![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Hebu soma somo lote hata kwa kujilazimisha.
◼️Kila mtu kuna mahali ametoka, kuna mahali yuko na kuna mahali anaelekea.
Mimi sijui wewe umetoka wapi, uko wapi sasa na unaelekea wapi.
✓✓Yuko mtu alitoka dhambini, kwa sasa yuko katika Wokovu wa KRISTO na anaelekea uzima wa milele.
Wafilipi 3:20 "Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana YESU KRISTO;"
✓✓Yuko mtu ametoka kwenye umasikini, yuko sasa katika kutafuta kazi na anakoelekea ni kwenye kupata kazi.
3 Yohana 1:2 "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo."
✓✓Yuko mtu ametoka kwenye Wokovu wa KRISTO, kwa sasa yuko dhambini na anakoelekea ni jehanamu.
Ufunuo 21:8 "Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."
Luka 18:41-43 " Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona. YESU akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya. Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza MUNGU. Na watu wote walipoona hayo walimsifu MUNGU."
Je wewe umetoka wapi, uko wapi sasa na unaelekea wapi?
Je umetoka kuzuri na uko sasa kwa kutafuta mganga ili uelekee kubaya?
Mara ngapi umeonywa uachane na waganga wa kienyeji ukashupaza shingo?
Mithali 29:1 "Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa."
Yaani badala ya kumtegemea MUNGU wa Mbinguni katika KRISTO YESU unategemea Wanadamu waganga? Kuna laana ya MUNGU kwa watu wa aina Yako.
Yeremia 17:5-6 " BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu."
Warumi 1:21-22 " kwa sababu, walipomjua MUNGU hawakumtukuza kama ndiye MUNGU wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;"
2 Petro 2:22 "Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni."
Yakobo 1:14-16 " Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike."
Kumbu 31:20 "Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu."
Mathayo 12:39 ''Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.''
Yuda 1:4 "Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya MUNGU wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu YESU KRISTO.
Je uko kwa YESU KRISTO na unaelekea uzima wa milele?
◼️Nakushauri uwe sasa katika Wokovu wa KRISTO ili uelekee uzima wa milele.
/✓✓Haijalishi ulitoka kubaya sana ila hakikisha sasa uko katika sehemu inayompendeza MUNGU, umeokoka na unaelekea uzima wa milele.
Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."
✓✓Ndugu hakikisha unaelekea uzima wa milele.
✓✓Baba au Mama hakikisha unaelekea uzima wa milele.
✓✓Kijana au Binti hakikisha unaelekea uzima wa milele.
✓✓Mtoto au mzee hakikisha unaelekea uzima wa milele.
✓✓Mtu wa Kanisa hakikisha unaelekea uzima wa milele.
MUNGU akubariki sana ukitengeneza na Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments