![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi. |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la kutupa mbinu za kuomba maombi ya vita ili tuwe washindi dhidi ya nguvu za giza.
◼️Maombi ni ufunuo hivyo hitaji sana kujifunza sana Neno la MUNGU ili upate maarifa ya kukusaidia namna ya kuomba na kushinda dhidi ya nguvu za giza.
Mwambie MUNGU akufundishe vita ya kiroho ndipo utashinda dhidi ya nguvu za giza.
Zaburi 144:1 "Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana."
Tunapojifunza silaha za kiroho ni muhimu tukajua kwamba ziko katika makundi mengi na kanuni kadhaa.
◼️ Kanuni sahihi yoyote ya ki MUNGU katika maombi ni ile kanuni ambayo tunaomba katika jina la YESU KRISTO huku tukiomba sawasawa na Neno la MUNGU.
Kumbuka tuna mamlaka ya jina la YESU KRISTO ya kuamuru na kumshinda adui, je wewe unapigana vita leo kwa kutumia nini katika jina la YESU KRISTO?
Ninachotaka kukuambia ni kwamba ukipata ufunuo wa kuombea kwa kutumia silaha mojawapo kati ya hizi chini itumie silaha hiyo dhidi ya nguvu za giza na utashinda.
Haina maana silaha za MUNGU katika maombi ya vita ni hizi tu bali ziko nyingi sana ila hata kwa hizi chache naamini utajifunza kitu muhimu sana hata adui ambaye labda ameyazoea maombi Yako leo atakutana na silaha za ajabu kwenye ulimwengu wa roho na baada ya hapa hatakufuatilia tena.
Kwa mtu ambaye anapitia vita kali sana ya kiroho dhidi ya nguvu za giza fanyia kazi na naamini utanipa ushuhuda kile MUNGU atakifanya ili kukushindia.
Wapo watu wanalala usiku na wanapoamka wanajikuta nje,
wapo watu wamefungwa uzao,
wako watu wamewekewa Mipaka kwenye ulimwengu wa roho,
wako watu wanaumwa kwa kurogwa,
wako watu wametumiwa mapepo ya kufarakanisha ndoa zao ili hizo ndoa zife,
wako watu wanateswa na mizimu,
wako watu kila mara ndotoni wanakimbizwa na nyoka au Wanyama wakali,
wako watu wamefungwa vifungo vya siri sana hata hawajui ila wanaona tu madhara yanyotokana na vifungo hivyo vya giza,
wako watu wanawindwa na roho za mauti na kukataliwa,
wako watu ni mawindo ya wachawi na majini kila siku,
wako watu ni mateka na wako kwenye mashimo ya kiroho,
wako watu wanateswa na nguvu za giza za kila namna.
Ninapokueleza haya Wewe rafiki yangu unayesoma somo langu hili nina shuhuda halisi za watu ambao wamewahi kunipigia simu na kuniambia juu ya mateso hayo niliyotaja na mengine mengi zaidi, ndio maana hapa nasema na mtu anayepigana vita ya kiroho kweli kweli, ufunuo wa leo utaongeza maarifa ya maombi ndani yako na ukiomba katika jina la YESU KRISTO huku ukitumia silaha hizi kimaandiko utamuona MUNGU wa miujiza mingi.
Mikono yako ya kiroho inatakiwa kufundishwa vita ya kiroho ndivyo andiko hapo juu linasema, silaha hizi za kimaandiko zitakupa msaada mkuu ukizitumia katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
Baadhi ya silaha za kupigania vita ya kiroho ni hizi.
1. Upanga wa MUNGU.
Mimi binafsi kama Peter Mabula hii ni moja ya silaha ya kiroho katika maombi ambayo huwa naitumia zaidi.
Upanga wa MUNGU ni hatari sana dhidi ya nguvu za giza.
Isaya 27:1 "Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini."
MUNGU anasema kuwa kwa kutumia upanga wake mkali na mkubwa atawaua nyoka hao aina nne, nyoka hawa ni nguvu za giza ambazo ni maroho wa kuzimu kama majini, mizimu, wakuu wa giza n.k
Je wewe hupambani katika ulimwengu wa roho na maadui hao walio roho za nyoka?
✓✓Kama unapambana nao leo nimekujulisha silaha inayoweza kutumika kwenye ulimwengu wa roho ili kukushindia.
Siku moja nilivamiwa na wachawi, majini na mkuu wa giza, niliogopa sana sana na nikajua siku hiyo nakufa maana nilikuwa nimekaa kitandani nikiwa macho kabisa nikiwaona wakinikaribia, ghafla rohoni mwangu nikapewa akili ya kutumia upanga wa MUNGU, nilipotamka kwamba "Sasa nashika upanga wa MUNGU na nawakata katika jina la YESU KRISTO " yaani ile natamka tu nikajiona nina upanga unaong'aa nikaanza kuwakata, yaani upanga ule ukimsogelea tu huyo nguvu za giza umeshammaliza tayari.
Ni upanga unaofanya kazi kama umeme.
Ezekieli 21:15 "Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje."
Huu upanga wa MUNGU katika ulimwengu wa roho unaweza kukufanya uzishinde nguvu za giza kirahisi sana.
Kama hao mashetani wamewahi kuona tu moto wewe ukiomba leo wabadilishie silaha wapelekee upanga wa MUNGU.
Na kuna panga za MUNGU nyingi, pia kuna panga huwa zinashikwa na malaika wanapokusaidia vita ya kiroho lakini pia kuna upanga wa MUNGU hutembea wengine yaani ni upanga ambao unauwezo wa kutembea wenyewe bila kushikwa na malaika au wewe kwenye ulimwengu wa roho, kuna upanga wa moto yaani ni upanga unaofanya kazi ukiwa unawaka moto pia, ni upanga unaoweza kugeuka huku na huko wenyewe, MUNGU ni wa ajabu sana.
Mfano hai ni upanga ulioilinda bustani ya Edeni baada ya akina Adamu kutenda dhambi.
Mwanzo 3:24 "Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima."
Upanga huu mimi nimeshautumia mara nyingi sana katika vita ya kiroho na niliona ushindi mwingi sana, huwa nafundisha vitu ambavyo nina uhakika navyo.
Ulishawahi kujiuliza ilikuwaje kwa usiku mmoja tu malaika mmoja tu wa MUNGU aliua jeshi la waashuru laki moja na themanini na tano elfu?
Isaya 37:36 "Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu mia na themanini na tano elfu katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia."
✓✓Ndugu, silaha za MUNGU ukiwemo upanga zinaweza kufanya kazi kubwa sana katika ulimwengu wa roho na matokeo yake ukayaona katika ulimwengu wa mwili.
Wewe mteule wa KRISTO uliyeokoka, wewe hakika ni jeshi la MUNGU, je unatumia silaha kama mwanajeshi wa vita ya kiroho kupitia mamlaka ya jina la YESU KRISTO?
Leo ukipata ufunuo wa kupigana na nguvu za giza kwa kutumia upanga wa MUNGU changamka na utashinda vita ya kiroho.
2. Giza la kiroho.
Giza la kiroho ni silaha ya kimaombi inayoweza kukupa ushindi wa ajabu dhidi ya nguvu zote za giza.
Giza hilo ninalozungumzia sio giza hili unalolijua wewe, hili giza unalolijua wewe nguvu za giza wanaona kama mchana, wachawi na majini na mizimu katika giza hili wanaona kama mchana kabisa na hulitumia giza hilo kufanya mambo yao.
Giza ninalozungumza ni giza lingine kabisa, ni silaha ya MUNGU ambayo inaweza kumpata adui yeyote kwenye ulimwengu wa roho hata asiweze tena kukufanya lolote alilokuwa amezoea kulifanya kwako.
Labda ngoja nianzie hapa ili unielewe vyema.
Giza ni nini?
Giza ni hali ya kutokujua kitu.
Hivyo unaweza kuomba maombi katika jina la YESU KRISTO ukiamuru giza la MUNGU la kiroho liwapate watenda kazi wa kuzimu wanaokuwinda au kufuatilia chochote kwako na litawapata hilo giza hivyo hawatakuwa na uwezo tena wa kufanya chochote kwako.
Musa aliitumia hiyo silaha ya MUNGU iitwayo giza na akashinda vita ya kiroho dhidi ya Farao na nchi yake.
Kutoka 10:21-23 " BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe giza juu ya nchi ya Misri, watu wapapase-papase gizani. Basi Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri muda wa siku tatu; hawakupata kuonana mtu na mwenziwe, wala hakuondoka mtu mahali alipokuwa muda wa siku tatu; lakini wana wa Israeli wote walikuwa na mwanga makaoni mwao."
Giza hili hata taa na tochi hazikufanya kazi.
Adui zako hata wanadamu wabaya unaweza ukawapiga kwa giza hili na kama walijiandaa kukuzuia kupata kazi watakuja kushtuka uko kazini muda mrefu.
Hujawahi kuona watu wanasema "fulani amezaa kweli?, kumbe alikuwa mimba, mbona hatukuiona hiyo mimba hadi amezaa? Haya maajabu"
Kuna watu wabaya wanaweza wakafanya kila mipango usipande cheo, usifanikiwe, usipate haki yako, giza la MUNGU ukilitumia linaweza kuwafanya wasioone wala kujua chochote wakati wa mchakato, watakuja kushangaa tu pale utakapokuwa umeshakalia eneo tayari.
Nimesema giza ni hali ya kutokujua kitu, giza hilo linaweza kuwapata kila maadui zako katika ulimwengu wa roho kama ukiomba katika jina la YESU KRISTO.
Mtu mmoja aliwahi kuumizwa na masomo yangu mtandaoni akanitamkia live kwamba "Mwisho wako kupost masomo yako ni mwaka huu" ajabu kipindi hicho nilikuwa kama nimeshapost masomo chini ya 100 lakini tangu anitishe na kusema watanishughulikia imepita miaka zaidi ya 10 na masomo sasa yameshavuka 1400 ambayo nimewahi kupost mtandaoni na safari ndio kwanza inaanza katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
✓✓Giza la MUNGU linaweza kumfanya mtu asitambue chochote kuhusu wewe, kile alichokuwa anataka kukuzuia, atashangaa tu uko nacho tayari.
Inawezekana kuna watu wabaya wameenda kwa waganga wa kienyeji ili wewe usiingie katika ndoa, usipate kazi, usimalize masomo, usiwe na huduma kubwa, usikubalike n.k hao wote pamoja na waganga wao, pamoja na wachawi wao, pamoja na majini yao, wote wote katika jina la YESU KRISTO ukitumia silaha hii ya giza la MUNGU ujue watashangaa kile walichokuzuia sana kiroho ndicho unafanikiwa sana kimwili.
Inawezekana unakabwa kila siku, wapo watu wanafanya mapenzi na majini, kuna siku nilishangaa sana baada ya wanaume wawili kuniambia kwamba kuna watu huwajia ndotoni na kuwalawiti na asubuhi wanakuta kweli wamechafuka, wanawake ndio wengi tu wamewahi kuniambia kwamba wanaingiliwa kinyume na maumbile ndotoni.
Kuna watu ni siri yao tu lakini wengine wamefundishwa ushoga na majini mahaba yaliyokuwa yanawaingilia.
Ndugu unayehusika nakuomba leo mpe YESU maisha yako na uwe sasa na hasira za kiroho za kuomba ukitumia silaha hizi za MUNGU na hao wakuu wa anga watajuta kukufuata wewe.
Omba kama haya Maombi ya Daudi akitumia giza la MUNGU.
Daudi aliwatamkia hivi maadui zake " Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa BWANA akiwafuatia.-Zaburi 35:6"
◼️Ndugu naomba uwe na hasira za kiroho na omba kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO utashinda.
Inawezekana wewe ni yule umefundishwa tu kwamba waombee adui zako na wanaokuudhi, ndugu YESU aliposema hivyo hakumaanisha maadui zako wanaotoka kuzimu.
Watu wengi wanapotoshwa kwa njia hiyo na kujikuta kila siku wanafanyiwa vitu vibaya na nguvu za giza harafu wao wanasema "tuwaombee wanaotuudhi"
Ndugu, hakuna andiko ambalo Biblia inasema tuwaombee mema wanaotoka kuzimu kuja kufanya kazi zao kwetu.
Kama ni hivyo basi watu wamuombee mema shetani maana ndiye anayeongoza kuwauzi watu, ndugu lielewe Neno la MUNGU ili ufanyike askari kamili wa vita ya kiroho, usiteseke harafu Mtumishi anakuambia usiombe maombi ya vita bali waombee mema wanaokuudhi, ndugu wanaweza kukuua hao wachawi unaowaombea mema.
Mtumishi kama hajawahi kupitia vita kali ya kiroho dhidi ya nguvu za giza ni rahisi sana kuwakataza watu kuomba maombi ya vita.
Miaka mingi iliyopita Mimi Peter Mabula siku moja nikiwa nimelala nilishangaa kuna kitu kimenisukuma nikaanguka chini kutoka kitandani kwa nguvu sana, haikuwa ndoto bali live, ningekuwa najua kutumia silaha za MUNGU za maombi hakika hata kama kuna silaha inaitwa bomu au msumeno ningetumia siku hiyo.
Ndugu kama hupitia vita kali ya kiroho unaweza usinielewe kabisa.
Kuna maeneo mchawi unamjua na anakutambia kila siku kwamba ni yeye anakutesa. Ndugu, mchawi wa hivyo akija kimwili wala usimuombee mabaya maana ni mwanadamu lakini akija kiroho tumia silaha za MUNGU za maombi ya vita ili kupambana naye na kumshinda.
Wako watu ufahamu umeondolewa kichawi, kuna watu hawaishi kwa amani kwa sababu ya nguvu za giza, ndugu kuanzia leo anza kuomba katika jina la YESU KRISTO ukitumia maandiko na unaweza kutumia pia maandiko yanayoonyesha silaha za MUNGU.
Anza kuwa muombaji, anza kuwa na maombi ya vita.
Anza kuwa na maombi ya kufunga, tumia silaha za MUNGU za kimaandiko.
Jifunze kuomba Maombi yanayoambatana na Sadaka.
Somo ni tamu sana, ndio kwanza nimesema silaha mbili tu bado silaha kama nane nitazungumzia wakati Mwingine.
Somo litaendelea
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Somo ni tamu sana, ndio kwanza nimesema silaha mbili tu bado silaha kama nane nitazungumzia wakati Mwingine.
Somo litaendelea
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments