![]()  | 
| Na Mwl Peter Mabula  Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi  | 
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
✓✓Kuna mzabibu mwema na kuna mzabibu mwitu yaani mzazibu mbaya.
Hiyo iko hivyo katika mti wa mzabibu lakini huo ni mfano pia kwa Wakristo kwamba katika wakristo kuna makundi hayo mawili, Kuna Mkristo aliye kundi la mzabibu mwema na kuna kundi la Mkristo aliye mzabibu mwitu.
Yeremia 2:21 "Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu?"
MUNGU anawauliza watu wake ambao mwanzo walikuwa watu wake wazuri lakini baadae wamegeuka na kuwa waasi mbele zake.
Kuna makundi ya sifa za Mkristo aliye mzabibu mwema na aliye mzabibu mwitu.
Ninachotaka kusema leo ni hiki tu;
 Hakikisha unakuwa mzabibu mwema na sio kuwa mzabibu mwitu yaani mzabibu mbaya.
Najua ni rahisi sana kumjua Mkristo aliye mzabibu mwema lakini ngoja nikuambie machache kuhusu Mkristo aliye mzabibu mwitu.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni Mkristo ambaye haishi maisha matakatifu.
✓✓Mtumishi aliye mzabibu mwitu ni mtumishi yule ambaye hamsikilizi ROHO MTAKATIFU ila utumishi wake yeye ni kuiga tu kwa watumishi wengine.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni Mkristo yule ambaye hurudi nyuma yaani humwacha YESU KRISTO.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni Mkristo yule anayeacha Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni yule Mkristo mzinzi, mwasherati au muongo muongo.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni yule Mkristo mtenda dhambi huku anajua ni dhambi, anatenda dhambi kwa siri akiwaogopa tu wachungaji wasimuone.
Ndugu, je wewe ni mzabibu mwema au ni mzabibu mwitu?
✓✓Kama wewe ni Mtumishi aliye mzabibu mwitu kwa sababu unalichanganya neno la MUNGU na uongo, basi badilika leo kwa kuamua kuwa Mtumishi mkweli na mwaminifu kwa KRISTO unayelitumia neno la MUNGU kwa kweli na haki.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni yule ambaye yuko katika dhambi na anafariji ujinga yaani anazini na mchumba wake, anawakosanisha Kanisa, anazuia kilicho cha MUNGU.
Ndugu, Mkristo aliye mzabibu mwitu ni yule ambaye yuko tayari kumwacha YESU ili aifuate dunia, yuko tayari kumwacha YESU ili apate mume au mke mpinga Kristo.
Ndugu, kama ni wewe ndio mzabibu mwitu basi fanyika leo mzabibu mwema.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni Mkristo yule anayekataa Kuokoka.
✓✓Mkristo aliye mzabibu mwitu ni Mkristo yule anayemkataa ROHO MTAKATIFU.
Ndugu, kama ni wewe inakupasa utubu na uache dhambi ili ufanyike mzabibu mwema.
✓✓Kuna Wakristo wasaliti wa ndoa, hao ni mizabibu mwitu.
✓✓Kuna Wakristo wezi, hao ni mizabibu mwitu.
◼️Ndugu hakikisha wewe unakuwa Mkristo aliye mzabibu mwema.
◼️MUNGU anataka uwe mzabibu mwema daima.
Ndugu, kama hujampokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako basi mpokee leo ili ufanyike Mkristo aliye mzabibu mwema.
Kama uliasi imani basi mpokee YESU KRISTO kwa upya leo ili uwe mzabibu mwema.
◼️Ndugu anza kutii Neno la MUNGU, anza kuwa mtoaji wa fungu la kumi, anza kuhubiri Injili ya KRISTO, anza kuwaambia watu kwamba YESU KRISTO anaokoa.
✓✓MUNGU alikutoa Misri(kwa shetani) ili uwe mzabibu mwema na sio kutaka tena kurudi Misri.
Zaburi 80:8-10 " Ulileta mzabibu kutoka Misri, Ukawafukuza mataifa ukaupanda.
Ulitengeneza nafasi mbele yake, Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi. Milima ilifunikwa kwa uvuli wake, Matawi yake ni kama mierezi ya MUNGU."
◼️MUNGU anapotuokoa katika KRISTO YESU hataki tufanye mambo mabaya hata tukageuka na kuwa mizabibu mwitu.
Ndugu, hakikisha unaanza kuwa mzabibu mwema katika KRISTO YESU.
MUNGU akubariki sana ukilifanyia kazi neno la leo.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe

Comments