MTEULE WA KRISTO INAKUPASA KUJITUMA KATIKA KAZI YA MUNGU.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.

✓✓Kama wateule wa MUNGU katika KRISTO YESU inatupasa kujituma katika kazi ya MUNGU.

◼️kujituma katika kazi ya MUNGU kutaifanya kazi ya MUNGU kuonekana na MUNGU wetu atatukuzwa zaidi.

Kwanini ujitume katika kazi ya MUNGU?

✓✓Ni kwa sababu kazi ya MUNGU itaonekana zaidi, MUNGU atatukuzwa na wewe utapata thawabu kutoka kwa MUNGU.

1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."

✓✓Thawabu ni malipo mema anayopewa mtu na MUNGU baada ya mtu huyo kuifanya kazi ya MUNGU.

Kujituma katika kazi ya MUNGU ni kufanyaje?

◼️Kujituma katika kazi ya MUNGU ni kufanya kazi ya MUNGU kwa bidii.

✓✓Kufanya kazi ya MUNGU kwa bidii ni kufanya jitihada katika majukumu ya ki MUNGU na kuhakikisha majukumu hayo yamekamilika kwa haraka na kwa ufanisi.

Wewe kama Mtumishi wa MUNGU hakikisha kazi ya MUNGU inaenda mbele na MUNGU anatukuzwa.

1 Wakorintho 4:1 "Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU."

FAIDA ZA KUJITUMA KATIKA KAZI YA MUNGU.

1. Mafanikio kwenye kazi ya MUNGU yataonekana.

Matendo 6:7 "Neno la MUNGU likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani."

2. Kazi ya MUNGU itakuwa kubwa na matunda yataonekana.

Yohana 15:16 "Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."

3. Watu wengi wanafunguliwa na kuwa huru katika jina la YESU KRISTO.

Marko 16:20 "Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, BWANA akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]"

4. Watu wengi Watafanyika wanafunzi wa YESU KRISTO.

Warumi 15:16 "ili niwe mhudumu wa KRISTO YESU kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya MUNGU kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na ROHO MTAKATIFU."

5. Watu wengi watalijua na kulielewa Neno la MUNGU.

1 Wathesalonike 1:9-10 " Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia MUNGU mkaziacha sanamu, ili kumtumikia MUNGU aliye hai, wa kweli; na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni YESU, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja."

◼️Ndugu hakikisha unajituma katika kazi ya MUNGU.

✓✓Ndugu jitume kwenye kazi ya MUNGU kwa kuihubiri injili ya KRISTO iokoayo.

✓✓Ndugu jitume kwenye kazi ya MUNGU kwa sadaka na zako zako.

✓✓Ndugu jitume kwenye kazi ya MUNGU kwa kufanya kila kitu cha ki MUNGU.

MUNGU akukumbuke na kukubariki ukizingatia kujituma katika kazi ya MUNGU.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments