![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Kama unatamani kumuona MUNGU katika KRISTO YESU katika maisha yako jiulize maswali haya:
1. Je unampenda MUNGU kiwango gani?
2. Je uko katika Wokovu wa KRISTO YESU?
3. Je huwa unamtii MUNGU katika mambo yote?
4. Je unaongozwa na ROHO MTAKATIFU?
5. Je unaishi maisha matakatifu?
6. Je unazaa matunda mema katika kazi ya MUNGU?
7. Je umejitenga mbali na machukizo ya dunia?
◼️Kwa mambo hayo 7 je umegundua kama ni kweli unampenda MUNGU?
✓✓Kama unampenda hakikisha unampenda MUNGU kwa kiwango kikubwa sana.
Marko 12:30 "nawe mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote."
◼️Kama unampenda MUNGU hakikisha uko ndani ya Wokovu wa Mwanaye yaani Wokovu wa YESU KRISTO Mwokozi.
Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."
◼️Kama unampenda MUNGU hakikisha unamtii katika mambo yote.
Yakobo 4:7-10 " Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza."
◼️Kama unampenda MUNGU hakikisha unaongozwa na ROHO MTAKATIFU siku zote.
Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."
◼️Kama unampenda MUNGU hakikisha unaishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
◼️Kama unampenda MUNGU hakikisha unazaa matunda mema katika kazi ya MUNGU kwa kumtumikia MUNGU, kuipeleka injili kwa mali zao, kuombea kazi ya MUNGU na watumishi wa MUNGU n.k
Yohana 15:16 "Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."
◼️Kama unampenda MUNGU hakikisha umejitenga mbali na machukizo yote ya duniani hii.
1 Yohana 2:15-17 " Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba(MUNGU), bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele."
✓✓Ndugu hakikisha unampenda MUNGU kwa wewe kutimia katika mambo hayo matano hapo juu.
◼️Pia kumbuka kwamba ukitaka kumwona MUNGU katika maisha yako basi uwe na moyo safi.
Mathayo 5:8 "Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona MUNGU."
◼️Ukitaka kumuona MUNGU katika maisha yako hakikisha unampenda na kumtafuta kwa bidii.
Mithali 8:17 "Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona."
◼️Ukitaka kumwona MUNGU katika maisha yako hakikisha unamtafuta kwa bidii, hakikisha unamtegemea yeye na kumtumaini yeye na mwisho hakikisha unamtafuta MUNGU kwa maombi ya imani.
Waebrania 11:6 "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao."
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments