FAIDA ZA KULITII NENO LA MUNGU NA MAAGIZO YAKE.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

Mithali 30:5 "Kila neno la MUNGU limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio."

◼️Kuna faida nyingi zinazotokana na mtu kulitii Neno la MUNGU katika KRISTO YESU.

Baadhi ya faida za Kulitii Neno la MUNGU ni hizi

1. Neno la MUNGU litakufanya uishi miaka mingi inayoambatana na Uzima na amani.

Mithali 3:2 " Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani."

2. Neno la MUNGU litakufanya kuwa na kibali na akili nzuri.

Mithali 3:3-4 "Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za MUNGU na mbele ya mwanadamu."

✓✓Kibali ni idhini anayopata mtu ili kupata vitu fulani avitakavyo.

✓✓Kibali ni kukubaliwa kufanya jambo jema unalolitaka kulifanya.

✓✓Neno la MUNGU linaweza kukufanya uwe na kibali mbele za MUNGU na mbele za Wanadamu.

3. Neno la MUNGU hutenda kazi kwa wanaoliamini.

1 Wathesalonike 2:13" Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru MUNGU bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la MUNGU mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la MUNGU; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini."

4. Neno la MUNGU hutakasa.

1 Timotheo 4:5-5 " kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la MUNGU na kwa kuomba.
Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa KRISTO YESU, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata."

✓✓Kutakasa ni kumfanya mtu kuwa safi, kuwa bila uchafu wowote.
Neno la MUNGU ukilifuata linaweza kukufanya kuwa safi kiroho.

5. Neno la MUNGU li hai tena lina nguvu na makali kuliko panga.

Waebrania 4:12 "Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."

◼️Nguvu ya Neno ina kazi nyingi baadhi ni kumfukuza adui, kuharibu nguvu za giza n.k

6. Neno la MUNGU linaumba.

Waebrania 11:3 "Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la MUNGU, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri."

7. Neno la MUNGU katika KRISTO YESU linaweza kumfanya mtu azaliwe Mara ya pili.

1 Petro 1:23 "Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la MUNGU lenye uzima, lidumulo hata milele."

Nini maana ya kuzaliwa Mara ya pili?

✓✓Kuzaliwa Mara ya pili ni kumwamini YESU KRISTO kama Mwokozi kisha kumpokea kama Mwokozi na baada ya hapo unaanza kuliishi Neno la MUNGU huku ukiongozwa na ROHO MTAKATIFU.

1 Yohana 5:1 "Kila mtu aaminiye kwamba YESU ni KRISTO amezaliwa na MUNGU. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye."

◼️Ndugu lihitaji sana Neno la MUNGU.

Na kumbuka kwamba YESU KRISTO ni Neno juu ya Neno la MUNGU.

Ufunuo 19:13 " Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la MUNGU. Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi."

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments