa muda mrefu nilipata ufunuo wa maombi ya toba kwa ajili ya nafasi/kiti cha uzee kiongozi Kanisani hapo, nilitubu pia kwa ajili ya makosa ya walionitangulia ili nisitembee kwenye makosa yao(hata kama siyajui makosa yao hata moja)
Sasa kama Mimi nilipewa ufunuo wa kuombea kiti/nafasi ya cheo cha kikanisa vipi kwa wewe uliyechukua nafasi ya mtu serikalini, kwenye kampuni n.k?
Vipi kwa wewe uliyechukua chumba cha biashara ambacho kilikuwa na mtu kabla.
Vipi wewe ambaye umechukua nafasi ya mtu aliyefukuzwa?
Vipi kwa wewe ambaye umenunua ardhi ambayo wengine haikuwapa faida?
✓✓Ndugu, inakupasa sana kuwa muombaji na mtoaji ili upate baraka za MUNGU katika eneo hilo.
Kuna watu huota ndoto kila Mara wakiona nyoka maeneo yao ya kazi, ndugu yuko mtu alikuwa anaona nyoka kazini kwake kumbe yule nyoka ni jini ambaye hupewa kafara ili kulinda kiti, usipomtowesha kwa jina la YESU KRISTO atakusumbua sana na hata kukuharibia sana.
Kuna mpaka shule au vyuo wamiliki walizika wanyama wa matambiko ili kufunga watu kipepo lakini baada ya masomo ukitoka hapo hakuna kupata ajira, ndugu sio watu wote ni wema kwako, mwema kwako ni YESU KRISTO tu na watumishi wake waaminifu.
Sasa kama wewe ndio unasoma shule hiyo iliyofanyiwa uchawi unaweza ukatoka shuleni hapo umeshikiliwa na uchawi wa ardhi hiyo, ndio maana ni muhimu sana kuombea ardhi ya eneo unaloishi kwa muda au unaishi maisha ya kudumu.
3. Omba ufahamu wako ili umtii ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye mwalimu wa kweli wa kukupeleka kwenye mafanikio yako sahihi.
Zaburi 32:8 "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."
4. Futa vifungo vya giza katika ardhi ya eneo lako la kufanikiwa kwako.
Kumbu 12:1-3" Hizi ndizo amri na hukumu mtakazotunza kuzifanya katika nchi aliyokupa BWANA, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi. Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo."
5. Simamisha agano na MUNGU katika eneo hilo, kwa sadaka inayoambatanishwa na maombi ili kuondoa maagano ya kipepo yaliyofanyika hapo.
Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha MUNGU wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu."
✓✓Ukisimamisha agano na MUNGU ujue maagano ya kishetani katika ardhi hiyo yataondoka.
Ombea pia sadaka zako na zaka zako unazozitoa kutokana na kazi yako eneo hilo.
6. Ita baraka ya MUNGU iambatane na wewe hapo.
Isaya 58:9 "Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;"
7. Omba MUNGU akufunulie hazina za sirini ambazo ni baraka zako.
Isaya 45:3 "nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, MUNGU wa Israeli."
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments