ILI UOMBE LOLOTE KWA MUNGU NA ULIPATE ZINGATII HII.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

✓✓Inawezekana wewe ni mkristo muombaji, safi sana.

✓✓Inawezekana wewe unalohitaji unataka MUNGU akutendee, Ubarikiwe kwa kumhitaji MUNGU.

Katika maombi kuna kanuni nyingi za kibiblia za kukusaidia uombe kwa MUNGU na kupokea, kanuni mojawapo ni hii ambayo nakufundisha leo, inawezekana ikawa ndio kanuni kuu zaidi ya zingine.

◼️Ni kwamba ukitaka MUNGU akujibu mahitaji yako timia katika Neno lake.

Yohana 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa."

1. Kaa ndani ya YESU KRISTO.

✓✓Kukaa ndani ya YESU KRISTO ni kumpokea YESU kama Mwokozi wako kisha unaanza kufuata uongozi wake kila siku, KRISTO anatuongoza kwa Neno lake ambalo ni Biblia takatifu.

Yohana 15:4 "Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu."

✓✓Kaa ndani ya YESU KRISTO ndipo utajibiwa maombi yako.

2. Neno la KRISTO likae ndani yako.

Wakolosai 3:16-17 " Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye."

✓✓Hakikisha Neno la MUNGU ambalo ndilo pia Neno la KRISTO, hakikisha linakaa ndani yako.

✓✓Neno la MUNGU likikaa ndani yako hutatenda dhambi, utazijua haki zako katika MUNGU hata uone umuhimu wa kuomba, Neno la KRISTO litakupa maarifa ya kuomba.

✓✓Neno la MUNGU litakufanya umshinde shetani na kila Nguvu za giza.

◼️Hivyo ukitaka uombe na kupokea kwa MUNGU hakikisha uko ndani ya KRISTO huku pia Neno la KRISTO likiwa ndani yako.

Ili uombe na kupokea kwa MUNGU hakikisha uko ndani ya KRISTO na neno la MUNGU liko ndani yako.

3. Uwe muombaji.

Mathayo 7:7-11 "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?''

◼️Ukitaka MUNGU akujibu maombi yako hakikisha uko ndani ya KRISTO, neno la KRISTO liko ndani yako na uwe sasa muombaji asiyekata tamaa.

✓✓Uwe muombaji pia anayeomba kwa imani.
MUNGU akukumbuke na kukubariki ukifanyia kazi Neno lake hili.

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments