UZINZI NA DIVAI MPYA HUONDOA FAHAMU ZA MWANADAMU.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 




Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Uzinzi na divai huondoa fahamu za mwanadamu.

Hosea 4:11 "Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu."

✓✓Uzinzi Naamini unafahamu kwa lugha rahisi ni kukutana kimwili na Mtu ambaye sio Mke wako wa Ndoa kwa Wanaume au sio Mume wako wa Ndoa kwa Wanawake.

Marko 8:38 "Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu."

◾Kizazi Cha uzinzi kinahusisha wakubwa na wadogo wote kwa sehemu kubwa ni wazinzi 

✓✓Maeneo mengine Biblia imetenganisha katika ya Uzinzi na Uasherati na maeneo mengine Uzinzi umejumuisha Vyote yaani na Uasherati ni sehemu ya uzinzi.

✓✓Lakini mwasherati ni Mtu ambaye hayuko katika Ndoa anapokutana kimwili na Mtu yeyote yule.

✓✓Lakini uzinzi umebeba maana nzima ya Mtu kukutana kimwili na Mtu yeyote ambaye sio mwenzi wake wa Ndoa.

Mfano ni hapa Mtu akitoka nje ya Ndoa yake wakati mwenzi wake yuko hai ni mzinzi.

Warumi 7:3 "Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine."

◼️Nikirudi katika "DIVAI MPYA " hii ni pombe.

Yoeli 1:5 "Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu."

✓✓Hivyo pombe huondoa akili njema za Mtu.

Wako watu leo wamefukuzwa kazi nzuri kwa ajili ya ulevi, divai mpya umeondoa akili njema ndani yao kama Biblia inavyosema.

◼️ Sasa hasara mojawapo ya Uzinzi  na pombe ni kuondoa akili nzuri ndani ya mhusika.

✓✓Inawezekana mume wako au mke wako kwa sasa hana fahamu kwa sababu ya uzinzi anaoufanya huko nje ya ndoa, uzinzi umeondoa akili njema ndani yake.

Kuna wanaume wengi leo ni mashoga kwa sababu walilewa na kuishiwa Nguvu au kupoteza fahamu Kisha vijana washenzi wakawaingilia kinyume na maumbile, ni hatari sana lakini pombe au divai mpya imeondoa akili njema ndani Yako hadi wakafanyiwa uchafu huo.

✓✓Je mwenzi wako wa ndoa kwa sasa hana fahamu kwa sababu ya uzinzi?

✓✓Je huna fahamu Sasa kwa ajili ya ulevi?

Moja ya hasara ya uzinzi ni akili kumtoka mtu husika.

Ndio maana unaweza kukuta Baba msomi kabisa lakini Mshahara wake wote anamalizia kwa hawara huku mke wake na watoto wake wanashinda njaa, huko ndiko kukosa fahamu kunakotokana na dhambi ya uzinzi.

Ndugu Mwanaume usiye na akili maana unatoka nje ya ndoa yako kufanya uzinifu, Biblia inakushauri kwamba usiwape nguvu zako wanawake Malaya.

Mithali 31:3 "Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme."

Hata wewe mwanamke usiye na akili kwa sababu ya kusaliti ndoa yako kwa kufanya uzinifu, usiwape nguvu zako wanaume Malaya.

✓✓Malaya yeyote amebeba kifungo kibaya sana.

Malaya ni Kahaba kwa jina lingine, na Biblia inasema kwamba Kahaba ni shimo lefu sana, shimo maana yake kifungo cha kipepo.

Mithali 23:27 "Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba."

✓✓Shimo lina maana ya kifungo cha giza hivyo makahaba au wanawake wa nje ya ndoa wamebeba kifungo cha kipepo kwako mwanaume.

Je pombe imeondoa akili njema ndani Yako?
Ndugu Acha pombe na ikatae katika Maisha Yako.

Ngoja nikusimulie Mambo haya 2 ambayo chanzo chake ni pombe.
Siku Moja Miaka mingi iliyopita Kuna Kijana mmoja aniliomba nimsaidie kiroho kwa sababu anahisi ana dhambi sana, nikamuuliza "kwani umeifanya  Nini kibaya" akasema jirani na nyumbani kwao Kuna bar na walevi wengi huenda pale kunywa pombe, akasema siku Moja alienda pale Mwanamke mwenye umri kama Miaka 50 na kidogo, akanywa hadi usiku saa nne, Sasa wakati wa kurudi nyumbani akawa anapepesuka hivyo akaomba kusindikizwa, Kijana huyu na mwezake 4 wakamsindikiza na walipofika mbali kidogo wakamwingilia kwa zamu Kisha mmoja akampeleka, Mwanamke yule nyumbani kwake, baada ya siku chache akarudi Tena kulewa Wala hakumbuki aliyofanyiwa, na vijana wale mchezo ule wakauendeleza kwa Mwanamke yule na Mwingine ambaye naye ana Miaka kama 60.
Siku Moja Kijana huyu akiwa na vijana wenzake 10 walimwingilia mama Mwingine baada ya kuleta hadi kupoteza fahamu, walimpeleka kwenye jengo ambalo halijaisha wakamwingilia Kisha wakamwacha alale pale, kesho yake akaanza kutafuta waliomfanyia hivyo hakuwaona.
Nini nataka kusema?

✓✓Pombe iliondoa fahamu za Wanawake hawa hadi kufanyia uchafu mbaya bila kujua.

✓✓pombe Inawezekana ingesababisha maambikizi ya magonjwa ya zinaa.

✓✓Wengine wameingilia kinyume na maumbile kwa sababu ya pombe.

Ndugu kwanini usiache pombe?
Kwa Nini utu wako uondoke kwa ajili ya divai mpya?
Ndugu, Biblia haikosei kamwe, inaposema uzinzi na divai mpya huondoa akili njema ndani Ya Mtu uwe na uhakika ni hivyo.

Inawezekana ujumbe huu umekuja kwako kama onyo la MUNGU kwako ili kukuepusha na madhara mabaya ambayo yangekuja mbele Yako kwa sababu ya uzinzi au pombe.

✓✓Wanaume wa nje ya ndoa wamebeba kifungo kibaya cha kipepo kwako mwanamke na wazinzi wasio pata neema ya MUNGU wanaiongia Katika shimo la Kahaba huishia jehanamu maana wazinzi wote wasiotubu na kuacha uzinzi, hao wakifa huenda jehanamu.

Ufunuo 21:8 " Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."

Nini ushauri wangu?

◼️Ewe Mwanaume uliye katika ndoa usikubali kuondokewa na akili kwa sababu ya usaliti wa ndoa yako, usikubali kumsaliti mke wako. 

Kama huwa unasaliti ndoa yako tubu leo na vunja mahusiano ya kipepo na wanawake wote wa nje ya ndoa yako.

◼️Ewe kijana ambaye hujaingia Katika ndoa, usikubali kuondokewa  akili kwa kufanya ngono na mtu yeyote yule, jitunze na kama ni wakati wako kuoa basi funga ndoa Katika hali takatifu na hata mchumba wako usikubali kuzini naye bali subiria tendo la ndoa ukiwa ndani ya ndoa, tendo la ndoa ni ndani ya ndoa takatifu tu.

◼️Ewe mwanamke uliye Katika ndoa usikubali kupungukiwa akili kwa sababu ya kuisaliti ndoa yako, kumbuka kuna jehanamu kwa wazinzi na waasherati wote, kama unafanya hivyo tubu leo na futa mahusiano hayo ya kishetani na hao wanaume wote wa nje ya ndoa yako.

◼️Ewe binti ambaye hujaingia Katika ndoa usikubali kamwe kupungukiwa akili kwa kufanya mapenzi na mwanaume yeyote yule.

✓✓Ndugu amua tu kuacha uzinzi maana ni dhambi na amua tu kuacha kunywa pombe maana ni dhambi.

Kumbuka hata mchumba wako ukiruhusu kuzini naye ujue utatengeneza kuaachwa na hata unaweza kuachwa ukiwa mimba au ukafa ukijaribu kutoa mimba au ukaenda jehanamu usipopata neema ya kutubu.

✓✓Ukiruhusu uasherati ujue umeruhusu maroho ya kuzimu kukuvaa, ni mbaya sana sana.

◼️Ndugu unayesoma ujumbe huo nakuomba ikimbie dhambi ya uzinzi/Uasherati, jitenge mbali na dhambi hiyo na usifanye dhambi hiyo tena.
Mpokee YESU KRISTO Mwokozi kwa upya, utubu na utengeneze na MUNGU.

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments