WAKATI ULIOKUBARIKA KUOKOKA NDIO SASA.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni 


◼️Huu ni wakati bora sana kwako.

✓✓Hakuna wakati mwingine kuokoka ila sasa ukiwa unaishi.

✓✓MUNGU yuko tayari kukusikia kama unataka kuokoka, MUNGU yuko tayari kukusaidia ili tu uokoke.

2 Wakorintho 6:2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)

◼️Kuokoka ni nini?

✓✓Kuokoka ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wake.

✓✓Kuokoka ndio ndio Wokovu wa KRISTO.

✓✓Wakati wa kuokoka sio kesho wala kesho kutwa bali wakati wa kuokoka ni Leo.

Usiwaze kuokoka kesho au kesho kutwa maana inawezekana kesho au kesho ukawa umeshakufa, inawezekana kesho kutwa utakuwa kichaa, inawezekana kesho kutwa utakuwa gerezani na hakutakuwa na mtu wa kukuongoza sala ya toba na kukuombea na kukusaidia kiroho.

✓✓Ninaposema haya sina maana kwamba hayo yatakupata kesho au kesho kutwa bali wewe leo yaani sasa ndio yako, kesho wewe mwanadamu huna mamlaka nayo ina unahitaji neema tu ya MUNGU.

✓✓Wakati wa kuokoka ni Leo wala sio kesho au kesho kutwa.

Ndugu, wapo waliopanga kuokoka kesho kutwa yao na haikuwezekana maana hawakujua hiyo kesho kutwa wangekuwa wapi.

✓✓Biblia inaposema Wokovu ni sasa ina maana ya sasa na sio kesho, ndugu itii Biblia na kuifuata.

Inawezekana kesho ukawa kilema, huwezi kufika kwa watumishi wa MUNGU wakusaidie kiroho.

Inawezekana kesho au kesho kutwa utakuwa Hospitali ukiumwa na hakuna Mtumishi atakuja kukuongoza sala ya toba hata ukaokoka.
Wokovu ni Leo ndugu.

✓✓Wakati wako wa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi ni leo ndugu.

✓✓Kama wewe ulishampokea YESU KRISTO ila ukaanguka dhambini, ndugu wakati wa kutengeneza na YESU KRISTO ni Leo.

◼️Mpokee Bwana YESU KRISTO kwa upya na utasamehewa na kuokoka.

Mathayo 3:2 "Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."

✓✓Inawezekana wewe ulirudi nyuma, ukaacha Wokovu na ukaacha ibada, ndugu wakati wa kutengeneza na MUNGU ni sasa, ndugu itumie nafasi vyema, usiiache nafasi hii ikapita hujaokoka.

✓✓Usiitarajie kesho kwa ajili ya kuokoka maana huna uhakika kama kesho utakuwa hai.
Wokovu ni leo ndugu.

Matendo 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"

Ndugu kumbuka kwamba MUNGU hulituma Neno kama alivyolituma leo ili wewe uchukue hatua na kuokoka.

Katika maisha yako hakikisha siku zote unaishi ndani ya kusudi la MUNGU na tembea kwenye kusudi la MUNGU.

Kusudi la MUNGU ni nini?

✓✓Kusudi la MUNGU ni mpango wa MUNGU wenye lengo la ki MUNGU.

✓✓Kusudi la MUNGU kwako ni mpango wa MUNGU kwako wenye lengo la MUNGU unaotakiwa kuufuaata na kuuishi.

Yako makusudi makuu mengi ya MUNGU juu wanadamu, baadhi yaliyo makuu ni haya:

1. MUNGU alimtuma Bwana YESU ili kusudi atuokoe tusiende jehanamu(Wagalatia 4:4-5)

✓✓Hivyo mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako kusudi usiende jehanamu.

2. Mpokee ROHO MTAKATIFU kusudi uyajue uliyokirimiwa na MUNGU(1 Kor 2:12)

✓✓Hivyo mpokee ROHO MTAKATIFU kusudi akusaidie katika mengi sana yakiwemo ili ujue aliyokukirimia MUNGU.

3. Huduma tano(5) za ROHO MTAKATIFU ziko katika kanisa la KRISTO duniani ili kuwakamilisha watakatifu( Waefeso 4:11-12)

4. YESU KRISTO analisafisha Kanisa lake kusudi liwe Kanisa takatifu(Waefeso 25:27)

✓✓Hivyo wewe kama Kanisa kubali kusafishwa na YESU kwa kulitii Neno lake linalokutaka uishi maisha matakatifu ya Wokovu.

5. Tunakaa ndani ya YESU KRISTO ili kusudi siku akija tusiabike bali twende na YESU uzima wa milele( 1 Yohana 2:28)

◼️Kukaa ndani ya YESU KRISTO sio kuitwa tu Mkristo bali kukaa ndani ya YESU KRISTO ni kuokoka na kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wake siku zote.

6. Bwana YESU alikuja duniani kusudi sisi tulio katika yeye tuzishinde nguvu za giza(1 Yohana 3:8b)

✓✓Hivyo ukitumia jina la YESU KRISTO na damu ya YESU KRISTO katika maombi hakika utazishinda nguvu zote za giza.

7. Bwana YESU alikuja duniani ili kuwaokoa wanadamu(Luka 19:10)

✓✓Hivyo kubali kuokolewa na Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Kumbe unatakiwa sana kulijua kusudi la MUNGU juu yako na liishi hilo kusudi la MUNGU maana ni muhimu sana kwako.

Haijalishi kuna makusudi Mengi ya MUNGU juu yako lakini makusudi ya MUNGU Saba(7) hapo juu ndio kiini hasa cha kila kusudi la MUNGU juu yako.
Ishi kwa kumtegemea MUNGU na kumcha MUNGU.

Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.


Comments