![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
✓✓Inawezekana Wewe ni kiongozi wa kiroho Kanisani, ni jambo zuri na la heshima kama unatimiza kazi aliyokupa KRISTO mwenye Kanisa.
✓✓Inawekana wewe ni Askofu, Mchungaji, Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mwalimu, Mzee wa Kanisa, Shemasi, Kiongozi wa Wamama au Vijana, kiongozi wa Kwaya n.k ni Muhimu sana kuzingatia haya mambo 10 yampasayo kiongozi.
✓✓Inawezekana Wewe sio kiongozi ila ni mshirika tu Kanisani Jifunze ujumbe huu maana inawezekana siku Moja ukawa kiongozi Kanisani.
Mambo 10 ya kiongozi wa kiroho kuzingatia.
1. Kiongozi wa kiroho usiwanenee wenzako uongo.
Waefeso 4:25" Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake."
2. Kiongozi wa kiroho hakikisha una umoja na wenzako.
Zaburi 133:1" Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja."
3. Kiongozi wa kiroho hakikisha unatunza ushirika mzuri na wenzako.
1 Petro 3:8-9 " Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;
watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka."
4. Kiongozi hutakiwi kuwa na ubaguzi wala upendeleo.
1 Timotheo 5:21 "Nakuagiza mbele za MUNGU, na mbele za KRISTO YESU, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo."
5. Kiongozi wa kiroho unatakiwa uwaone wengine kama MUNGU katika KRISTO YESU anavyowaona.
1 Samweli 16:7 "Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo."
6. Epuka makundi na mgawanyiko kati yako na viongozi wenzako Kanisani.
1 Wakorintho 1:10 "Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu YESU KRISTO, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja."
7. Kiongozi wa kiroho usikubali kuwa mtu wa kuongozwa na tamaa za mwili.
1 Petro 2:11 "Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho."
8. Kiongozi wa kiroho usiwe mtu wa kiburi, maana kiburi huwashusha walionacho.
Mithali 29:23" Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa."
9. Kiongozi wa kiroho usiwe mtu wa lawama kwa viongozi wenzako.
Zaburi 69:20 "Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu."
10. Kiongozi wa kiroho epuka kuwa mtu wa mashindano.
Wafilipi 2:3 "Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake."
✓✓Ndugu, fanyia kazi na itakusaidia sana.
Haijalishi wewe ni kiongozi wa idara gani, haijalishi wewe ni Mchungaji au Askofu au mzee wa Kanisa, au shemasi, kiongozi wa kwaya au timu ya kusifu na kuabudu, kiongozi wa vijana au wamama au wababa au watoto n.k
Fanyia kazi Mambo hayo kumi.
◼️Nini viongozi wa Kanisa wafanye ili kuinua Kanisa.
1 Wakorintho 1:9-10 " MUNGU ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, YESU KRISTO Bwana wetu. Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu YESU KRISTO, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja."
✓✓ Ili kuinua Kanisa viongozi wa Kanisa lazima wanene mamoja.
✓✓Ili kuinua Kanisa viongozi wa Kanisa lazima wasiwe na mafarakano.
✓✓ Ili kuinua Kanisa viongozi wa Kanisa lazima wahitimu katika nia moja.
Lakini pia Bibla katika Wafilipi 2:3 inasema "Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake."
Hivyo kila kiongozi mzuri Kanisani anatakiwa kuwa hivi;
✓✓Kiongozi mzuri wa kiroho huwasikiliza wenzake ili waamue jambo la pamoja.
✓✓Kiongozi mzuri wa kiroho lazima awe anawakubali watu wanaomwambia ukweli pale anapokosea.
✓✓Kama viongozi Kanisani kila mmoja ana misimamo yake, mitazamo yake na itikadi zake, sasa ili Kanisa liende mbele wewe mmoja wa viongozi usilazimishe Watu wote kukubaliana na msimamo wako tu au itikadi yako tu.
1 Petro 4:9 -11 "Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika; kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za MUNGU.
Mtu akisema, na aseme kama mausia ya MUNGU; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na MUNGU; ili MUNGU atukuzwe katika mambo yote kwa YESU KRISTO. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina."
◼️Mawazo ya viongozi wote Kanisani yanaweza kuwa sahihi lakini kwa sababu mko kikaoni mkubaliane kwa upendo, usilazimishe utakacho wewe tu ndicho kipite.
✓✓ Kama kiongozi uwe mtu wa kujishusha na shirikiana na viongozi wote Kanisani kwenu.
✓✓Viongozi Kanisani lazima sana waepuke sana makundi na uongo.
MUNGU akubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments