![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU.
✓✓Kama Weteule wa KRISTO tunajua umuhimu wa sadaka,zaka, na dhabihu.
◼️Kutoa zaka na sadaka ni njia mojawapo ya kumheshimu MUNGU.
Mithali 3:9-10 "Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."
◼️Zaka ni sehemu moja kati ya kumi na vipato vyetu ambayo tunamtolea MUNGU
✓✓Zaka pia ni asilimia 10% ya mshahara, ni asilimia 10% ya faida iliyopatikana katika biashara iwe kwa mwezi au zaidi, zaka ni fungu la kumi kwa lugha nyingine
◼️Dhabihu ni sehemu yeyote unayoitoa kwa kuiongezea katika zaka, ni sadaka ya hiari ila ina Baraka zake.
✓✓Kwa ujumla zaka, sadaka na dhabihu ni vitu vya thamani kiroho katika kanuni ya ufalme wa MUNGU.
✓✓Ndio maana ni maandiko mengi yanasisitiza kwamba watu wa MUNGU wasiende mbele za MUNGU mikono mitupu.
✓✓Utoaji ni takwa la kiroho katika kununi za mambo ya ufalme, matoleo ni moja ya vitu ambavyo Biblia inafundisha na kusisitiza.
✓✓Lakini pia ni muhimu kujua pia kwamba sadaka yoyote ukiitoa mahali ambapo MUNGU hakukusudia huwa inapoteza thamani yake.
✓✓Matoleo ni ibada, matoleo yakiambatana na maombi na utakatifu huleta matokeo makubwa sana.
✓✓Wakati mwingine matoleo husimama kama moja ya ufunguo katika mambo ya kiagano kwenye ulimwengu wa roho.
Ona mifano hai hii juu ya msisitizo wa utoaji kibiblia.
✓✓MUNGU anataka watu wote wawe wanatoa Sadaka.
Kutoka 23:15 "........... wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu;"
✓✓MUNGU anataka twende mbele zake na Sadaka.
Kumbu 16:16 "............ wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu."
✓✓MUNGU anataka wote tuwe watoaji wa matoleo.
Kutoka 34:20 "............... Wala hapana atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu."
✓✓Lakini pia ijapokuwa Biblia inasisitiza juu ya utoaji matoleo ila haina maana kwamba ukiwa huna sadaka usiende Kanisani, bali nakuomba jiwekee ratiba ya kwenda ibadani, ratiba yako hakikisha haiathiriwi na kitu chochote.
✓✓Sadaka ni jambo jema na lenye maana kubwa ila tu isiwe sadaka ya kulazimishana bali ni ile ambayo mtoaji anaitoa kwa moyo wa yeye kwa hiari kupenda kuitoa hiyo sadaka.
Kutoka 25:2 "Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu."
✓✓Ingawa watumishi hawa wa MUNGU waliamriwa na MUNGU kwamba wazipokee sadaka za watu wa MUNGU lakini MUNGU hakutaka wapokee kila sadaka bali wapokee tu sadaka zinazotoka kwenye moyo wa mtu aliyependa kutoa mwenyewe kwa hiari yake.
Hata leo inapaswa kuwa hivyo, Mtumishi asipokee tu kila sadaka bali apokee sadaka inayotokana na hiari ya mtoto na mtoaji huyo awe anamtolea MUNGU kwa moyo wa upendo, hapo ndipo sadaka hiyo ikiambatana na maombi sahihi ya Mtumishi wa MUNGU majibu ya MUNGU yatakuwa dhahiri.
Sadaka ni nini?
◼️Sadaka ni matoleo ya hiari anayotoa mtu ili kumpa MUNGU kupita madhabahu au watumishi.
✓✓Lakini pia ni muhimu kujua kwamba MUNGU hahitaji sadaka kilema baki anahitaji sadaka kamili na ya thamani hata mtoaji mwenyewe.
Kutoka 35:5 "Katwaeni kati yenu matoleo kwa BWANA; mtu awaye yote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba;"
Hapa Biblia inazungumzia uthamani wa hicho unachotaka kumtolea MUNGU.
Je sadaka yako ina thamani ya dhahabu moyoni mwako hata umtolee MUNGU katika KRISTO YESU?
Je sadaka yako ina thamani ya fedha impendezayo MUNGU moyoni mwako hata umtolee MUNGU katika KRISTO YESU?
Je sadaka yako ina thamani ya madini ya shaba moyoni mwako hata umtolee MUNGU katika KRISTO YESU?
Uthamani huu unaweza usimaanishe tu wingi wa sadaka ila uthamani na ubora wa sadaka hiyo, ndio maana wapo waliotoa sadaka nyingi lakini mioyoni mwao hicho kingi kilikuwa ni ziada tu kwako kulingana na hali zao ndio maana mbele za MUNGU sadaka zao hazikuwa bora kama sadaka kidogo sana ya mama mmoja aliyemtolea MUNGU kwa moyo wa upendo na sio kwa kujionyesha kwamba ana pesa.
Luka 21:1-4 " Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo."
✓✓Mahali pengine Biblia inataka utoe sadaka kwa siri, yaani uende madhabahu utoe bila kuwatangazia watu ulichotoa, au uende kwa Mtumishi ukatoe sadaka yako kwa siri.
Mathayo 8:4 "YESU akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao."
Sio ukitoka tu unaanza kumtangazia kila mtu kwamba nimetoka kutoa sadaka kwa Mchungaji kiasi fulani, anayehitaji baraka za MUNGU zilizo ndani ya sadaka lazima awe anafuata kanuni za Kibiblia za utoaji unaoleta matokeo mazuri.
Sadaka ziko za aina nyingi kulingana na anayetoa
Kwa ufupi baadhi ya aina ya sadaka ni hizi;
1) Sadaka ya shukrani.
2 Nyakati 29:31" Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa BWANA, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa BWANA. Basi kusanyiko wakaleta dhabihu na MATOLEO YA SHUKRANI; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa."
Unakuwa Ukimshukuru MUNGU alichokutendea n.k
Walawi 22:29 "Tena mtakapomchinjia BWANA DHABIHU YA SHUKRANI, mtamchinja ili mpate kukubaliwa."
2) Sadaka ya malimbuko.
Kutoka 34:26 "Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya BWANA Mungu wako. ........"
Soma pia Kutoka 22:29-30 .
✓✓Haya ni sehemu ya mazao ya kwanza kuiva shambani, mshahara wa kwanza,na faida ya kwanza ya biashara n.k unamtolea MUNGU kwa hiari na kwa moyo wa upendo.
3) Sadaka ya nadhiri.
Hesabu 30:3 "Tena mtu mke atakapomwekea BWANA nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo,.......;"
Hii ni nadhiri uliyoweka mbele za MUNGU.
Mfano ni huu.
Mwanzo 28:20 "Yakobo akaweka nadhiri akisema, MUNGU akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;"
4) Sadaka ya ahadi ya hiari.
Kumbu 23:23 "Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako."
Ni ahadi uliyoahidi kutoa katika kazi ya MUNGU, katika Kanisa au kwa Mtumishi wa MUNGU n.k
5) Sadaka ya kawaida.
Kumbu 12:14 "bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo."
✓✓Hii ni sadaka unayoitoa ibadani,kwenye semina za Neno la MUNGU au kwenye mikutano ya injili au kwa watumishi, wahitaji n.k
Ina maana kubwa sana sadaka hii ikiiambatanisha na maombi, ndio maana leo tunajifunza maombi ya kuombea matoleo.
6) Sadaka ya changizo.
1 Wakorintho 16:1 "Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo."
Kwa ujumla kuna aina nyingi za sadaka na sio lazima utoe zote bali sikiliza maelekezo ya ROHO MTAKATIFU ndani yako.
✓✓Kuna mpaka sadaka za kupanda mbegu, ni sadaka uliyoipanda kwenye kazi ya MUNGU au madhabahuni ili izae kwenye ulimwengu wa roho na matokeo unayapta wewe katika ulimwengu wa mwili.
✓✓Ni sadaka inahusisha maisha ya baadae ya mtu, yaani unaipanda sasa kwa ajili ya kuja kuvuna matokeo baadae.
2 Wakorintho 9:6 "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."
✓✓Sadaka zote hata kama sijamaliza kuzitaja ni lazima zitolewe kwa hiari na kwa usafi wa moyo na imani huku zikiambatana na maombi katika jina YESU KRISTO .
✓✓Sadaka zote hata kama sijamaliza kuzitaja na zaka na dhabihu ni lazima zitolewe kwa imani huku zikiambatana na usafi wa moyo.
Je unataka kumpendeza MUNGU kupitia sadaka zako?
Biblia inakujibu hivi.
2 Wakorintho 9:7 "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana MUNGU humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."
Lakini pia sadaka zinapaswa kuambatana na maombi sahihi katika jina la YESU kristo
Huu ni ufunuo binafsi ambao mimi Peter Mabula nilifunuliwa katika kuombea sadaka, nilipofunuliwa rohoni mwangu niliwaza sana, je Watumishi wote huombea sadaka hivyo?
Au kila mtumishi amepewa ufunuo binafsi wa kuombea sadaka?
Niliwaza sana ila nikatamani wewe rafiki yangu unayejifunza masomo yangu ulijue jambo hili uwe unaombea sadaka yako au zaka yako au dhabihu yako mwenyewe hata kabla ya kutoa ili mtumishi asipoombea sadaka kama ipasavyo bado maombi yako yatasimama yakiambatana na sadaka yako.
Mtoaji wa sadaka ndiye hasa hujua anatoa sadaka kwa ajili ya nini, akiombea kitu hicho huku akiambatanisha na sadaka yake kama alivyokusudia hakika matokeo huwa mazuri, kama pia mtumishi akiambiwa juu ya sadaka anayotoa mtu na akaambatanisha na maombi juu ya hitaji husika matokea huwa dhahiri.
Najua kuna sadaka za watu wote na hizo Mtumishi huomba ibadani kulingana na na ufunuo wa jumla wa maombi siku hiyo.
Swali, je kama mtumishi hajaomba kulingana na sadaka yako ilivyotaka Inakuaje?
Mfano wewe ibadani umekuja na sadaka ya ahadi au nadhiri na unaiunganisha na sadaka za kawaida za wengine kwenye chombo kimoja cha sadaka, unatamani mtumishi aombe kama sadaka yako ukivyotoa lakini yeye akaomba tofauti maana hajui kama wewe umetoa sadaka nje na sadaka za kawaida.
✓✓Ndio maana Mkristo wakati mwingine inampasa kutoa na sadaka zingine nje na sadaka za watu wote, ila atoe tu kulingana na msukumo wa ROHO MTAKATIFU ndani yake.
Yaani unamfuata Kuhani na kumweleza kwamba unatoa sadaka fulani kwa ajili ya jambo fulani ili mtumishi huyo akuombee kulingana na hitajio la moyo wako kuhusu sadaka yako.
Maombi ya kuombea sadaka.
1. Iombee sadaka yako inene mema
Sadaka huwa inaongea hivyo isemeshe sadaka yako ili iendelee kunena mema juu ya afya,uchumi,kibali kazini, ndoa, uchumba n.k kulingana na hitaji lako unaweza kumwambia Mtumishi pia ili akuombee hivyo kuhusu sadaka yako kulingana na sababu zako njema za kutoa sadaka hiyo.
Sadaka za Dorkasi zilisababisha afufuke, zilionekana, huko ndiko kunena.
Matendo 9:39-41 " Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai."
2. Omba Mungu awakemee maadui zako.
Malaki 3:11 "Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi."
Hivyo kabla ya kutoa au baada ya kutoa omba maombi ya kumwambia MUNGU awakemee maadui zako huku ukiambatanisha Zaka yako au sadaka yako, ni ahadi ya MUNGU kwa mtoaji kwa fungu la kumi na sadaka kwamba MUNGU Atawakemea maadui wa mtu huyo, hivyo omba hivyo na ahadi ya MUNGU kwako mtoaji itafanya kazi.
Mfano; kama maadui zako ni wachawi akiwakemea MUNGU maana yake hatawaruhusu kukudhuru, MUNGU kuwakemea maadui ina maana kubwa sana, unaweza pia kumwambia mtumishi akuombee hivyo juu ya sadaka yako.
3. Omba sadaka yako itengeneze ukumbusho/ikumbukwe mbele za MUNGU
Zaburi 20:3-4 " Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote."
Kuna Sadaka huwa ukumbusho maana yake ikumbukwe na MUNGU na akiikumbuka sadaka yako atayaona na maombi yako yakiwa na hiyo sadaka hivyo atakutimizia mahitaji yako yote.
✓✓Sio sadaka zote zinatengeneza ukumbusho mbele za MUNGU lakini zipo pia sadaka zinazotengeneza ukumbusho mbele za MUNGU.
Matendo 10:1-4 " Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa MUNGU, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba MUNGU daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa MUNGU, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za MUNGU."
Sasa ni juu yako kutoa sadaka itakayo kuwa na hadhi ya kukumbukwa na MUNGU hata utendewe muujiza wako.
4. Iombee sadaka yako ili ihusike katika agano lako na MUNGU kama unaweka agano au ameweka agano.
Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha MUNGU wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu."
✓✓Agano ni patano sasa unaweza ukatoa sadaka ikaumba patano na MUNGU na agano ni kitu kinachodumu.
Hakikisha unatoa sadaka yenye hadhi ya kutengeneza agano na MUNGU na ambatanisha na maombi na agano hilo litachipusha msaada wa ajabu sana wa MUNGU kwako au kwa watoto wako au familia yako au wajukuu wako baada yako. Ibrahimu alifanya agano na MUNGU kwa sadaka yake yenye hadhi kubwa.
Mwanzo 22:16-18 "akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu."
Miaka zaidi ya 500 badae agano kale lilifanya kazi pale uzao wako walipookolewa kwa sababu ya agano lake na MUNGU na hilo agano lilifanyika kwa sadaka iliyotolewa kwa imani.
Kutoka 2:24 "MUNGU akasikia kuugua kwao, MUNGU akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo."
5. Dorkasi alifufuka kwa sababu ya sadaka zake, kuna nguvu ya ufufuo ndani ya sadaka.
Matendo 9:39-40 " Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi."
✓✓Omba nguvu ya ufufuo iliyo ndani ya sadaka ikafufue kwako afya, uchumi, ndoa, uzao, kibali na kila baraka unayoihitaji katika kusudi la MUNGU.
✓✓Wako watu maisha yao yaalibadilika na kuwa bora zaidi baada tu ya kutoa sadaka, mfano hai ni Ibrahimu, Dorkasi na wengine wengi.
Hata mimi nina shuhuda za watu ambao maisha yao yalibadilika baada ya kuwa waaminifu katika kutoa fungu la kumi na sadaka.
Hayo ndio maombi ya kuombea sadaka, zaka, au dhabihu omba wewe unayetoa au ombea na Mtumishi mwaminifu wa KRISTO unayempa sadaka hiyo au unayetoa madhabahuni.
Pia muhimu sana mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments