MUNGU AMEKUWEKEA MUME WAKO/MKE WAKO

Mr&Mrs Mabula 
Watenda kazi katika Shamba la MUNGU 




Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

◼️Kijana uliyejitunza na unaishi maisha matakatifu je unajua kwamba MUNGU amekuwekea Mke wako ili kwa majira yake ufunge ndoa na huyo mwanamke?

✓✓Hakika MUNGU amekuhifadhia mke wako na kaa kwenye kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU na majira yakifika MUNGU atamfunua kwako huyo binti mzuri na mtafunga ndoa takatifu.

◼️Binti uliyejitunza na unaishi maisha matakatifu je unajua kwamba MUNGU amekuwekea Mume wako ili kwa majira yake mfunge ndoa?

✓✓Hakika MUNGU amekuhifadhia mume wako na kaa kwenye kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU na majira yakifika MUNGU atamfunua kwako huyo mwanaume  na mtafunga ndoa takatifu.

Vijana wengi na mabinti wengi huwa wanakuwa na wasiwasi kama kweli watapata wenzi safi na kufunga nao ndoa.
MUNGU amekuwekea mke wako au mume wako hakika.
Ukisoma Mwanzo 24:44 Biblia inaonyesha Isaka aliwekewa Binti mzuri aitwaye Rebeka kwa ajili ya Ndoa. Biblia hapo inasema "naye akaniambia, Unywe wewe, na ngamia zako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke BWANA aliyemwekea mwana wa bwana wangu."

✓✓Isaka alikuwa Kijana anayemcha MUNGU na amejitunza ndio maana wakati wake wa kuona ulipofika MUNGU alimfunua kwake Mke mwema mzuri sana na kiwango sana aitwaye Rebeka.

✓✓Hali ilikuwa hivyo hivyo kwa Rebeka ambaye alikuwa ni binti akiyejitunza, ana akili na anajiheshimu , wakati wake ulipofika wa kufunga ndoa MUNGU akamletea Mwanaume safi aitwaye Isaka.

◼️Hawa walikuwa hawajawahi kuonana kabla lakini kujitunza kwao na kukaa kwako katika kusudi la MUNGU kuliwaleta pamoja Katika Ndoa takatifu, na aliyewaleta pamoja hata wanafunga ndoa ni MUNGU, andiko hapo juu linaonyesha kutumia aina ya ufunuo wa kumpata Rebeka ili akaolewe na Isaka.

Inawezekana wewe unasubiri tu uote ndoto ndipo ujue ni nani atakuwa mume wako au mke wako, ndugu kama hujitunzi hakika atakayekuotesha ndoto wakati huo inawezekana akawa ni shetani na sio MUNGU.

Kusudi la MUNGU liko katika wanaomcha tu na hao ndio watafunuliwa mambo mbalimbali na MUNGU.
Zaburi 25:14 "Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake."

Hakika MUNGU amekuhifadhia mwenzi wako, kaa tu kwenye kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU na majira yakifika MUNGU atamfunua kwako huyo mwenzi na mtafunga ndoa takatifu.

Inawezekana wewe umeokoka na umepata Mchumba lakini wenye YESU ndani yao wote wana mashaka na mchumba huyo, ndugu, kama ni kusudi la MUNGU hata wazazi wako au ndugu zako wenye YESU ndani yao au watumishi wa MUNGU wanaweza kuthibitisha kwamba Mchumba wako huyo ni kusudi la MUNGU, watathibitisha jambo hilo limetoka kwa MUNGU hivyo mtafunga ndoa takatifu kwa amani na furaha.

Ona mfano hai ilivyokuwa kwa Rebeka baada ya wazazi na ndugu zake kuwa na amani maana jambo hilo limetoka kwa MUNGU. Biblia inasema hivi katika 
Mwanzo 24:50-51 " Ndipo Labani na Bethueli wakajibu wakasema, Neno hili limetoka kwa BWANA, wala sisi hatuwezi kukuambia neno jema wala baya. Tazama, huyo Rebeka yuko mbele yako, umchukue, ukaende zako awe mke wa mwana wa bwana wako, kama alivyosema BWANA."

Ndugu usiwafanye wazazi wako au ndugu zako wenye YESU ndani yao au watumishi wa MUNGU, usiwafanye kuona hatari mbele yako kwa sababu ya mchumba uliyemjulisha kwao kwa sababu tu hakuna kusudi la MUNGU wewe ufunge ndoa na huyo.

Mfano hai ni huu.
Rebeka na Isaka wakiwa wazee walisikitika sana kuona Esau mtoto wao anamuoa Yudithi Mhiti.

Mwanzo 26:34-35 " Esau alipokuwa mwenye miaka arobaini, akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti. Roho zao Isaka na Rebeka zikajaa uchungu kwa ajili yao."

Sio kwamba akina Judithi hawafai kuwa wake wema, wanafaa sana sana lakini Judithi Mhiti alikuwa hafai hata kidogo kwa sababu ni mwabudu shetani anayetokea ukoo wa wahiti ambao ni waabudu shetani, ndio maana watu wenye ROHO MTAKATIFU ndani yao walisikitika sana juu ya ndoa hiyo maana haikuwa kusudi la MUNGU.

Ndugu kwa mfano huu ndani ya Biblia tunagundua kwamba haiwezekani wewe Mkristo yaani umeokoka harafu eti MUNGU akupe mume au mke mpinga KRISTO, haiwezekani kamwe.

Ndugu yangu, Mimi Peter Mabula Niko hapa leo kukuambia kwamba ishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU na MUNGU atakuletea mke mwema wako au mume mwema wako.
Kumbuka hilo na usije ukasahau kwamba mume mwema au mke mwema hutoka tu kwa MUNGU.

Hakika MUNGU amekuhifadhia mwenzi wako, kaa tu kwenye kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU na majira yakifika MUNGU atamfunua kwako huyo mwenzi na mtafunga ndoa takatifu.

✓✓✓Hivyo endelea na maombi, endelea kumtumikia Bwana YESU na majira ya MUNGU hayatauvuka umri wako hivyo utafunga ndoa mapema sana.

Wewe kijana wa kiume kumbuka tu kujiandaa kutoa mahari ili usije ukalizuia kusudi la MUNGU, jiandae, andaa mahari.
Ona mfano hai wa mahari ya Isaka ya kumuoa Rebeka kulingana na utaratibu wao kwa jamii hizo.
Jiandae kama familia ya Isaka walivyojiandaa.
Mwanzo 24:53 "Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia."
Andaa mahari na fanya kazi njema kwa ajili ya maisha yako.
Najua mahari hata wazazi wanahusika hivyo wakumbushe wazazi wako ili waandae mahari hiyo mapema.
Hakika MUNGU amekuhifadhia mwenzi wako, kaa tu kwenye kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU na majira yakifika MUNGU atamfunua kwako huyo mwenzi na mtafunga ndoa takatifu.
Kwenye kusudi la MUNGU ukimhusisha MUNGU hakika utafanikiwa.

Inawezekana wewe ni yatima au wazazi hawana uwezo, basi jiandae mapema wewe mwenyewe na huku ukimuomba MUNGU na utafanikiwa.

Jitahidi ndugu, sio muda wa kupata mwenzi umefika harafu wewe huna mahari hata mia, ndugu jiandae na MUNGU atakuwezesha.

Hakika MUNGU amekuhifadhia mwenzi wako, kaa tu kwenye kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU na majira yakifika MUNGU atamfunua kwako huyo mwenzi na mtafunga ndoa takatifu.

Na kwa wewe ambaye ulishafunga ndoa tayari basi kazi Yako ni kuwabariki wanaofunga ndoa takatifu sasa.
Kuwabariki wanaofunga ndoa takatifu ni jambo jema.
Ona mfano hai.
Mwanzo 24:60 "Wakambarikia Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao."

Baraka za wazazi na ndugu zake Rebeka, hizo baraka ziliambatana na Rebeka katika ndoa, ndugu wewe mbariki anayefunga ndoa, Sisi watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU kazi yetu ni kuwabariki wanaofunga ndoa.
Hata mimi Peter Mabula hapa muda huu nakubariki wewe unayetarajia kuingia katika ndoa, MUNGU Baba akukumbuke na kukulinda, akupe baraka na ushindi katika ndoa unayetarajia kuingia, akupe maisha marefu, akupe uzao bora na ailinde familia yako usiku na mchana.
Baraka baraka hizi ziambatane na wewe katika ndoa yako " MUNGU na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, ...... Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe." sawasawa na Mwanzo 27:28a na 29

Hakika MUNGU amekuhifadhia mwenzi wako, kaa tu kwenye kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU na majira yakifika MUNGU atamfunua kwako huyo mwenzi na mtafunga ndoa takatifu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292( whatsapp, ushauri na Sadaka ya kuipeleka mbele Injili).
Ubarikiwe sana

Comments