![]()  | 
| Na Mwl Peter Mabula  Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi  | 
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Haya chini ni mambo ya kuzingatia kama kweli unahitaji kukua kiroho.
1. Ili ukue kiroho unahitaji sana kulisoma sana na kulitafakari Neno la MUNGU.
Wakolosai 3:16-17 ''Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye.''
◼️Neno la MUNGU lina ujumbe wa namna nyingi kulingana na nyakati na lakini wakati huu tuliopo ni wakati wa injili ya KRISTO, hivyo injili ya KRISTO ndio msingi wa sasa Wokovu.
Lakini pia ili mtu akue tunafahamu kwamba anahitaji vyakula mbalimbali, hata kukua kiroho unahitaji vyakula mbalimbali vya kiroho.
✓✓Kuna aina 4 za vyakula vya kiroho na vyakula hivyo wachungaji na wahubiri wote wanatakiwa kuhusika navyo katika kuwalisha watu wa MUNGU ili watu wa MUNGU wakue kiroho.
A.Vyakula vya kulinda mwili;
✓✓Mfano kufundisha watu wa MUNGU kujiepusha na dhambi na kuwafundisha hila za shetani ambazo wanatakiwa kuziepuka, wakiziepuka hila hizo za mawakala wa shetani hakika hapo unakuwa umeulinda Mwili wa KRISTO ambao ndio Kanisa. 
✓✓Kuwafundisha watu wajitenge na mafundisho ya uongo, hapo hakika unakuwa unawalinda watu hao ambao ni kanisa la MUNGU. 
✓✓Kanisa lazima lilindwe ili shetani asipate nafasi katika Kanisa, mafundisho ya namna hiyo mimi nayaita vyakula vya kiroho vya kuulinda mwili, yapo mengi na sio hayo tu ila kwa mifano miwili ni hiyo.
Matendo 20:28 ''Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo ROHO MTAKATIFU amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.''
B. Vyakula vya kujenga mwili;
✓✓Mfano wa vyakula vya kiroho vya kuwajenga watu ni kuwafundisha imani, kuwafundisha jinsi ya kutembea na MUNGU, kuwafundisha kazi za ROHO MTAKATIFU ndani yao n.k
Waefeso 2:20-22 ''Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye KRISTO YESU mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika BWANA. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya MUNGU katika ROHO.''
✓✓Kujengwa juu ya msingi wa mitume na manabii maana yake Neno la MUNGU walilofundisha mitume na manabii wa ndani ya Biblia linatujenga, Neno la KRISTO linatujenga kiroho na linatuunganisha hadi tunakuwa hekalu la MUNGU na tunakuwa makazi ya ROHO MTAKATIFU.
 Vyakula vya kuwajenga watu kiroho ni lazima viwepo.
C. Vyakula vya kutoa uchafu(dhambi) mwili:
 Vyakula hivi vya kiroho navyo ni muhimu sana. 
✓✓Mfano ya vyakula hivi ni Neno la kuwafungua watu waliokuwa wamefungwa na nguvu za giza.
✓✓ Mapepo ni uchafu, dhambi ni uchafu, mila za kipepo ni uchafu, kujitegemea pasipo MUNGU ni uchafu n.k
◼️Ziko sumu nyingi za kishetani ambazo watu walimezeshwa kipindi hawajampokea YESU, sumu hizo za kipepo ni lazima ziondoke ndani ya watu wa MUNGU.
✓✓Yako masomo mengi anayofunua ROHO MTAKATIFU ili watu wafunguliwe.
Kumbuka kazi mojawapo ya Bwana YESU iliyomfanya aje duniani ni ''Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. -1 Yohana 3:8b ''
D. Vyakula vya kuupa mwili nguvu:
✓✓ Vipo vyakula vingi sana vya kiroho vya kuupa mwili wa KRISTO nguvu, mfano mmoja wapo ni kufundisha sana juu ya maombi maana maombi huambatana na nguvu za MUNGU na nguvu hizo zikiwa ndani ya mwili wa KRISTO ambao ni mteule basi hakika mteule huyo atakuwa na nguvu daima.
1 Nyakati 16:11 '' Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote. ''
✓✓Mwili wa KRISTO lazima ule chakula cha kiroho cha kuupa nguvu.
Chakula cha kiroho ni Neno LA MUNGU.
Wakristo ni kanisa na kanisa ni mwili wa KRISTO.
Mkristo ni mwili wa KRISTO.
Ili mwili utimilike ni lazima mwili huo upokee vyakula vya aina hiyo 4 niliyoitaja.
Chakula ni neno La MUNGU.
Kuna watu hupenda vyakula vya kujenga mwili tu lakini chakula cha kulinda mwili hawahitaji ndio maana afya zao za kiroho zinazorota maana wamekosa chakula cha kulinda mwili.
Kuna watu hupenda tu chakula cha kulinda mwili lakini chakula cha kutoa uchafu hawakitaki wakati uchafu huo mwilini hadi utoke ndio watakuwa na afya nzuri ya kiroho.
Chakula cha kulinda mwili ni maombi.
Chakula cha kutoa uchafu mwilini ni neno la maonyo ili watu watubu na kukimbilia toba kwa BWANA YESU ndio uchafu(dhambi) wao utaondoka.
2. Ili ukue kiroho unatakiwa kuliweka Neno la MUNGU kwenye vitendo.
Kuongezeka kiroho hutokana na mambo yafuatayo.
◼️Maisha ya maombi.
✓✓Baada ya kujifunza Neno la MUNGU ambalo linakuelekeza maombi na kisha ukaingia katika maombi na ukawa unatembea katika maombi siku zote, basi hapo neno la MUNGU ulilojifunza umeliweka katika vitendo, hiyo hukufanya ukue kiroho.
◼️Maisha ya ibada.
✓✓Ulilisikia Neno la MUNGU linalokuelekeza umuhimu wa kuhudhuria ibada kila mara na umezingatia Neno hilo, hapo unakuwa umeliweka Neno katika vitendo.
◼️Maisha ya kushuhudia wengine injili ya KRISTO.
✓✓ Umejifunza Neno la MUNGU juu ya umuhimu wa kuwashuhudia wengine injili ya KRISTO, unaposhuhudia hakika umeliweka Neno la MUNGU katika vitendo, na hiyo ni njia mojawapo ya kukua kiroho maana MUNGU atakutumia hata huko kwenye kushuhudia.
◼️Kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU.
✓✓ Umejifunza kuhusu ROHO MTAKATIFU na umeamua kumtii na kumsikiliza kila siku, hiyo itakupa faida na zaidi ya faida katika kukua kiroho.
◼️Maisha matakatifu.
 ✓✓Unapoanza kuishi maisha matakatifu baada ya Neno la MUNGU kukujulisha basi hapo unakuwa umehamishia Neno katika matendo na ndivyo Biblia inavyotaka.
✓✓Mfano umefundishwa FAIDA ZA MAOMBI na MAOMBI YA KUFUNGA, vitendo vinavyotokana na Neno hilo ni wewe kuwa muombaji, kuhudhuria mikesha ya maombi na kutenga muda wa kuwa na maombi ya kufunga.
Kumbuka ili ukue kiroho Biblia inasema yafuatayo.
Yakobo 1:22-25 " Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake."
Mfano umefundishwa JINSI YA KUISHI MAISHA MATAKATIFU , vitendo ni kuhakikisha unaishi maisha matakatifu katika mienendo yako yote.
Umefundishwa FAIDA ZA MATOLEO, vitendo hakikisha unakuwa mtoaji na toa kwa moyo wa upendo.
Mfano umefundishwa MAADUI WA IMANI, vitendo ni hakikisha unajiepusha na maadui wa imani.
3. Ili ukue kiroho unatakiwa kuzaa matunda.
Bwana YESU anasema juu yako Mteule kwamba " Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni.-Yohana 15:16"
Uzaeje matunda?
◼️Ukiwashuhudia watu injili unazaa matunda.
✓✓Ukiwaombea watu na nguvu za Giza zikawatoka umezaa matunda, na kuzaa matunda ni njia mojawapo ya kukua kiroho kwa haraka.
✓✓Kuzaa matunda katika KRISTO ndio matokeo ya kukua kiroho.
✓✓Ukifanya huduma mfano uinjilisti, uimbaji n.k unakuwa unazaa matunda katika ufalme wa MUNGU na hatua hiyo ni ukuaji wa kiroho.
Hivyo ili ukue kiroho hakikisha unazaa matunda.
Ndugu Fanya juhudi za kukua kiroho ukizingatia maelekezo hapo juu.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments