MTIHANI WA UBATIZO.

Na Mwl Peter Mabula 


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Miezi ya karibuni MUNGU alinipa neema ya kufundisha darasa la ubatizo, namshukuru MUNGU maana wiki tatu zilizopita Wateule 11 wa KRISTO YESU walibatizwa.
Namshukuru MUNGU pia maana wote ambao walifanya mtihani walifaulu vizuri na kubatizwa.
Mtihani ni huu hapo chini, najua wewe umeshabatizwa lakini ukipenda noa ubongo kwa kujipima katika mtihani huu rahisi na MUNGU akubariki sana.
KAWE PENTECOSTAL CHURCH (KPC)
MTIHANI WA UBATIZO MAY 2019

JIBU MASWALI YOTE:
1. Ubatizo ni nini?
….................................................

2. Ni nani aliagiza kwamba waamini wabatizwe?
……………………………………………………

3. MUNGU wetu anaitwa nani jina lake?
……………………………………………………………

4. Kuna aina ngapi za ubatizo? (zitaje)
a) ……………………………………………
b) ……………………………………………

5. Taja sifa tano (5) anazopaswa kuwa nazo mtu anayebatizwa
a) ……………………………………………………………………………………………
b) ……………………………………………………………………………………
c) ……………………………………………………………………………………………
d) ……………………………………………………………………………………………
e) …………………………………………………………………………………………

6. Kipi hutangulia kati ya kumpokea YESU kama mwokozi wako na kubatizwa?
…………………………………………………………………………………………

7. Biblia inasema
a) Yohana 3:5 “YESU akajibu, Amini, Amini,nakwambia , Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa ROHO, Hawezi kuingia ufalme wa MUNGU”
b) Wakolosai 2:12 “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za MUNGU aliyemfufua katika wafu”
c) Warumi 6:3 -4 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika KRISTO YESU tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama KRISTO alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa BABA, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima”
d) Waefeso 4:5 - 6 “Bwana mmoja, imani moja , ubatizo mmoja. MUNGU mmoja, naye ni Baba wa wote,aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.”
e) Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”
f) Matendo 2:38 “Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO , mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU.”
g) Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA na ROHO MTAKATIFU.”
Katika maandiko hapo juu andika maandiko mawili ambayo ni Bwana YESU alizungumza mwenyewe kwa kinywa chake
i. ………………………………………………………………………………………………………………

ii. …………………………………………………………………………………………………


8. Andika NDIYO au HAPANA
a) Ubatizo wa maji ni ishara ya nje ya mtu inayoonesha badiliko la ndani ya mtu …………………………
b) Agano la kale lina vitabu 39 huku agano jipya likiwa na vitabu 28 …………………………

9. Andika kwa ufasaha andiko moja la Biblia unalolifahamu nje na maandiko yaliyotumika kwenye mtihani huu.
………………………………………………………………..........

10. Taja vitabu kumi vinavyopatikana agano jipya
a) …………………………………………
b) ……………………………
c) …………………………………….

d) …………………………………
e) …………………………………
f) ………………………………
g) …………………………………

h) ……………………………………………
i) …………………………………………

J) …………………………………………….

MUNGU akubariki sana
Mtihani huu umeandaliwa na Peter M. Mabula
Mwalimu wa Darasa la Ubatizo

Warumi 13:14 “Basi mvaeni Bwana YESU KRISTO,wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.”

Comments