![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu mpendwa.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
Kuna mambo matatu muhimu sana yanaweza yakakufanya wewe mteule wa KRISTO usiogope na yakakufanya ukawa jasiri sana katika maisha yako ya Wokovu.
Mambo hayo yameelezwa vyema katika Isaya 43:1
Biblia inasema mambo haya.
Isaya 43:1 "Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu."
Mambo hayo matatu ni haya.
1. Kukombolewa na YESU.
Katika andiko hapo juu Biblia inasema "Nimekukomboa "
Na katika 1 Petro 1:18-19 Biblia inasema " Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO."
✓✓Hivyo tuliokoka hatuna uoga kwa sababu tumekombolewa kwa damu ya thamani ya YESU KRISTO Mwokozi wetu.
Labda unajiuliza "Kukombolewa ni nini?
Kuna maana nne za neno kukombolewa, maana hizo ni hizi.
A. Kukombolewa ni kutolewa katika hali ya kutawaliwa, kukandamizwa, kudhulumiwa na mwingine.
◼️Sisi tumekombolewa na YESU KRISTO kwa kutolewa kwenye kutawaliwa na dhambi, shetani na kila mambo yasiyofaa.
B. Kukombolewa ni kutolewa kwenye unyonge na hali mbaya za kimaisha.
✓✓Inawezekana ulikuwa unawaogopa wachawi lakini ukijua umekombolewa kwa damu ya YESU KRISTO hutaogopa na kwa maombi utapambana nao na kuwashinda.
C. Kukombolewa ni kutolewa katika tabia mbaya mfano uzinzi, ulevi,uhuni, uabudu sanamu n.k
✓✓Sisi mwanzo tulikuwa na tabia hizo chafu mbele za MUNGU lakini kwa Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi wetu tumekombolewa kwa kutolewa katika tabia hizo chafu.
Kama wewe una hizo tabia chafu hujakombolewa au hutaki kukombolewa na YESU KRISTO yaani hutii neno la MUNGU na huutaki uzima wa milele.
Nafasi ya kukombolewa ipo hata leo, tubu, okoka kwa upya, tii neno la MUNGU na jitenge na dhambi zote.
1 Wathesalonike 5:22" jitengeni na ubaya wa kila namna."
D. Kukombolewa ni kulipiwa deni ili utoke kifungoni, uachiwe huru na uwe mali ya aliyekukomboa.
✓✓Sisi tumekombolewa na MUNGU katika KRISTO YESU kwa kulipiwa deni la dhambi.
✓✓Tumekombolewa MUNGU katika KRISTO YESU kwa kuondolewa katika vifungo vya giza na utumwa wa shetani.
✓✓Tumekombolewa na MUNGU katika KRISTO YESU kwa kuondolewa kwenye kuwa mali ya shetani na sasa tu mali ya YESU KRISTO aliyetukomboa kwa damu yake ya thamani, tumelipiwa deni na sasa tu huru.
1 Wakorintho 7:23 "Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu."
✓✓Kukombolewa na YESU KRISTO ni njia kuu ya kuondoa uoga kwetu na sasa kuleta ujasiri kwetu.
Katika mambo matatu yanayoweza kukufanya usiwe mkristo mwoga basi ni kukombolewa na damu ya YESU KRISTO iliyo ya thamani sana.
Kama hujakombolewa na YESU KRISTO mpokee leo na atakukomboa.
2. Kuitwa na MUNGU ili uwe Wokovuni.
Kuitwa na MUNGU kunapelekea kuhamishwa kama tukitii.
1 Wathesalonike 2:12 "ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa MUNGU, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake."
✓✓Ukiitwa na MUNGU na ukatii hakika hutakuwa mwoga tena maana unajua MUNGU yuko pamoja na wewe maana umemtii na unajua kwamba uko katika ufalme wake, hivyo hutaogopa vitisho vya wanadamu na nguvu za giza.
2 Timotheo 1:9 "ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika KRISTO YESU tangu milele,"
✓✓Tunapoitwa na YESU KRISTO ni muhimu tu kutii na kutembea kwenye Neno la MUNGU na tukizingatia tutakuwa hatuna uoga wowote tena.
1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
3. Ukijua wewe ni wa MUNGU na u mali yake kwa njia ya Wokovu.
✓✓Watu wengi ni waoga kwa sababu hawana uhakika kama ni wa MUNGU na wako na MUNGU wakati wote.
✓✓Watu wengi ni waoga kwa sababu wako dhambini.
✓✓Watu wengi ni waoga kwa sababu hawako na MUNGU na hawalitii Neno lake la injili ya wokovu wa KRISTO.
✓✓Watu wengi ni waoga kwa sababu bado wao ni mali ya shetani na sio mali ya YESU KRISTO, maana hawajampokea kuwa Mwokozi wao.
◼️Sasa utakuwa jasiri na sio mwoga kama tu utajua wewe ni wa MUNGU katika KRISTO YESU.
MUNGU anaposema katika Isaya 43:1 kwamba "usiogope" ni kwa sababu pia amesema kwa sababu "u wangu"
Kwa hivyo ukijua u wa MUNGU na uko pamoja na YESU KRISTO hutaogopa kamwe.
Ili uwe wake ni yeye ndiye alikuchagua.
Yohana 15:16 "Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."
◼️Tulichaguliwa na MUNGU ili tuwe wake kwa njia ya YESU KRISTO hivyo tukijua kwamba tu wa MUNGU na yeye yu pamoja nasi lazima tutakuwa majasiri.
Ni MUNGU alituchagua ili tuwe mali yake ndio maana tu majasiri.
Waefeso 1:4-5 " kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya YESU KRISTO, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake."
◼️Kila mtu duniani akiamua kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi na kuanza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu mtu huyo anakuwa amechaguliwa na MUNGU na kwa njia hiyo uoga utaondoka na ujasiri kuingia maana mtu huyo atakuwa na ROHO MTAKATIFU, atakuwa muombaji na hatakuwa na mashaka na atakuwa na Neno la MUNGU ndani yake.
✓✓MUNGU ametufanya wa thamani mbele zake kwa sababu tumekubali kuwa wake.
Isaya 43:4 "Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako."
Hivyo mambo hayo matatu humfanya mteule wa KRISTO kuwa jasiri sana.
Hata ukipita katika misukosuko hutaogopa maana MUNGU atakuwa pamoja na wewe maana amekukomboa, amekuita ukakubali na sasa u mali yake unaishi maisha safi ya wokovu hivyo hutaogopa na usiogope.
Isaya 43:2 "Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza."
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe

Comments