MVINYO NA KILEO JITENGE NAVYO MBALI.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Lengo la somo hili ni mtu ambaye hunywa Mvinyo na Kileo aache.

Mvinyo ni nini?

✓✓Mvinyo ni kinywaji chenye kileo.

Kileo ni niNi?

✓✓Kileo ni kinywaji Ambacho hulevya.

◼️Kwa ujumla Mvinyo na Kileo vinabebwa na jina moja liitwalo Pombe.

Hivyo pombe ndio Mvinyo na ndio Kileo.

✓✓Mtu anayetumia Mvinyo na vileo anaitwa Mlevi na ukiangalia kamusi maana ya Neno "Mlevi " ni mtu anayetumia vitu vinavyolevya ambavyo ni pombe na madawa ya kulevya, ni mtu mwenye tabia ya kulewa.

◼️Katika Biblia baadhi ya maandiko ambayo ni mengi yalipozungumzia Mvinyo na Kileo yalianza na Neno "Ole"

✓✓Habakuki 2:15 "Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!"

✓✓Isaya 5:22 "Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo;"

✓✓Isaya 5:11 "Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!"

◼️Kwanini "Ole"?
Unamjua maana ya neno "Ole"

✓✓Neno "Ole" ukiangalia kamusi ya kiswahili sanifu lina maana ya tamko la kuelezea majuto, mapigo na masikitiko.

◼️Sasa ni Ole wake anayempa mwenzake pombe, Hiyo ni Habakuki 2:15.

◼️Ole wake mtu aliye hodari katika kunywa pombe, hiyo Isaya 5:22

◼️Ole wake mtu anayekunywa pombe, huponi Isaya 5:11

✓✓Maana yake kwa anayeuza pombe na anayekunywa pombe mbele yao hao kuna majuto, mapigo na masikitiko.

 Majuto, mapigo na masikitiko yatawapata watakakwenda jehanamu, ndio Maana ndugu yangu nakusihi acha pombe kisha okoka upya ili YESU KRISTO awe Bwana na Mwokozi wako.

◼️Kama kuna mtu alikufundisha kunywa pombe basi ni hakika mtu huyo alikiwa wakala wa shetani ili usiende uzima wa milele.

◼️Kama kuna mtumishi anakuhubiria unywe pombe hakika huyo ni mpambe wa shetani ili wewe usiende uzima wa milele.

◼️Ndugu jitenge mbali na mtumishi Mlevi maana mtumishi Mlevi ndiye hufundisha Watu kulewa, ndiye nabii wa walevi.
Mika 2:11 "Mtu akienda kwa roho ya uongo, akinena maneno ya uongo, akisema, Nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa."

◼️Kama kuna mtu anakuambia kunywa kidogo ila usilewe huyo ni mtumishi wa shetani ili usiingie uzima wa milele.

Kwanza siamini kama yuko mtumishi anaweza kuwahubiria Watu kwamba waendelee tu kunywa pombe.

Ndugu yangu, kama wewe kweli ni Mkristo na YESU KRISTO ni Mwokozi wako basi Usimkubali kunywa Mvinyo wala kileo.

◼️Bwana YESU pale Golgotha walijaribu kumpa Mvinyo akakataa.
Marko 15:23 "Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane, asiipokee."

Bwana YESU KRISTO aliikataa pombe, vipi Wewe mlevi wa lengo ungepewa pombe katika mazingira hayo si ungesema "ongeza ili nipunguze maumivu"
Vipi Wewe unayeshinda Bar ungepewa pombe katika mazingira kama hayo, nadhani ungesema "niongee pombe maana ponda raha kifo chaja"
Lakini Bwana YESU aliikataa pombe, hata Wewe kuanzia Leo jifunze kukataa pombe.

Inakuwaje wewe unayejiita Mkristo unapewa pombe unakunywa na kuomba nyongeza?
Wewe unamfuata KRISTO yupi?
Maana KRISTO alikataa pombe.

◼️Biblia iko wazi sana ikitukataza kunywa pombe.
Waefeso 5:18 "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe ROHO;"

Ndugu, pombe inaweza kumletea mtu Baadhi ya matatizo haya.

1. Pombe huleta umasikini.

Mithali 21:17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
Wako Watu wameuza hadi nyumba na viwanja Kwa sababu ya pombe.
Watu wengi wamefukuzwa kazi Kwa sababu ya pombe, ukifukuzwa kazi umasikini lazima uingie, ndugu jitenge mbali na pombe maana pombe ni chanzo kimojawapo kikuu cha umasikini.

2. Pombe ni chanzo kimojawapo kikuu cha uzinzi na uasherati.

Hosea 4:18 "Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu."

✓✓Kuna Watu walipata magonjwa ya zinaa Kwa sababu ya pombe iliyozaa uzinzi na uasherati.

✓✓Kuna Watu maisha yako yalikosa mwelekeo mzuri kwa sababu ya pombe iliyozaa uzinzi na uasherati.

3. Pombe huleta dhihaka na ugomvi.

Mithali 20:1 "Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima."

✓✓Kuna Watu walifanyika vilema Kwa sababu ya kulewa kulikozaa kupigana, wakapigwa na kuumizwa.

✓✓Kuna Watu waliua watoto wao, wenzi wao au ndugu zao Kwa sababu walikuwa wamelewa, ni hatari sana.

Ndugu, ujumbe wa leo ni muhimu sana ufanyie kazi wewe unayehusika.
MUNGU akubariki kama ukifanyia kazi.
Nakuombea pia Neema ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe.

Comments