NA WAIBIKE WANAOABUDU SANAMU WOTE.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

✓✓Na waibike wanaoabudu sanamu wote hili ndilo somo letu la leo.
Kama Kuna mwabudu sanamu atajisikia vibaya akidhani nimemhukumu kwa kumwambia alaaniwe naomba kumjulisha kwamba laana hiyo sijaitoa Mimi Bali Neno la MUNGU mwenyewe ndilo linamlaani kila mwabudu sanamu.

Zaburi 97:7 "Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa;......"

Kwanini waabike wanaoabudu sanamu?

1. Ni kwa sababu kuabudu sanamu ni kumwabudu shetani.

Kutoka 20:4-5 "Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni MUNGU mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,"

✓✓Ndani ya sanamu yeyote inayoabudiwa kuna mashetani/maroho ya kuzimu yaani wakuu wa giza kutoka kuzimu.
Hivyo kuabudu sanamu yeyote ni kumwabudu shetani.

2. Ni kwa sababu sanamu ni kazi ya mikono ya wanadamu.

Yeremia 1:16 "Nami nitatamka hukumu zangu juu yao kwa habari ya uovu wao wote; kwa kuwa wameniacha mimi, wakaifukizia uvumba miungu mingine, wakaziabudu kazi za mikono yao wenyewe."

✓✓Haiwezekani Mwanadamu mwenye akili timamu aliyeumbwa na MUNGU Kisha akaabudu sanamu, kama Yuko anayeabudu sanamu basi alaaniwe sawasawa na Neno la MUNGU.

3. Sanamu hazina ufahamu, sanamu sio kiumbe hai.

Zaburi 135:15-17 " Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, Zina masikio lakini hazisikii, Wala hamna pumzi vinywani mwake."

Inawezekana unaabudu mawe, sanamu, wanyama n.k huku ukijua kabisa hicho unachokiabudu hata Wewe unakizidi akili? Na sanamu haziwezi hata kusikia 

4. Sanamu ni chukizo kwa MUNGU.

1 Wakorintho 6:9 "Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala WAABUDU SANAMU, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,"

✓✓Ndugu ngoja nikupe Siri hii.
Nje na Wokovu wa KRISTO YESU Kuna sanamu, Wewe kama hujaokolewa na Bwana YESU KRISTO ni ukweli mmoja Wewe uko upande wa kuabudu sanamu, ni mbaya sana.

5. Sanamu hazina msaada hata mmoja kwa mwanadamu.

Zaburi 115:4 -8 "Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu, Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake. Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia."

Ni kujitoa ufahamu tu Kufuata kitu ambacho hakiwezi hata tu kupumua harafu ukakiabidu

6. Wanaoabudu sanamu hawataenda uzima wa milele.

Waefeso 5:5 "Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa KRISTO na MUNGU."

Kwanini ushughulike na kitu ambacho hakitakufikisha uzima wa milele?
✓✓Ni ujinga wa mwisho kabisa kuabudu sanamu.

7. Hakuna ushirika kati ya sanamu na YESU KRISTO.

2 Wakorintho 6:16-17 " Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai; kama MUNGU alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha."

◼️Ndugu, ambatana na YESU KRISTO achana na sanamu.

8. Wanaotumainia sanamu hufanana nazo.

Zaburi 135:18 "Wazifanyao watafanana nazo, Na kila mmoja anayezitumainia"

✓✓Kwa sababu hizo 8 Mimi naungana na Biblia kusema waabike kuanzia leo waabudu sanamu wote.

✓✓Uabike kuanzia leo wewe mwanaume unayeabudu sanamu.

[[Uaibike kuanzia leo wewe mwanamke unayeabudu sanamu.

Hata kuabudu Mungu mwingine nje na MUNGU katika KRISTO YESU ujue wewe ni mwabudu sanamu/shetani.

Kutengeneza sanamu ili uiabudu au kununua sanamu au kupewa sanamu na watumishi wa shetani ili utumie sanamu hizo kuabudu ni machukizo makuu kwa YAHWEH MUNGU wa pekee na wa kweli aliyejifunua kupitia Wokovu wa KRISTO YESU.

Waabike waabudu sanamu wote kokote waliko.

✓✓Kama ni wewe ndiye mwabudu sanamu nakuomba utupe sanamu hiyo, ichome moto na jitenge mbali na kusanyiko la waabudu sanamu.

✓✓Kama unautaka uzima wa milele ujue unamhitaji YESU KRISTO Mwokozi na sio kuhitaji sanamu.

Narudia tena waabike waabudu sanamu wote.

Isaya 42:17" Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu."

Tengeneza na MUNGU katika KRISTO YESU na utaitwa heri.

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments