AMKA USINZIAYE.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Waefeso 5:14-15" Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na KRISTO atakuangaza. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; "

✓✓Kuna wamesinzia kiroho, Biblia inasema kwamba watu hao wanatakiwa kufufuka katika wafu na Bwana YESU atawaangazia.

✓✓Usingizi huu sio usingizi huu wa kawaida bali ni hali ya mtu kutokuzingatia Wokovu wa KRISTO na kujikuta hayuko tena katika kundi la waenda mbinguni.

Ndugu, kama ni wewe umesinzia usingizi huo amka leo.

Wewe uliyesinzia usingizi wa kiroho amka.

✓✓Wewe usinziaye kwa habari za kujifunza Neno la MUNGU amka.

✓✓Wewe uliyesinzia katika usingizi wa dhambi amka na uache dhambi.

✓✓Toka kwenye huo usingizi wa uzinzi na uasherati, toka kwenye usingizi wa usaliti na wizi.

✓✓Toka kwenye usingizi wa kila dhambi.

◼️Dhambi humfanya mtu asinzie kiroho ndio maana kuna watu akizama dhambini anasinzia hadi atajikuta jehanamu, usingizi wa dhambi humfanya mhusika hata akionywa na watumishi wa MUNGU kwa sababu ya usingizi wa dhambi alionao yeye atadhani watumishi wanamuonea wivu au watumishi wanahitaji sadaka.
Ndugu, amka leo katika usingizi wa dhambi.

Usingizi wa dhambi ni mbaya sana, ukiendelea na dhambi inaweza kupelekea kifo na kisha jehanamu.

Mtu aliyesinzia usingizi huu hata akihubiriwa kila siku yeye hafanyii kazi Neno la MUNGU maana bado yuko kwenye usingizi wa kishetani.

Mtu wa hivyo hata akiambiwa "Okoka ndugu" kwa sababu ya usingizi huo atakataa na kuendelea na ushetani wake.

✓✓Ndugu, amka wewe usinziaye.

Inawezekana umemwacha YESU ili upate mume mpinga Kristo na wewe umeamua kuwa mpinga Kristo, ndugu huo usingizi uliopo ni usingizi wa jehanamu usipopata neema.

Inawezekana bosi wako ni mpinga Kristo na wewe amekushawishi uwe mpinga Kristo ili uendelee kupata mshahara, ndugu hiyo ni hatari kwako, ni heri usiwe na kazi ila uwe na YESU KRISTO Mwokozi.

✓✓Usikubali kuwa na usingizi wa kiroho unaokufanya umwache YESU KRISTO.

Kuna watu walikuwa Wakristo wazuri sana lakini walipoajiriwa na Mabosi wapinga KRISTO ilibidi wamwache YESU KRISTO ili kuwafurahisha bosi zao wapinga KRISTO.

Kuna Mtu ili asifukuzwe kazi na boss mpinga KRISTO alibadili hadi Jina na dini ili kumfurahisha Boss kumbe anajitenga na YESU KRISTO mwenye uzima wake wa milele.

✓✓Usikubali kuwa na usingizi wa kiroho unaokufanya usahau wajibu wako kwa MUNGU katika KRISTO.

◼️Ndugu hakikisha wewe ni wa mchana na sio wa usiku.

1 Wathesalonike 5:6-9 " Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. Kwa kuwa MUNGU hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu YESU KRISTO;"

Amka ndugu maana zamani hizi ni zamani za uovu.

Waefeso 5:16-17 " mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA."

✓✓Usikubali kuendelea kuvutwa na dunia, amka kwenye huo usingizi.

✓✓Usikubali kuvutwa na anasa, amka kwenye huo usingizi.

◼️Ndugu, hakikisha YESU KRISTO ni Mwokozi wako na ishi maisha matakatifu katika yeye.

Kama uko katika dhambi na usingizi wa kishetani umeshakupata kiasi kwamba hata tu kushtuka kwamba ukifa katika dhambi hizo unaenda jehanamu, hata hushtuki, ndugu amka leo kwa kutubu na kuacha dhambi hizo.

Watumishi wanapokuonya au kukushauri ili usikose mbingu wewe kwa sababu ya usingizi huo unawaona hao watumishi wamekosa kazi ya kufanya au usingizi huo unakupa kuwaza kwamba hao watumishi wanahitaji fungu la kumi ndio maana wanajaribu kukurudisha katika wokovu, ndugu amka leo katika usingizi huo mbaya.

✓✓Inawezekana umenaswa sasa katika dhehebu ambalo halimtaki YESU, wamekuvuvia usingizi wa kishetani ili ujitenge na YESU KRISTO, ndugu amka wewe usinziaye, fufuka katika wafu na KRISTO YESU atakuangazia nuru yake.

◼️Kumbuka ukimwacha YESU umepishana na uzima wa milele, hivyo hao wanaokutoa kwa YESU wa wokovu tambua kwamba hao wanakupeleka jehanamu.

Ndugu nakuomba ambatana na YESU KRISTO na sio vinginevyo.
MUNGU akubariki ukifanyia kazi Neno hili muhimu.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe.


Comments