![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU.
✓✓Njia mojawapo aliyotupa MUNGU ili tutambue kilichopo kwenye ulimwengu wa roho ni kwa kupitia ndoto na maono.
Watu wengi sana wanaomba maombi ya kujinasua na vifungo mbalimbali lakini walipojulishwa kwa ndoto au maono juu ya vifungo hivyo vya giza kwa kupitia kuona mashambulizi katika maeneo ya miili yao hawakushughulikia kimaombi hivyo tatizo likaendelea kuwapata hata kama wanatamani tatizo hilo litoke, ila tu hawakujua wanatakiwa kupambana na nini kwenye maombi.
✓✓Ndugu, katika KRISTO YESU umepewa mamlaka ya kuomba hivyo itumie nafasi hiyo ili ushinde vita vya kiroho.
Yeremia 51:20-21 " Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;"
Ndugu, usipohusika na maombi katika Jina la YESU KRISTO tatizo lako litaaendelea kukutesa.
Kila tatizo unaloliona kwenye ulimwengu wa roho kwenye eneo fulani la mwili wako, hakikisha unajua namna ya kuomba ili kuondoa tatizo hilo kiroho.
Ngoja nikupe mifano hai michache ambayo Mimi Peter Mabula kutoka kwa baadhi ya watu ambao niliwahi kuwasiliana nao kwenye huduma ili unielewe vyema kabla sijaendelea na ujumbe wa leo.
Ndugu mmoja aliota chura anaingia kwenye unyayo wa mguu wake wa kulia na kupotelea mwilini, tangu siku hiyo ndugu huyo anaumwa mguu na hata wakati mwingine anashindwa kutembea.
Mama mmoja siku moja aliota ndoto mkono wake wa kushoto umepakwa kinyesi, tangu siku hiyo watu wakaanza kumdharau na hadi watoto wake wa kuzaa wakaanza kumchukia, hata aliowasaidia sana wakamgeuka.
Mtu mmoja aliota mikono yake imefungwa na kamba, kila akijaribu biashara yeyote hafanikiwi, anakula hadi mtaji na kufilisika.
Ngoja nikujulishe kwenye ulimwengu wa roho mkono unaposhambuliwa inajulisha nini.
Mikono ina maana nyingi kiroho hivyo unaposhambuliwa mikono ndotoni au unapoota mkono mmoja umedhurika ujue na kutambua ni nini kimelengwa kwako kuharibiwa na nguvu za giza.
Mtu mmoja aliota ndoto mkono wake wa kulia unashambuliwa na nyoka hakujua maana yake hadi alipoingia katika matatizo yaliyosababishwa na hiyo roho ya kuzimu iliyo katika umbo la nyoka.
Ngoja tuangalie maandiko.
Mithali 3:16 "Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto."
✓✓Ukishambuliwa na nguvu za giza kwenye mkono wa kiume ujue nguvu za giza zinawinda uhai wako maana mkono wa kiume kiroho umebeba wingi wa siku, hivyo ukiona unashambuliwa na chochote kwenye ulimwengu wa roho kwenye mkono wako wa kulia ujue nguvu za giza wanajaribu kuhakikisha hauishi miaka mingi yaani wanakuletea tatizo ambalo litakuletea matatizo yanayolenga usiishi miaka mingi.
Hata Adamu alifukuzwa Edeni ili asije akatumia mkono wa kulia kuchukua tunda kisha akaishi milele(Mwanzo 3:22)
Kuna uhusiano wa kiroho kati ya mkono wa kulia na kuishi miaka mingi.
Mawakala wa shetani hawataki uishi miaka mingi hivyo wanafanya kila mipango ya kipepo kukatisha uhai wako, ndio maana unaota mkono wako wa kulia ukishambuliwa na nguvu za giza, wanyama au Watu wabaya, Ukiona ndotoni adui anawinda mkono tu wa kulia elewa Leo kwamba anawinda uhai ili usiishi Miaka mingi.
Lipo Jina la YESU KRISTO ambalo Lina ushindi wote juu ya Nguvu za giza na dhidi ya mipango yote ya kichawi, omba leo katika Jina la YESU KRISTO ukipambana na kila uliyewahi kumuona akiwinda mkono wako wa kuume.
Kwa sababu Biblia inasema kuna wingi wa siku za kuishi katika mkono wa kiume, hivyo ukishambuliwa mkono wa kiume tambua ni nini kinawindwa na mawakala wa shetani.
Ukiwa unaongea na watu mbalimbali ni rahisi tu kusikia mara mtu ameumwa na nyoka mkono wa kulia ndotoni, mara simba, au paka wengine chui au mtu au viumbe hai wengine wameshambulia mkono wake wa kuume , ndugu tambua kinachowindwa na hizo nguvu za giza.
✓✓Ukiona ni mkono wa kushoto ndio unawindwa na nguvu za giza au unashambuliwa na nguvu za giza, tambua kwamba adui anawinda uchumi na heshima.
Mithali 3:16 "........ Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto."
Ukiona mkono wa kushoto ndio unashambuliwa ndotoni ujue adui anafanya kila mbinu kuhakikisha wewe huheshimiwi na maana nyingine pia ni kwamba shambulio la mkono wa kushoto ndotoni ni kwamba adui anakuzuia kufanikiwa kiuchumi.
Ndugu, tambua hicho ulichokiona kinashambulia mikono kinawakilisha nini?
Ukiona kwenye ndoto au maono adui awawinda tu mkono wa kushoto elewa kinawindwa nini na ukiona unalengwa zaidi mkono wa kulia elewa kinalengwa nini ili ujue namna ya kuomba katika Jina la YESU KRISTO.
Ukishambuliwa mkono wa kushoto tu.
Tambua kwamba kinachowindwa ni utajiri na heshima (Mithali 3:16) Unaweza kuwa unafanya biashara, kazi au kilimo na mara kwa mara unaota ukishambuliwa mkono wa kushoto tu au ukifanyiwa jambo baya mkono wa kushoto, ndugu tambua hilo ni shambulio la kishetani linalolenga kukusababisha usiheshimiwe na watu na usiwe na uchumi mzuri.
Tambua kwamba kinachowindwa ni utajiri na heshima (Mithali 3:16) Unaweza kuwa unafanya biashara, kazi au kilimo na mara kwa mara unaota ukishambuliwa mkono wa kushoto tu au ukifanyiwa jambo baya mkono wa kushoto, ndugu tambua hilo ni shambulio la kishetani linalolenga kukusababisha usiheshimiwe na watu na usiwe na uchumi mzuri.
Katika mikono si tu lazima ushambuliwe bali hata kufunikwa kitu au kufungwa kitu n.k
Muhimu tambua unawindwa uchumi na heshima.
Wako watu ni wanandoa na wanadharauliwa na wenzi wao kiasi cha ndoa kujaa migogoro na wanapoomba huota ndotoni wanashambuliwa mkono wa kushoto na kumbe heshima yao imeondolewa.
Unaweza kufanya kazi yako kwa bidii kuliko wenzako hapo kazini kwenu na bado wewe unaongoza kwa kudharauliwa na kumbe lilianzia rohoni na uliona ndotoni.
Ndugu omba katika jina la YESU KRISTO na utazishinda hizo nguvu za giza zinazoshambulia mkono wako yaani zinashambulia uchumi na heshima yako, omba ndugu.
Ayubu 16:20 "Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia MUNGU machozi;"
Unapokuwa huwezi kupewa heshima ujue kinachofuata kwako ni kudharauliwa.
Kuna matatizo mengi chanzo chake ni vita ya kiroho kutoka kwa nguvu za giza, wewe unaweza kuona tatizo kwenye mkono wa kushoto na kumbe ni agenda ya kipepo ili usiheshimiwe na mtu yeyote.
Ayubu 19:18 "Hata watoto wadogo hunidharau; Nikiondoka, huninena."
Unaweza kuona nguvu za giza zikiwinda mkono wako wa kuume na kumbe wanawinda uhai wako kwa kutumia watu katika mashambulizi ya kimwili, yaani unaweza kukosana na mtu na anakutumia watu wa kukuuwa.
Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.
Lakini pia unaweza kuona wanyama ndio walishambulia mkono wako elewa ni mnyama gani na amebeba nini na anawinda nini kwako.
✓✓Mfano Ukiona simba ndio awawinda mkono wako Maana yake wakuu wako wa kazi au wakuu wa kiserikali katika eneo lako la kazi ndio una vita nao na pia wanatumia roho za vitisho ili kukuharibia au kukudhuru ili upate madhara yanayohusika na mkono kiroho kama nilivyokueleza hapo juu ya mkono una maana gani kiroho,
pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.
Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.
✓✓Ukiona ng’ombe Ni roho ya kishetani katika ukoo wako au Mizimu ndio inakuwinda, pambana na nguvu hizo za giza na utashinda.
Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.
✓✓Ukiona Mbwa Ni roho ya uzinzi na uasherati, hivyo wanawinda uhai wako kupitia wewe ili uanguke kwenye uzinzi au uasherati ili upate madhara yatokanayo na uzinifu ili usiishi Miaka mingi, mfano homa ya ini, ukimwi, homa ya manjano n.k
Hivyo jitenge mbali na dhambi hiyo inaweza kukukatisha uhai wako, hata ukiona tu mbwa analamba mkono wako elewa nini kinalengwa na hiyo roho ya uzinzi na uasherati, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.
✓✓Ukiona Nyoka Ni majini, wachawi, waganga wa kienyeji, wakuu wa giza, na kila mwanadamu aliye wakala wa giza, sasa elewa tu nini adui huyo anawinda ili ajue namna ya kuomba, Hivyo haribu roho hizo za nyoka zinazowinda uhai wako,pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.
Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.
Lakini pia kama unaota mikono yako yote ikifungwa hiyo inaweza kuwa na maana tofauti na kufuatiliwa mkono mmoja tu.
Kufungwa mikono yote Kwa kamba au chochote hiyo ina maana adui anafunga mkono kiroho ili kukuzuilia kufanikiwa katika lolote mfano mambo ya kiuchumi.
Maana yake adui anafunga mafanikio yako.
Mtu aliyefungwa mikono kiroho hata akipewa milioni 50 afanyie biashara ndani ya muda mfupi atakuwa hana hata lakini na hajui imekuwaje, adui alishamfunga mikono kiroho ili kumzuilia kufanikiwa, hapo inabidi kuomba maombi ya kufunguliwa mikono kiroho.
Nini ufanye ukiona kwenye ulimwengu wa roho mkono wako wa kulia/kuume unawindwa au unashambuliwa ?
1. Omba maombi kuharibu kila kilichoharibu kiroho mkono wako wa kuume.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."
2. MUNGU ameahidi atatimiza miaka yako.
Kutoka 23:26 "....... na hesabu ya siku zako nitaitimiza."
Hivyo dai ahadi ya MUNGU kimaombi ili muda wako wa kuishi utimie na sio mawakala wa shetani kukatisha uhai wako.
Kumbuka ahadi za MUNGU zilizo katika yeye ni ndio na kweli
2 Wakorintho 1:20 "Maana ahadi zote za MUNGU zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; MUNGU apate kutukuzwa kwa sisi."
✓✓Hivyo timiza wajibu wako wa kuomba mbele za MUNGU na atapewa.
Mathayo 7:7 "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;"
3. Takasa mkono wako kwa damu ya YESU KRISTO.
Walawi 11:44 "Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi."
4. Tumia mamlaka ya jina la YESU KRISTO kukataa kifo cha kabla ya wakati wako kilichopangwa na nguvu.
Zaburi 118:17 "Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA."
5. Jitenge mbali na dhambi ili vitu hivyo visipate nafasi ya kukutumikisha kukatisha uhai wako.
Mfano hai jitenge mbali na uzinzi na uasherati ili dhambi hiyo isikatishe maisha yako.
1 Wakorintho 6:18 "Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."
Nini ufanye juu ya shambulio la kuondoa heshima na utajiri/uchumi?
Kuhusu HESHIMA.
1. Kwa damu ya YESU KRISTO takasa mikono yako kiroho kwa maombi na kutubu.
Isaya 1:16 "Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;"
2. Ishi maisha matakatifu na ya haki katika KRISTO YESU na heshima yako itarudi.
1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
3. Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO futa kila kifungo cha giza cha kukuondolea heshima.
Yeremia 15:21 "Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha."
Kuhusu UTAJIRI/UCHUMI.
1. Tubu kwa ajili ya chanzo cha tatizo.
Isaya 59:1-3 "Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya."
2. Tembea kwenye kanuni za ki Mungu zinazoleta utajiri na heshima.
Mithali 3:9-10 "Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."
3. Fanya kazi kwa juhudi zote.
Mithali 10:4 "Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha."
Hakikisha tu unafanya kazi njema na halali.
4. Ombea ufahamu wako.
Mithali 21:5 "Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji."
5. Nyenyekea mbele za MUNGU.
Mithali 22:4 "Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima."
6. Usitegemee akili zako mwenyewe bali mtegemee MUNGU katika KRISTO YESU
Mithali 23:4 "Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe."
7. Takasa mikono yako kiroho na shughulikia tatizo hilo kiroho.
Walawi 20:7 "Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu."
8. Hitaji ulinzi wa MUNGU kwenye uchumi wako huku ukifanya kazi.
Utaupata ulinzi wa MUNGU kwenye mali zako kwa wewe kutoa sadaka na zaka pamoja na dhabihu, yaani uwe mtoaji wa zaka na sadaka ndipo utaruhusu mbingu kulinda uchumi wako.
Malaki 3:10-11 "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi."
9. Haribu vifungo vya giza vilivofunga utajiri wako.
Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."
10. Pambana na nguvu za giza zinazoshambulia uchumi wako kiroho huku ukiendelea kufanya kazi.
Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe

Comments