![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu kujifunza Neno la MUNGU, nakuomba soma hadi mwisho.
✓✓Neno la MUNGU ni la thamani sana katika maisha yako kama mteule wa KRISTO YESU.
✓✓Litumie tu Neno la MUNGU katika ROHO MTAKATIFU ili ushinde, ufanikiwe, ufaulu na ubarikiwe.
Mithali 2:1-8 "Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua MUNGU. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake."
✓✓Tumia vizuri Neno la MUNGU katika maisha yako.
✓✓Tumia vizuri Neno la MUNGU katika maarifa mema aliyoweka MUNGU ndani yako.
✓✓Neno la MUNGU limebeba maarifa mengi sana ya kukusaidia katika mambo mengi sana.
✓✓Neno la MUNGU ni mfano wake ni kama kitu kimoja chenye kazi nyingi njema.
✓✓Neno la MUNGU mfano wake naweza kusema ni kama unga safi wa ngano ambapo kwa kutumia unga huo wa ngano mtu mmoja atatengeneza chapati, mwingine atatengeneza andazi, mwingine atatengeneza keki, mwingine atatengeneza donati n.k lakini vitu hivyo vyote vimetengenezwa na kitu kimoja kiitwacho unga wa ngano.
Kwanini nasema hivyo?
✓✓Ni kwa sababu Neno la MUNGU linaweza kukupa maarifa fulani unayoyahitaji ili ushinde au ufanikiwe.
✓✓Neno la MUNGU linaweza kukufanya unaonekana una elimu na akili kuliko hata baadhi ya wasomi wasiomjua MUNGU.
Zaburi 119:100 "Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako."
✓✓Neno la MUNGU linaweza kutengeneza elimu ndani yako itakayokusaidia kumshinda shetani na mawakala zake.
✓✓Neno la MUNGU linaweza kukupa akili ya kufanikiwa kwako.
Zaburi 119:66 "Unifundishe akili na maarifa, Maana nimeyaamini maagizo yako."
✓✓Neno la MUNGU linaweza kukupa ufahamu unaokufanya uwe mshindi siku, zote.
Mithali 2:6 "Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;"
✓✓Neno la MUNGU linaweza kukufinyanga na ukawa mshindi dhidi ya dhambi kama tu ukilitii na kulifuata.
Mithali 1:7 "Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu."
Changamoto kwa watu wengi ni kwamba hawajui kulitumia Neno la MUNGU katika hali zao wanazopitia ndio maana wanakosa maarifa ya maombi au maarifa ya kufanya ili wafanikiwe kulingana na hali zao.
Zaburi 49:20 "Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama wapoteao."
Ngoja nikupe mifano miwili
Mfano wa kwanza.
Binti amefikia umri wa kuolewa na anatamani sana apate mchumba kisha wafunge ndoa takatifu Kanisani, binti huyu ni muombaji na maombi yake ni kwamba "nipate mume mwema" ni sawa kabisa kuomba hivyo lakini akisoma Neno la MUNGU katika hatua aliyopo ili apate mume mwema anaweza kupata maarifa mengi ya kiakili na kimaombi hata akafanikiwa kirahisi.
Mfano kama binti atajifunza nini kilisababisha Esta akafunga ndoa na Mfalme Ahusuero ataona kwamba ili aolewe alihitaji mambo mengi, baadhi ni haya
1. Esta hakutakiwa kudhihirisha familia yake na kabila lake.
Esta 2:10 "Walakini Esta hakudhihirisha kabila yake wala jamaa yake, kwa maana ndivyo alivyomwagiza Mordekai asiwadhihirishe."
Sasa binti wa leo anaweza kuwa ni muombaji sana lakini akiwa karibu tu na vijana waoaji atasema "Familia yetu masikini sana, tukioana itabidi umvumilie mama yangu maana ni mchawi, tukioana itabidi uchukuliane na familia yangu maana ni wakorofi, wana magonjwa ya kurithi, wabishi, wanafiki, wanakula sana, wezi n.k"
Sasa ukijifunza Neno la MUNGU mfano hapo kwa habari za Esta alivyoolewa unapata ufahamu kwamba sio unaanika kila kitu cha familia yako au ukoo wako wakati hata mchumba hujapata, usije ukamfanya mchumba wako akakuunganisha kwenye kundi la ndugu zako wote hata kama huhusiki hivyo akaghairi mapema tu suala la kukuoa, wapo mabinti huachwa kabla hata hawajatamkiwa.
Yaani kijana moyoni mwake alikuchagua kabisa na akapanga hadi tarehe ya kukueleza lakini akisikia tu habari zako na familia yako anakukataa hata dakika chache kabla hajakuambia, sifundishi leo masuala ya ndoa na uchumba ila nataka uwe unajifunza Neno la MUNGU ili upate maarifa ya kukupa akili njema ya kukusaidia.
2. Ili Esta aolewe na Ahusuero ilitakiwa Esta apate neema na kibali machoni pa Ahusuero.
Esta 2:17 "Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti."
◼️Jambo la kujua ni kwamba binti hata kama ni mzuri kiasi gani hawezi kuolewa na mwanamume yeyote kama binti huyo hatapata neema na kibali machoni mwa mwanaume husika, na hata kwa mwanaume ni hivyo hivyo.
Ninachotaka kukuambia ni kwamba kwa kujifunza Neno la MUNGU unaweza kugundua hivyo na katika listi ya maombi yako basi ukaweka na kipengele cha kuomba kwamba upate Neema na kibali machoni pa yule aliyekuchagulia MUNGU.
Hata kwa walio katika ndoa, ni muhimu kujua kwamba nguvu za giza na mawakala wa shetani wanaweza kuiroga ndoa yako kwa kuua kiroho neema na kibali mbele za mwenzi wako ndio maana kila siku ndoa yako ina vita na majanga, kikiondoka kibali na neema machoni pa mke wako au mume wako kuhusu wewe ujue atakuwa anakuona wewe kama takataka au kifurushi na sio kukuona wewe kama mke mwema au mume mwema wake, hivyo kwenye maombi yako baada ya kujifunza Neno la MUNGU la maarifa utajua ujiombee neema na kibali machoni mwa mwenzi wako.
Ukikirudisha kibali na neema machoni pake kuhusu wewe ujue atakuheshimu, atakuona wewe ni bora, atakuona wewe ni mpya kila leo hata kama mko kwenye ndoa miaka 20 au zaidi, atakuona wa thamani sana, atakupenda, atakuhudumia kwa upendo n.k
Ndugu unaona namna Neno la MUNGU linavyoweza kuwa msaada kwako na zaidi ya msaada?
Zaburi 119:169-170 " Ee Bwana, kilio changu na kikukaribie, Unifahamishe sawasawa na neno lako. Dua yangu na ifike mbele zako, Uniponye sawasawa na ahadi yako."
Ndio maana unafurahi YESU KRISTO Mwokozi anaposema hivi kuhusu Neno lake ambalo pia ndilo Neno la MUNGU.
Mithali 8:14 "Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu."
Mfano wa pili.
Ili uongezeke kiuchumi, upate baraka kubwa na kibali, utengeneze agano na MUNGU, upate ulinzi juu ya uchumi wako n.k inakupasa kuwa mtoaji zaka na sadaka.
Mithali 3:9-10 " Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."
Sasa watu wengi ni watoaji lakini wakati mwingine hawaipokei baraka ya MUNGU kwa sababu hawafuati Kanuni zilizo ndani ya Neno la MUNGU.
Ngoja nikupe mifano michache.
Kuna mtu ni mtoaji lakini hadi alazimishwe kutoa, kuna wengine hadi wadanganywe na watumishi feki ndipo wanatoa.
Je Neno la MUNGU linataka utoe zaka au sadaka kwa kulazimishwa?
Si kweli hivyo anayetoa kwa kulazimishwa hapokei kutoka kwa MUNGU.
2 Wakorintho 9:7" Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana MUNGU humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."
Kuna mtu hutoa sadaka au zaka kwa moyo usio wa upendo , je huyo atapokea kwa MUNGU, jibu ni hapana maana MUNGU anataka watu wake wamekuwa upendo.
Kutoka 25:2-3 "Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, na fedha, na shaba,"
✓✓Wakati mwingine kutoa vizuri ni kuonyesha kiwango chako cha kumpenda MUNGU na kujali kazi yake ya injili ya KRISTO.
✓✓Sasa unaweza kujifunza Neno la MUNGU la kukusaidia ili utoe na kupata baraka zote za kiroho zilizo ndani ya utoaji.
Yuko mtu hawezi kumtolea MUNGU zaka na sadaka na mtu huyo ni muombaji sana lakini hapokei, kukosa maarifa ya Neno la MUNGU ni hatari sana.
2 Wakorintho 9:6 "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."
Kuna mtu mmoja siku moja nilikuwa namuombea ghafla nikasikia sauti inasema nimwambie atoe sadaka, nilisita kumwambia maana niliogopa asije akadhani nataka pesa zake maana kuna watu kwenye utoaji huwaangalia watumishi na sio MUNGU.
Wakati mtu mwenyewe binafsi anaweza kufunuliwa rohoni mwake mwenyewe na ana uwezo huo mfano kwamba atoe milioni kumi ili kazi ya injili isonge mbele, mtu huyo kwa kumwangalia mtumishi na sio kumwangalia MUNGU anajisemea "Huyu Mchungaji au Mtumishi nikimpa Milioni 10 atafaidi sana ngoja nimpe laki moja maana sadaka ni sadaka tu"
Mtu wa namna hiyo hawezi kupokea kutoka kwa MUNGU hata kama ametoa mara 7 maana yeye anamwangalia Mtumishi na sio kumwangalia MUNGU.
Wakati mwingine hata mtumishi akipewa hiyo sadaka hatafaidika nayo binafsi maana MUNGU atamwambia afanyie kitu fulani ili kukuza huduma au kuipeleka mbele.
Mtumishi mmoja wa MUNGU siku moja alibarikiwa pesa nyingi akanunua spika za kuhubiria hadi Familia yake wakamshangaa maana hakuwa na pesa, Mtumishi mwingine akubarikiwa Millioni moja akainua viti vya kanisani vyote, hata familia wakati mwingine inaweza usimuelewe Mtumishi wa MUNGU ambaye anasikiliza maelekezo ya MUNGU.
Sasa kuna mtu kwa sababu ya kukosa maarifa ya Neno la MUNGU anaweza kujikuta anatoa bila kupata baraka za utoaji wake, ndugu jifunze sana Neno la MUNGU ili upate maarifa sahihi ya kiroho ukiongozwa na ROHO MTAKATIFU ndipo utafanikiwa na kustawi sana kiroho na kimwili.
Mithali 1:23 "Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu."
✓✓Kuna watu wana akili ila hawana maarifa ya Neno la MUNGU ndio maana akili zao haziwasaidii .
◼️Neno la MUNGU linaweza kukupa ufahamu sahihi, hekima njema, maarifa sahihi na akili nzuri kwa pamoja.
✓✓✓Ndugu unalihitaji sana Neno la MUNGU la maarifa ya ROHO MTAKATIFU.
✓✓Ilimradi ni maarifa sahihi ya ki MUNGU basi maarifa hayo ya Neno la KRISTO yatumie ili ufanikiwe.
Mfano kuna watu wana vipawa ila vipawa vyao haziwasaidii, wanachopungukiwa sio kipawa bali wanapungukiwa Neno la MUNGU la maarifa ya ROHO MTAKATIFU.
◼️Ndugu, maarifa ya ki MUNGU yanayopatikana ndani ya KRISTO YESU ni ya thamani sana.
Fanyia kazi na utaitwa heri.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments