KWANINI UMTEGEMEE MUNGU?

Mwl Peter Mabula na Jemimah Mabula 
Watendakazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo tunajifunza kumtegemea MUNGU wa Mbinguni.

◼️Ni Muhimu sana kumtegemea MUNGU Baba wa Mbinguni.

Yeremia 17:7 "Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.'

✓✓Kuna watu wanakiri kwa vivywa vyao kwamba walimtegemea MUNGU tangu utoto, huo msimamo unatakiwa kuwa kwa watu wote.

Zaburi 71:6" Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima."

✓✓Kumtegemea MUNGU ndio pia kumtegemea Bwana YESU KRISTO, hakuna tofauti hivyo mtegemee daima.
Kabila la Yuda walimtegemea MUNGU wakawashinda ndugu zao.

2  Nyakati 13:18 "Ndivyo walivyotiishwa wana wa Israeli wakati ule, wakashinda wana wa Yuda, kwa kuwa walimtegemea BWANA, Mungu wa baba zao."

✓✓Ni jambo la baraka kumtegemea Bwana YESU KRISTO.
Ni Muhimu sana kila Mtu Duniani amtegemee.

Kwanini umtegemee MUNGU katika KRISTO YESU?

1. Unamtegemea MUNGU kwa sababu ndiye aliyekuumba tumboni mwa mama yako.

Isaya 44:24 "BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?"

◼️MUNGU Baba ndiye chanzo cha uhai wako, chanzo cha baraka zako na mwisho wako.

2. Unamtegemea MUNGU kwa sababu ndiye aliyekulinda tumboni kwa mama yako na kwa upendo wake akakutoa tumboni kwa mama yako.

Zaburi 71:6 "Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima."

3. Unamtegemea MUNGU kwa sababu ndiye anayekulinda sasa katika KRISTO YESU.

Zaburi 127:1" BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure."

4. Unamtegemea MUNGU kwa sababu ndiye aliyekuandalia Wokovu katika KRISTO YESU.

Yohana 3:16-18 "Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."

5. Ni baraka kumtegemea MUNGU.

Yeremia 17:7-8" Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda."

6. Ukimtegemea MUNGU atakulinda.

Isaya 26:3-4 " Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele."

7. Unamtegemea MUNGU katika KRISTO YESU kwa sababu ndiye MUNGU wa kweli na wa pekee.

Zaburi 83:18 "Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote."

◼️Nje na MUNGU katika KRISTO YESU, huko nje kuna miungu tu na so vinginevyo.

Ndugu mtegemee MUNGU katika KRISTO YESU na utaitwa heri.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe

Comments