![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.
Ulishawahi kujiuliza swali hili
✓✓"Kwanini YESU KRISTO alikufa na kufufuka?"
✓✓"Kwanini YESU KRISTO hayumo kaburini? "
✓✓"Kwanini Bwana YESU KRISTO alifufuka? "
Inawezekana una majibu mengi juu ya swali hilo lakini Biblia ndio ina majibu sahihi.
◼️YESU KRISTO alifufuka na yuko hai milele.
◼️YESU KRISTO alifufuka na yuko kwenye kiti cha enzi mbinguni.
◼️YESU KRISTO alifufuka, limbuko lao waliolala.
1 Wakorintho 15:12-22 " Basi, ikiwa KRISTO anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, KRISTO naye hakufufuka; tena kama KRISTO hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. ................. Maana kama wafu hawafufuliwi, KRISTO naye hakufufuka. Na kama KRISTO hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika KRISTO wamepotea. ........... Lakini sasa KRISTO amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. ............ Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika KRISTO wote watahuishwa."
Hakika Bwana YESU KRISTO yu hai.
Lakini kwa nini YESU KRISTO alifufuka?
Ngoja nikujulishe baadhi ya majibu kwanini YESU KRISTO alifufuka.
1. YESU KRISTO alifufuka kwa sababu ana mamlaka yote na uwezo wote, hata mamlaka ya kutoka mautini anayo ndio maana akafufuka.
Mathayo 28:18 "YESU akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani."
✓✓YESU ana uwezo hata wa kutoka mautini.
Yohana 10:17-18 " Ndiposa Baba(MUNGU) anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi(YESU) nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu."
2. YESU KRISTO alifufuka ili litimie Neno la MUNGU kwamba atafufuka.
Isaya 53:5-11 " Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. ..........Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake; Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao."
"Ataishi siku nyingi" maana yake baada ya kufa atafufuka tena na kuendelea kuishi.
"Atawafanya wengi kuwa wenye haki" yaani watakaompokea kama Mwokozi wao na kumuishi watakuwa wenye haki mbele za MUNGU.
Kumbe Bwana YESU alifufuka kwa sababu Neno la MUNGU lilisema atakufa na kufufuka.
1 Wakorintho 15:3-4 " Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa KRISTO alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;"
3. YESU KRISTO alifufuka ili watu wote wahubiriwe jina lake kwa ajili ya toba na ondoleo la dhambi.
Luka 24:46-47 " Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba KRISTO atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu."
✓✓Ndugu, hata mimi leo nakujulisha mapema kabisa kwamba kama hujaokoka basi tubu kwa MUNGU katika KRISTO YESU na utapata ondoleo la dhambi.
✓✓YESU yuko mbinguni lakini ukiliita tu jina lake anatokea.
✓✓YESU KRISTO yuko mbinguni lakini ukilitumia tu jina lake anatokea ili kukushindia.
4. YESU KRISTO alifufuka kwa sababu alisema atafufuka.
Mathayo 28:6 "Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa."
Andiko hili huwa linanifurahisha sana, Malaika anaeleza kwamba YESU amefufuka kama alivyosema kabla kwamba atafufuka, andiko linatoa uhakika wa ajabu sana kwamba YESU KRISTO akisema jambo lolote lazima liwe.
◼️YESU alisema atakufa na kukufuka na ikawa hivyo hivyo maana YESU akisema neno lolote lazima liwe.
✓✓Hata pale YESU aliposema watu fulani wapone walipona mfano ni Bartimayo kipofu, hata aliposema wafufuke walifufuka mfano ni Lazaro.
✓✓Hata leo akisema upone wewe unapona, akisema usiteswe tena na wachawi na majini hakika hutateswa.
✓✓YESU akisema amesema na itakuwa kama alivyosema, naomba imani yako iongozeke na endelea kumwita YESU kwa maombi na akisema kitu kwako hakika kitakuwa maana ona mfano wa ajabu ambapo alisema atafufuka na hakika akafufuka.
Ndugu imarisha imani yako kwa YESU KRISTO na sio kwa vitu ili aseme Neno juu yako na hilo hakika litakuwa kama alivyosema.
YESU akisema amesema na itakuwa kama alivyosema, alisema atafufuka na akafufuka kweli, hakuna aliyewahi kuishi duniani mwenye mamlaka kama ya YESU KRISTO.
5. YESU KRISTO alifufuka ili watu wote walio hai wawe hai kwa ajili yake.
2 Wakorintho 5:15 "tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao."
✓✓Ashukuriwe MUNGU maana YESU KRISTO alifufuka ili walio hai wawe hai kwa ajili yake.
✓✓Ni maamuzi tu ya kila mwanadamu duniani kuamua kuishi kwa ajili ya KRISTO au amkatae KRISTO ili aishi kwa ajili ya shetani kisha iwe jehanamu.
Ndugu, mimi nakushauri ishi kwa ajili ya KRISTO na sio vinginevyo.
6. YESU KRISTO alifufuka ili watakaomwamini wazaliwe mara ya pili.
1 Petro 1:3-4 " Ahimidiwe MUNGU, Baba wa Bwana wetu YESU KRISTO, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake YESU KRISTO katika wafu; tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu."
Nini maana ya kuzaliwa Mara ya pili?
◼️Kuzaliwa Mara ya pili ni kumwamini YESU KRISTO kama Mwokozi kisha kumpokea kama Mwokozi na baada ya hapo unaanza kuliishi Neno la MUNGU huku ukiongozwa na ROHO MTAKATIFU.
YESU KRISTO alifufuka ili tuzaliwe mara ya pili.
7. YESU KRISTO alifufuka ili damu yake ifanye kazi kwetu.
Marko 14:24 "Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi."
◼️Damu ya YESU KRISTO ina kazi nyingi sana kimaandiko(siku moja nitafafanua juu ya hili tu)
Kwa kifupi tu ni kwamba tumeokolewa kwa jina la YESU KRISTO lakini tumekombolewa kwa Damu ya YESU KRISTO.
✓✓Tunapozungumzia kutakaswa, inayotutakasa ni damu ya YESU KRISTO.
✓✓Tunapozungumzia kusafishwa kiroho, damu ya YESU KRISTO ndio inayotusafisha.
✓✓Tunapozungumzia ondoleo la dhambi, damu ya YESU ndio huondoa dhambi na kuzifuta.
Ulinzi, utakaso n.k damu ya YESU KRISTO inaweza kufanya kazi hizo.
Muhimu tu ni maombi katika jina la YESU KRISTO huku ukitumia damu ya YESU KRISTO huelekea hitaji lako.
◼️YESU KRISTO alifufuka ili damu yake ya thamani sana ya agano jipya ifanye kazi kwetu wanadamu tunaomtii.
Bwana YESU KRISTO mwenyewe anasema " Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. ..................... Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.- Yohana 6:54:56
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments