![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Amani ya MUNGU inapita akili zote za wanadamu.
Wafilipi 4:7 "Na amani ya MUNGU, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika KRISTO YESU."
✓✓Amani ya MUNGU inazidi akili zote za kufundishwa au akili za kuzaliwa au akili za kujifunza.
✓✓Amani ya MUNGU iko na ROHO MTAKATIFU.
◼️Ndugu mhitaji sana ROHO MTAKATIFU ili amani ya MUNGU ianze kufanya kazi ndani yako.
Amani ya MUNGU inazidi akili zote za wanadamu.
✓✓Amani ya MUNGU hukusaidia katika maamuzi.
✓✓Amani ya MUNGU hukupa uhakika wa jambo jema la kufanya.
✓✓Amani ya MUNGU hukupa uhakika wa rohoni juu ya nani ni mtu sahihi, nani ni rafiki sahihi, nani wa kumweleza jambo lako, nani wa kumsaidia n.k
✔️✔️Tunaishi na wanadamu wengi na kwa macho yetu ya kimwili ni vigumu kuwajua kwa usahihi, ni vigumu hata kumjua adui, ni vigumu kumjua anayepanga kukudhuru n.k
✓✓Lakini amani ya MUNGU hutusaidia katika maamuzi sahihi.
Wakolosai 3:15 "Na amani ya KRISTO iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani."
Nini kinafanyika?
✓✓Unapokuwa katika maamuzi ambayo huna uhakika ukiona amani ya MUNGU moyoni ujue ni kwema.
✓✓Unapokuwa katika maamuzi ambayo huna uhakika na rohoni amani ya MUNGU imeondoka na huzuni kuchukua nafasi maana yake jambo hilo usiliendee au omba sana kwanza ili kuondoa mitego ya shetani iliyo katika hicho unachotaka kuamua.
Ndugu ihitaji sana amani ya KRISTO moyoni mwako.
◾Mtu asiye na amani ya KRISTO moyoni mwake hata kama anaamua jambo lenye madhara kwake hatajua kama jambo hilo lina madhara hadi madhara yatakapotokea ndipo atajua kwamba aliamua vibaya.
✓✓Kumbuka pia kuna amani ya MUNGU ambayo pia jina lingine inaitwa amani ya KRISTO, lakini pia kuna amani ya kibinadamu.
◾Amani ya kibinadamu pekee inaweza kukupoteza maana amani ya kibinadamu hutokana tu na unayoyaona kwa macho au unayoyasikia kwa masikio.
Mfano wewe ni binti, anaweza kukufuata kijana ili akuoe, wewe ukawa na amani naye kwa sababu tu ana mali na kazi nzuri lakini kumbe kijana yule yuko katika mikataba ya kishetani na ameshaambiwa miaka 4 baadae atoe kafara ya Mke, wewe kwa sababu unaongozwa na amani ya kibinadamu unakuwa na amani naye mtu huyo hata kama watumishi wa MUNGU wenye amani ya MUNGU ndani yao wakikukataza wewe utasema wanakuonea wivu na utawachukia. Wakati wa kutaka kutolewa kafara ndipo utashtuka kwamba amani ya kibinadamu iliyojaa tamaa za mambo ya dunia ndiyo ilikuongoza kumkubali huyo muuuaji.
Ndugu ihitaji sana amani ya KRISTO ndani yako.
Jinsi ya kuipata amani ya MUNGU ndani yako ni kufuata mfululizo huu.
1. Mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Yohana 1:12-13 " Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.
Wakolosai 3:16 "Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu."
3. Jifunze kuijua sauti ya MUNGU.
Kumbu 13:4 "Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye."
Marko 13:33 "Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.'
Zaburi 1:1-2 " Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku."
6. Jazwa nguvu za ROHO MTAKATIFU.
Matendo 2:4 "Wote wakajazwa ROHO MTAKATIFU, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama ROHO alivyowajalia kutamka."
3 Yohana 1:11 "Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa MUNGU, bali yeye atendaye mabaya hakumwona MUNGU."
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments