![]() |
| Peter na Jemimah Mabula Watendakazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu ndugu yangu.
Karibu ujifunze kitu Katika ujumbe huu wa Neno la MUNGU aliye hai.
✓✓Mtu anapookoka huwa mtu huyo habadiliki mwili ila anabadilika matendo yafanywayo na mwili wake.
Kwa hiyo matendo hubadilika Katika mwili ule ule.
2 Wakorintho 5:17 "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya."
Maana yake nini?
✓✓Kama Mtu alikuwa anautumia mwili wake Kwa uzinzi na uasherati akiokoka Mtu huyo anaachana na dhambi hiyo.
✓✓Kama Moyoni mwake alijaza matusi basi akiokoka lugha za matusi zinaondoka nafsini mwake.
✓✓Kama mtu alikuwa msaliti wa ndoa yake basi akiokoka anatulia na mke wake tu au mume wake.
1 Wathesalonike 4:3-5 " Maana haya ndiyo mapenzi ya MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua MUNGU."
✓✓Kama mtu alikuwa anautumia mwili wake katika dhambi, akiokoka Mtu huyo anaanza kuutumia mwili wake katika matendo mema ya mwili.
2 Wakorintho 4:1-2 " Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei; lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU."
Kuokoka ni nini?
◼️Kuokoka ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu ya kuifuata Biblia takatifu.
Warumi 6:6 "mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye(YESU), ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;"
◼️Mtu anapookoka na kuruhusu Neno la MUNGU kuwa kiongozi wake, kitu ambacho Neno la MUNGU huwa linafanya ndani ya mtu huyo ni kuubadilisha utu wa ndani wa mtu huyo na kuufanya mwili kubadilika kutoka matendo mabaya na kuanza tu kufanya matendo mema.
✓✓Ndugu kama kweli umeokolewa na YESU KRISTO basi ishi kama iwapasavyo waliookoka, zingatia maandiko haya hapa chini.
Waefeso 4:22-32 " mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya MUNGU katika haki na utakatifu wa kweli. Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake. Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi. Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji. Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. Wala msimhuzunishe yule ROHO MTAKATIFU wa MUNGU; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na MUNGU katika KRISTO alivyowasamehe ninyi."
✓✓Ndugu, nakuomba kubali kuokoka na kubali kubadilishwa na YESU KRISTO kupitia neno lake kwa wewe kulitii na kuliishi.
Ndugu kubali utu wako wa ndani utakaswe na kuondolewa uchafu wote wa rohoni.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana.

Comments