![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
MUNGU Hana Usahaulifu ndio ujumbe wa leo.
Yaani MUNGU wa Mbinguni huwa hasahau.
Neno Usahaulifu Linatokana Na Neno Kusahau.
Kusahau Ni Kitendo Cha Mtu Kuacha Kufanya Jambo Fulani Ambalo Lilikuwa Limepangwa Au Umepanga Mwenyewe.
◼️Wewe Mteule Wa Bwana YESU Ni Muhimu Kujua Jambo Hili Kwamba MUNGU Hana Usahaulifu.
Katika Biblia MUNGU Mwenyewe Anasema Neno Hili.
Isaya 49:14-16 " Bali Sayuni Alisema, YEHOVA Ameniacha, BWANA Amenisahau. Je Mwanamke Aweza Kumsahau Mtoto Wake Anyonyaye, Hata Asimhurumie Mwana Wa Tumbo Lake? Naam, Hawa Waweza Kusahau, Lakini Mimi Sitakusahau Wewe. Tazama, Nimekuchora Katika Vitanga Vya Mikono Yangu; Kuta Zako Zi Mbele Daima.".
Hii inakufundisha nini?
MUNGU hana usahaulifu.
Ndugu Yangu Ahadi Ya MUNGU Maishani Mwako Ni Kweli Na Ndiyo.
✓✓Usikate Tamaa Binti Unayeona Umri Unakwenda Na Hakuna Kijana Wa Kukuoa, Ongeza Maombi Na Acha Manung'uniko Na Kujilinganisha Na Wengine.
✓✓Usiseme MUNGU Amekusahau Kijana Kwa Maana Umeomba Muda Mrefu Ili Upate Kazi, Songa Mbele Na YESU Na MUNGU Baba Anaandaa Jambo Jema Mbele Yako, Ongeza Maombi Na Usitegemee Wanadamu.
◼️Watu wengi sana hupishana na baraka zao maana wanaomba na MUNGU anawaambia kwamba atawapa kile walichoomba lakini baada ya muda kidogo imani yao inapungua na kurudi nyuma na kipindi wakirudi nyuma na majibu ya MUNGU yanakuwa yanakuja lakini MUNGU anaghairi baada ya kuwakuta wamerudi nyuma.
Ndugu ni muhimu sana kutambua kwamba MUNGU hana usahaulifu, endelea kuomba na muujiza wako utakuja tu.
Zaburi 62:8. "Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; MUNGU ndiye kimbilio letu."
Wanaomtumaini MUNGU hawakati tamaa.
◼️Wanaomtumaini MUNGU wanaenenda katika ROHO MTAKATIFU siku zote.
◼️Wanaomtumaini MUNGU kwao Jina la YESU KRISTO ndio msaada mkuu.
◼️Wanoamwamini MUNGU wana uhakika na MUNGU wao wala hawawezi kumdhania kwamba MUNGU kasahau ahadi zake kwao.
Biblia hapo juu imesema kwamba ''Ifunueni mioyo yenu'' yaani semeni mnahitaji nini kwa MUNGU katika KRISTO YESU, Kwa lugha nyingine unaweza kusema kwamba ''Ombeni kwa MUNGU''
Bwana YESU KRISTO anasema katika
Yohana 15:7 kwamba "Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa."
Hakikisha neno la MUNGU linakaa kwa wingi moyoni mwako.
Waebrania 4:16 "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji."
Ndugu uliyempokea Bwana YESU tambua kwamba maombi ni haki yako, yaani MUNGU atakusikia na kukujibu hata bila kupitia kuombewa na wengine.
Je MUNGU yuko tayari kusikia maombi yetu na kutujibu.
Mathayo 7:11 "Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema je! si zaidi BABA yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?".
✓✓MUNGU hajakusahau ndugu yangu.
Anakuandalia jambo jema.
Endelea tu kusubiri kwa maombi.
na tambua jambo hili kwamba ''ILI MUNGU AWE MUNGU NI LAZIMA YEYE NDIYO AAMUE NA SIO SISI WANADAMU TUMUAMLIE''
Anatujua vyema ndio maana hutuandalia mema katika muda sahihi.
Ndugu usiache kuomba na wala imani yako isipungue na kudhani kwamba MUNGU amekusahau.
MUNGU hana usahaulifu hata kidogo.
''MUNGU si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?-Hesabu 23:19''
MUNGU sio Mwanadamu hata aseme uongo
MUNGU anajibu maombi, ndugu omba siku zote.
Je umeomba nini kwa MUNGU katika KRISTO YESU, ndugu Endelea kusubiri na kuomba maana MUNGU atakuonekania tu.
Kama unaumwa na unahitaji YESU KRISTO akuponye, ndugu endelea kuomba na kumngoja MUNGU.
Zaburi 27:14 "Umngoje BWANA, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA."
Ndugu, Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na hadi whatsapp).
Ubarikiwe

Comments