DHAMBI YA UZINZI NA UASHERATI.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Rafiki yangu mmoja aliniandikia hivi
"Eti mtumishi Mabula tunajua kwamba dhambi zote ni sawa, vipi kuhusu dhambi ya uzinzi???
Inatofautiana wapi na dhambi zingine???
Au ina madhara gani kiroho tofauti na dhambi zingne???
Nina kiu ya kujua kiundani zaidi juu ya dhambi ya uzinzi kibiblia na madhara yake tofauti na dhambi zingne
Maana niliwahi kufundishwa kuwa ina madhara makubwa sanaa kiroho ina nataka kujua zaidi"

Majibu ya maswali ya rafiki yangu huyu naomba yawe msaada na kwako unayesoma somo hili ili na liwe msaada kwa watu ambao utawatumia somo hili.

Majibu ya Mtumishi Peter Mabula:

✓✓Dhambi zote ni sawa kwa sababu zote zinaweza kumpeleka mtu jehanamu.

1 Wakorintho 6:9-10 "Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."

✓✓Lakini ukiwa uko duniani dhambi ya uzinzi na uasherati ina madhara zaidi.

dhambi ya uzinzi ina madhara zaidi ya dhambi zingine.
Mfano mtu akitukana, hiyo ni dhambi mbaya ila inaweza ikawa na dhara moja tu kwamba ni dhambi lakini uasherati una madhara zaidi ya dhambi.

Ngoja nikuonyeshe kwa ufupi maandiko mawili ya madhara ya uzinzi.

1 Wakorintho 6:18" Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."

◼️Maana yake uzinzi kwanza ni dhambi lakini madhara mengine ni kwamba uzinzi huunajisi/huuchafua mwili kiroho yaani huuchafua mwili kiroho.

Mfano binti kijana mwasherati kwa sababu ya uadherati anaweza kukosa mtu sahihi wa kufunga naye ndoa na mtu huyo atajiona kama ana gundu, kumbe mwili wake umechafuka kiroho.

Hayo ni madhara zaidi nje na dhambi.

Kuna uzinzi ni mlango wa roho ya mauti.

Walawi 20:10 "Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa."

Hiyo roho ya mauti ni madhara zaidi nje na dhambi ya uzinzi.

Ndio maana kuna watu kwa sababu ya uzinzi na uasherati wamejikuta wakiondoka duniani kabla ya muda wao, wengine kwa magonjwa ya zinaa kama ukimwi na wengine Kwa kupigwa na hata kufa kutokana na kufumaniwa au kukamatwa n.k

Anayezini hana akili kabisa na tukio hilo alifanyalo litamletea maangamizo.

Mithali 6:32 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake."

✓✓Lakini pia uzinzi hutengeneza agano la kishetani, hayo ni madhara nje na dhambi ya uzinzi.

✓✓Usikubali kuwa mzinzi wala mwasherati.

✓✓Kama uko katika ndoa heshimu ndoa yako.

✓✓Kama una mchumba usikubali kufanya naye uasherati.

✓✓Kama uko kwenye ndoa hakikisha ni ndoa ya mke mmoja au mume mmoja tu.

Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."

fanyia kazi Neno la MUNGU na utaitwa heri.
Ishi maisha matakatifu katika Wokovu wa KRISTO YESU na utaitwa heri.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji, whatsapp n.k).
Ubarikiwe 

Comments