![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu kujifunza Neno la MUNGU.
◼️Ukimwamini MUNGU unaimalishwa, ukiwaamini watumishi wa MUNGU unafanikiwa.
2 Nyakati 20:20b ".... mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa."
Kumwamini MUNGU ni nini?
✓✓Kumwamini MUNGU ni kumkubali na kukubaliana na uweza wake kisha kunyenyekea chini yake katika KRISTO YESU huku ukimtegemea.
Yohana 14:1 "Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi."
✓✓Kumwamini MUNGU pia ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako maana MUNGU wa kweli amejifunua tu katika KRISTO YESU Mwokozi.
Wakolosai 2:9 "Maana katika yeye(YESU) unakaa utimilifu wote wa MUNGU, kwa jinsi ya kimwili."
Kuwaamini watumishi wa MUNGU ni nini?
✓✓Kuwaamini watumishi wa MUNGU ni kuzingatia maneno ya MUNGU sahihi ya wanayotuambia kwa jinsi ya KRISTO YESU.
✓✓MUNGU husema kupitia watumishi wake waaminifu, MUNGU hutenda kupitia watumishi wake waaminifu.
✓✓Usipowaamini watumishi waaminifu wa MUNGU katika KRISTO YESU ujue utakuwa unazuia miujiza yako katika hitaji lako.
◼️Mwamini Mtumishi wa kweli wa Bwana YESU ndipo utafanikiwa.
Kutoka 14:31" Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake."
✓✓MUNGU anataka watu wawaamini watumishi wake, ukimwamini Mtumishi wa kweli wa MUNGU katika KRISTO YESU utafanikiwa.
2 Nyakati 20:20b ".... mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa."
✓✓MUNGU anataka watu waamini watumishi wake, ukimwamini Mtumishi wa kweli wa MUNGU katika KRISTO YESU ujue umefuata kufanikiwa kwako.
Inawezekana unateswa na nguvu za giza, wewe kumwamini Mtumishi wa kweli wa Bwana YESU KRISTO kwamba anaweza kukuombea kwa MUNGU na ukafanyia kazi Neno la MUNGU analokufundisha Mtumishi huyo ujue utazishinda hizo nguvu za giza zinazokutesa.
Inawezekana adui zako wamekufunga mikono kiroho ili usifanikiwe katika kazi yako, ukimwamini Mtumishi wa MUNGU na ukafanya kazi Neno la MUNGU analokufundisha alilopewa na ROHO MTAKATIFU kwa ajili Yako utafunguliwa na ndipo mafanikio yako yatatokea.
Inawezekana umerushiwa roho ya kukataliwa au roho ya mauti, ukimwamini Mtumishi mwaminifu wa KRISTO na ukalifanyia kazi Neno la MUNGU analokufundisha alilopewa na ROHO MTAKATIFU utafunguliwa na hizo mipango za shetani hazitagusa maisha yako tena.
✓✓Hakikisha unamwamini MUNGU na waamini watumishi wake waaminifu katika KRISTO YESU Mwokozi.
Usipomwamini Mtumishi wa MUNGU hutaweza kuliamini Neno la MUNGU analofundisha, na kama hutaliamini Neno la MUNGU hutalifanyia kazi na kwa sababu hutalifanyia kazi basi hutafunguliwa, utabaki na tatizo lako.
Ndugu, mwamini MUNGU na waaminifu watumishi wake waaminifu aliowatuma.
2 Nyakati 20:20b ".... mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa."
Ngoja nikupe baadhi ya shuhuda zinazonihusu mimi Peter Mabula katika utumishi wangu kwa KRISTO.
◾Nianze na ushuhuda kabla sijaokoka, nikiwa sekondari miaka ya 2003 kuna siku niliumwa sana hata nilijua sitapona, ugonjwa ulianza asubuhi na niliteseka katika kiwango ambacho nilishindwa hadi kutembea. Ilipofika jioni saa kumi na mbili nilijikuta nawasha redioni na kukutana na mahubiri ya Mwalimu Mwakasege akifundisha kwa njia ya cd redioni yaani haikuwa live, baada ya muda mfupi alianza kuombea na ajabu Bwana YESU akaniponya saa ile ile.
Kwanini nilipona?
Ni kwa sababu nilimwamini MUNGU katika KRISTO YESU na nilimwamini Mtumishi wake.
Nisingemwamini Mtumishi yule ningebadilisha kituo cha redio cha kusikiliza.
Kumwamini MUNGU na Mtumishi wake kulinipa kupona ugonjwa mbaya.
Ndio maana Biblia inasema
2 Nyakati 20:20b ".... mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa."
◾Miaka mingi kidogo iliyopita kuna siku moja kuna dada mmoja alikuwa anaumwa ukimwi akanipigia simu nimuombee, katika maelezo yake alisema kwamba ameshawaendea watumishi wengi na hakupona hivyo mimi Peter Mabula nitakuwa wa mwisho kumuombea, kama nikishindwa hafuati maombezi tena, nilimkemea katika hilo kisha Nitamuombea kwa siku kadhaa kisha Bwana YESU akampa neema kwa kumponya kupitia maombi hayo.
Kama dada huyu asingeniamini basi asingekubali nimuombee.
Kumwamini kwake YESU KRISTO na kuniamini mimi Mtumishi wa YESU kulileta uponyaji kwake baada ya kumuombea.
Sio kwamba wote walionijia niwaombee walipona, wengine hata hawakupona lakini wale ambao MUNGU amewapa neema kupitia maombi yangu walipona, kuwaamini watumishi waaminifu wa MUNGU kuwaweza kuwa sababu ya uponyaji wako.
◾Dada mmoja siku moja aliniambia mambo ambayo sikuwa nayajua.
Alisema kwamba ananiomba msamaha maana siku ya kwanza namuombea hakuniamini kwa sababu sauti yangu sio nzito kama watumishi wengine hivyo hakuamini kama maombi ya sauti yangu isiyo nzito yanaweza kufukuza nguvu za giza, baada ya kumuombea akaona mabadiliko ya ajabu na baada ya muda akajibiwa mahitaji yake aliyokuwa anahitaji ndipo akaona alinikosea sana kwa kutokuniamini kutokana na sauti yangu isiyo nzito au isiyo ya kuunguruma.
◾Nikiwa Zanzibar miaka ya 2010 yaani miaka miwili tangu nilipookoka, Mama mmoja alikuwa anachezewa na wachawi kwa kunyolewa nywele sehemu za siri, baada ya kuteseka kwa muda mrefu alikuja Kanisani kwetu ili kuombewa na Mchungaji, bahati mbaya kwake alimkuta Mchungaji yuko safarini nje ya Zanzibar, nilipomueleza kwamba Mchungaji Yuko Dodoma kihuduma akaanza kuondoka kwa hasira hadi nikipomsimamisha na kumwambia kwamba kama anahitaji Maombezi basi mimi na vijana wadogo niliokuwa nao hapo Kanisani tunaweza kumuombea na akaondoka katika mateso ya uchawi.
Alipotii alipona katika hilo hadi akanipa ushuhuda mzuri mrefu juu ya muujiza huo alioupata.
Watu wengi wamebaki katika matatizo yao ya kiroho kwa muda mrefu kwa sababu tu hawamuamini MUNGU na hawawaamini watumishi wake kupitia Neno la KRISTO wanalofundisha .
Ngoja nikupe baadhi ya faida za kumwamini MUNGU.
1. Ukimwamini MUNGU na ukakubaliana naye unahesabiwa haki.
Mwanzo 15:6 "Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki."
Warumi 4:3 "Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini MUNGU, ikahesabiwa kwake kuwa haki."
2. Ukimwamini MUNGU na ukamuomba akuokoe dhidi ya maadui atakuokoa.
2 Samweli 22:3-3 " MUNGU wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu."
3. Kumwamini MUNGU ni baraka.
Mithali 16:20 "Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri."
4. MUNGU huleta ulinzi kwa wanaomwamini.
Mithali 30:5 "Kila neno la MUNGU limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio."
5. Kumwamini YESU kama Mwokozi ni njia ya uzima wa milele.
Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."
6. Wanaomwamini YESU KRISTO kama Mwokozi wao huhesabiwa haki mbele za MUNGU.
Matendo 13:39 "na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa."
✓✓Ndugu waige hawa ambao walimwamini MUNGU wa Filipo kisha wakaliamini Neno la KRISTO alilofundisha Filipo hadi wakabatizwa na kufunguliwa.
Matendo 8:12 "Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa MUNGU, na jina lake YESU KRISTO, wakabatizwa, wanaume na wanawake."
7. Ukimwamini MUNGU katika KRISTO YESU itakuwa vilevile kama yeye MUNGU alivyokusemesha.
Matendo 27:25 "Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini MUNGU, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa."
8. Kila amwaminiye YESU KRISTO hatatahayarika.
Warumi 10:10-11 " Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika."
9. Kumwamini YESU KRISTO ni njia pekee ya kumpokea ROHO MTAKATIFU.
Waefeso 1:13 "Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na ROHO yule wa ahadi aliye Mtakatifu."
10. Kuna ujasiri na uwezo katika kumwamini YESU KRISTO.
Waefeso 3:11-12 " kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika KRISTO YESU Bwana wetu. Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini."
11. Kumwamini MUNGU huleta furaha na amani.
1 Petro 1:8 "Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,"
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments