JE WEWE NI MKRISTO?

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Ombi langu ujumbe huu ausome kila Mkristo aliyeokoka.
Ausome hadi mwisho maana ni ujumbe mfupi.

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

Kama wewe ni Mkristo nisikilize maana nina ufunuo huu.

◼️Watu wengi walimwamini YESU KRISTO kule Samaria kwa sababu ya mwanamke mmoja.

Yohana 4:39 "Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda."

✓✓Je wewe umekuwa sababu ya watu wangapi kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao?

◼️Filipo alikuwa sababu ya Nathanaeli kumwamini YESU KRISTO na kumfuata?

Yohana 1:45-48 " Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, YESU, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. Basi YESU akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? YESU akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona."

✓✓Je wewe umekuwa sababu ya nani kumpokea YESU KRISTO?

✓✓Umekuwa sababu ya watu wangapi kuokoka?

◼️Petro alikuwa sababu ya Watu wengi sana wa Yerusalemu kuokoka.

Matendo 2:37-42 " Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na BWANA Mungu wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali."

✓✓Wewe je umekuwa sababu ya watu wangapi kuokoka?

✓✓Je umekuwa sababu ya watu wangapi kujitenga na mizimu ya ukoo, uganga na kujitenga na miungu?

✓✓Umekuwa sababu ya watu wangapi kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao?

◼️Filipo alikuwa sababu ya mkushi kuokoka na kubatizwa.

Matendo 8:37-38 " Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza."

✓✓Je wewe umekuwa sababu ya watu wangapi kuokoka?

◼️Ndugu hakikisha unakuwa sababu ya watu wengi kumjua MUNGU wa kweli ambaye amejifunua pekee katika KRISTO YESU.

◼️Hakikisha unaujenga mwili wa KRISTO ambao ni Kanisa.

◼️Hakikisha unakuwa sababu ya maelfu ya watu kuokoka.

◼️Hakikisha unafanyika mtumishi mwaminifu wa MUNGU katika KRISTO YESU.

1 Wakorintho 4:1 "Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU."

Mimi binafsi kama Peter Mabula nilijiwekea Ahadi moyoni kwamba kila mwaka angalia niwe nimewaongoza Sala ya Toba watu 10, hayo ni malengo yangu tangu naokoka mwaka 2008. MUNGU alinipa Neema hiyo ni Kuna Miaka niliongoza Sala ya Toba watu zaidi ya 200.
Ndugu yangu, kumbe Inawezekana, jiwekee malengo katika kazi ya Injili ya KRISTO iokoayo.
Sio lazima wote tuwe wahubiri lakini hata ukialika watu Kanisani umemtumikia MUNGU wa Mbinguni, unaweza kujiwekea Ahadi moyoni kwamba angalau kila mwaka uwe umewaalika tu Kanisani watu 200, watu hao wakifika Kanisani watakutana na Watumishi wa Bwana YESU hivyo watafundishwa na wengine wataokoka kwa sababu Yako, hapo utakuwa umeihubiri sana Injili.
Jiwekee hata sadaka kila mwezi au kila baada ya miezi ili kuwatumia Watumishi waaminifu wa MUNGU katika KRISTO YESU ambao unawafahamu Wana kazi ya kuipeleka Injili ya KRISTO ili sadaka Yako hiyo iwapeleke, iwasaidie kupata vifaa vya Injili n.k
MUNGU anajua yote hivyo anajua ni Wewe umeifanya kazi yake hata Injili Yake njema inahubiriwa.

◼️◼️Ndugu, Hakikisha Kwa namna Moja au nyingine kama kweli Wewe ni Mkristo basi ipeleke Injili.

✓✓Pia Kumbuka na hakikisha unakuwa barua njema inayosomwa na watu wote kwa mema na sio mabaya.

2 Wakorintho 3:3-4 " mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya KRISTO tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa ROHO wa MUNGU aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama. Na tumaini hilo tunalo mbele za MUNGU kwa njia ya Kristo."

✓✓Ndugu katika maisha yako ya Wokovu hakikisha utamtumikia MUNGU wa Mbinguni.

◼️Utumishi mkuu kwa MUNGU ni wewe kuokoka na kuwa sababu ya wengine kuokoka.

✓✓Uwe sababu ya wengine kuokoka kwa wewe kuwashuhudia injili ya KRISTO YESU uokoaji.

✓✓Uwe sababu ya wengine kuokoka kwa wewe kuwapeleka wahubiri au kuwawezesha wahubiri kwa pesa zako ili Injili ya KRISTO iende mbele.

✓✓Uwe sababu ya wengine kuokoka kwa wewe kuwafundisha Neno la MUNGU.

✓✓Uwe sababu ya wengine kuokoka kwa wewe kuwaalika Kanisani au kwenye mikutano ya Injili, wengi huwaalika tu waliokoka wenzao lakini kwa MUNGU wanatafutwa zaidi ambao hawajaokoka ili waokoke.

✓✓Uwe sababu ya familia yako na ukoo wako kumgeukia MUNGU wa kweli ambaye amejifunua pekee katika KRISTO YESU.

✓✓Ndugu ubarikiwe sana kama ukiwa sababu ya watu hata 10 tu Kwa mwaka kuokoka.
MUNGU akubariki sana sana ukifanyia kazi ufunuo huu.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments