MALAIKA WA MUNGU AKUTOE KATIKA GEREZA ULILOPO.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Kuna Malaika wa MUNGU wenye kazi tofauti tofauti kwetu.
Leo namzungumzia Malaika wa MUNGU anayeweza kukutoa katika gereza la kiroho ulilipo, omba kwa MUNGU katika Jina la YESU KRISTO utatoka katika gereza hilo.

◼️Kuna Malaika wa MUNGU ambao kazi yao ni kuwatoa watu katika magereza.

Matendo 5:18-20 " wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;
lakini malaika wa BWANA akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,
Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu."

Mitume walikuwa katika gereza la kimwili, hiyo ikufundishe kwamba hata katika gereza la kiroho ulilipo unahitaji msaada wa MUNGU ili utoke katika gereza hilo, Malaika wa MUNGU anaweza kufanya hiyo kazi ya kukutoa katika gereza hilo.

Je uko katika gereza gani kiroho?

Je gereza lako ni magonjwa au kukataliwa?

Je gereza lako ni laana au vifungo?

Je gereza lako ni migogoro isiyoisha ya ndoa au uchumba?

Je gereza lako ni kuachwa?

Je gereza lako ni nini?

✓✓Wako watu afya zao ziko gerezani

✓✓ wako watu uzao wao uko gerezani

✓✓wako watu ndoa zao ziko gerezani

✓✓wako watu vibali vyao viko gerezani na wako watu uchumi wao uko gerezani.

◼️Leo unaweza kuomba ili kutoka gerezani na MUNGU kwa kuwatumia Malaika zake  unaweza kutoka gerezani kwa Jina la YESU KRISTO.

Siku Moja Petro aliwekwa gerezani  Kanisa likawa na Bidii ya kufanya Maombi hadi Maombi Yale yakamfanya Malaika wa kutoa watu gerezani akaenda kumtoa Petro gerezani.

Matendo  12:6-9 " Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Mara malaika wa BWANA akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.

Ndugu je uko katika gereza gani?
Je ni utasa ndio gereza lako?
Naomba kukuambia kwamba Mke wa Manoa alikuwa kwenye gereza la Utasa lakini Malaika wa MUNGU alipokuja tu utasa ukaondoka na Mama yule akamzaa Samsoni shujaa.

Waamuzi 13:2-3 " Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto. Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume."

Malaika hakuhitaji kusema mara mbili mbili ndio gereza la  Utasa kwa Mke wa Manoa liondoke Bali kwa Neno Moja utasa uliondoka na akatoka katika gereza la Utasa.

Waamuzi 13:24 "Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, BWANA akambarikia."

Je Wewe uko kwenye gereza gani?
Katika Jina la YESU KRISTO unaweza kutoka katika gereza hilo kwa Maombi katika Jina la YESU KRISTO.
Malaika anaweza kukutoa gereza kama alivyofanya kwa Petro.

Matendo  12:11 "Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa BWANA amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi."

◼️Ndugu Inawezekana hakika katika Jina la YESU KRISTO kutoka katika gereza ulilipo.

Kumbuka wale ambao walikuweka gerezani ni pamoja na mizimu, wachawi, waganga wa kienyeji, majini, washirikina, matambiko, mazindiko, kuabudu miungu, ibada za sanamu, majini, wakuu wa giza na kila mwanadamu anayetumika kipepo.

◼️Ndugu, katika KRISTO YESU ukiamua kutoka gerezani hakika unaweza hata leo kutoka  gereza hilo kwa Maombi katika Jina la YESU KRISTO.

✓✓Malaika wa MUNGU wako tayari kukutoa gerezani leo leo.

◼️Hakikisha tu unaishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU.

✓✓Kama unajua kuomba kwa MUNGU kwa imani katika KRISTO YESU unaweza kushangaa Malaika wa MUNGU anakutoa katika gereza lako.

✓✓Tambua tu namna ya kuomba ukiwatumia Malaika ili utoke katika gereza.

✓✓Omba ndugu na MUNGU akubariki.
Endelea kufuatilia masomo yangu na siku moja utakutana na ufafanuzi zaidi.

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments