SHUHUDA 14 MBALIMBALI.


SHUHUDA 14 MBALIMBALI.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Hapa chini ni shuhuda mbalimbali ambazo baadhi ya rafiki zangu walinitumia.
Shuhuda hizi baadhi zinatokana na masomo ambayo ROHO MTAKATIFU amenipa neema kuyaandika, na shuhuda nyingine zinatokana na maombi.
Utukufu wote kama ulivyo ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni.
1. Mtumishi Bwana Yesu asifiwe, Mungu ni mwema sana maana mtoto wangu ambaye kila siku usiku wa manane lazima alie sana sana, wakati akianza kulia ni hadi asubuhi. Tangu siku umemuombea hajalia tena usiku hata kidogo.
Mungu akubariki sana.
2. MTumishi nakushkuru sana kwa msaada wako wa kuniombe, MUNGU na azidi kukutumia, jamani kwa sasa mimi ni mzima afya na nimeruhusiwa kutoka hospital nimerudi nyumbani.
AMINA
3. Haleluya mchungaji, hakika Mungu amenitendea makuu nilivyokupigia juu ya kuniombea nilikua nimeshika kipimo cha mimba na nilivyokata simu kwa imani nikasema leo lazima nipime nimekuta niko na ujauzito hakika Mungu atukuzwe sana.
Siku nyingi siingii katika siku zangu na tukipima mimba hakuna, nilikuwa na wakati mgumu sana lakini baada ya kuniombea nimepima na nina mimba.
Mungu akubariki sana mchungaji.
4. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Ndugu yangu amejifungua mtoto wa wa kike, hali ya mama na mtoto ni nzuri kabisa.
ubarikiwe mtumishi kwa maombi yako.
5. BARIKIWA SANA NDUGU MTUMISHI KWA SOMO LA MAOMBI YA KUFUNGA. NIMEKUPATA KUPITIA GOOGLE ULIFUNDISHA MWAKA 2015.
NIMEBARIKIWA SANA.
NIKUULIZE, BADO UNATEMBEA NA YESU AU ULISHAMWACHA? MAANA NI MIAKA MINGI, KWA YESU NI KUZURI SANA.
Majibu ya Mtumishi Peter Mabula.
"Bado naendelea na YESU KRISTO hadi uzima wa milele.
Hakuna namna naweza kumwacha YESU KRISTO.
Endelea kujifunza Neno la MUNGU na MUNGU akubariki sana "
6. Ooo mtenda kazi katika shamba la Bwana, Mungu akubariki sana, leo nimesoma somo lako ambalo linaitwa ""MWANAMAOMBI MAKINI"" Kupitia somo lako nimeongezeka uwelewa na maarifa.
Hakika ubarikiwe sana.
7. Bwana Yesu Asifiwe Mtumishi Namshukuru Mungu Kwa Maombi Yako Mimi Lucy niliwahi Kukupigia Uniombee Juu Ya Ndoa Yangu. Nashukuru Mungu Anazidi Kuonekana Asante Na Endelea Kuniombea Ili Iwe Vizuri Zaidi, Lakini Pia Somo La MAOMBI YA KUMILIKI MILANGO YA BARAKA ALIYOKUWA AMESHIKILIA ADUI Nilifanya Maombi Hayo Na Usiku Nikiwa Nimelala Nikaota Ndoto Nawateketeza Nyoka Wanne Kwa moto.
Asante Na Mungu Akubaliki Sana Sana Nataman Nitume Chochote Kwako Lakini Mambo Hayajakaa Vizuri Kwangu Maana Hata Kazi Tu Sina Ila Nazidi Kumuomba Mungu Nipate Angalau Chochote Kile Nami Nichangie Hata Uchapishaj Wa Vitabu Vyako, Naamin Mungu Atatenda.
8. JINA LA BWANA ALIE JUU LIINULIWE MTUMISHI MAOMBI YAKO YANAFANYA KAZI HAKIKA.
KUNA KIKWAZO NILIKUWA NACHO NASHANGAA KIMETOWEKA TU MPAKA NASHANGAA.
MUNGU AKUBARIKI SANA.
9. Bwana Yesu atukuzwe Mtumishi wa Mungu. nashukuru sana kwa somo lako juu ya KUMILIKI MILANGO YAKO YA BARAKA na nililisoma kwa bidii na maombi yake niliyaomba kwa imani kubwa, kabla sijalimaliza ndani ya gari la abiria nikakutana na binti mzuri mcha Mungu ambaye alinipendeza nami nipo mpweke kwa miaka yote ya maisha yangu bila mchumba, Sasa baada ya kuongea nae maongezi ya kawaida baada ya kama wik 2. Akaja kunitafuta napofanya biashara zangu ndogondogo na mpaka sasa tunawasiliana japo sinae mahusiano ila tunaonyesha uelewano, Hivo bado namsikiliza Roho juu ya nini nifanye zaidi, Naomba uniombee mtumishi ili tusikomee hapa bali tufunge ndoa takatifu.
asante sana.
10. BWANA YESU asifiwe mtumishi wa Mungu kwa kweli namushukuru Mungu sana kwa masomo na maombi yako nimeona mabadiliko mengi sana katika maisha yangu nilikuwa mtu wa kuteswa na ndoto mbaya sikuhizi sizioti tena maishani mwangu nimefanya kazi kwa mda mrefu bila kuona faida yoyote ila ashukuriwe Mungu Muumba mbingu na nchi ameniwezesha kununua shamba heka tano zidi kunikumbuka kwa maombi Ili Siku moja nipate kujenga nyumba, nilikuwa nilikuwa mtu wa hasira lakini siku hizi hata mtu anikasirisha huwa na furaha moyoni Mungu azidi kukubariki kwa masomo na maombi yako.
11. Mchungaji Mungu amezidi kudhihirisha ukuu wake. Baada ya kuteswa na mavyaa pamoja na mume wangu nimefaulu kununua uwanja hata nimeanza kujenga. Naomba tu neema na kibali cha kukamulisha ujenzi. Hakika Mungu yuko na hujibu maombi kwa wakati unaofaa.
Asante kwa kuomba nami Mara kwa mara.
Mama Jane Koimburi wa Kenya.
12. Mwinjilisti Mabula,Zidi kubarikiwa!Mungu wa Mbingu na Nchi ,Asikupungukie kitu!!!!!!!
I speak to you Evangelist Mabula!Receive breakthroughs,in health,peace,more spiritual growth and increase,wealth,financial,grace ,mercy and favour til HE (JESUS CHRIST)Come to take the CHURCH!!!!
Unanibariki sana na maombi yako ni ya ushindi mkubwa.
13. Bwana atukuzwe Mchungaji, Mchungaji nahisi Kama unaniona katika mawazo yangu, Kila kitu ninachopanga kukifanya unakitolea neno/Mafundisho. Jana nilishika Biblia nikaanza kusoma kitabu Cha Kumbukumbu la Torati naona Leo umenirahisishia kwa sababu nilikuwa nasoma ila Si unajua lugha Ni ngumu kidogo mpaka utafakari zaidi.
Lakini wewe umefundisha somo KWANINI KITABU CHA KUMBUKUMBU LA TORATI.
Na sio Leo Ni mara nyingi nikiwaza kusoma kitu au kuomba kitu nakuta kile kitu unakitolea neno/Mafundisho hivyo inakuwa rahisi Mimi kujifunza na kuomba.
Nashukuru Sana Mchungaji.
Nimejifunza kitu kikubwa Sana katika mafundisho haya na kwa vile toka juzi Jumamosi mpaka Jumapili nilikuwa nasoma mafundisho haya nilikuwa sijaelewa vizuri ila kwa ufafanuzi huu kwa kweli nimelielewa vizuri Sana kuwa mambo haya yaliwapata waisreli kwa jinsi ya mifano na yaliandikwa ili kutuonya sisi tuliofikiria na miisho ya zamani kwa hiyo anayejifikiria kasimamana aangalie asianguke. Funzo kwetu Ni kwamba labda tunafikiri tuko imara katika Imani na tunajiamisha kumbe tukipata majaribu kidogo tunaanguka kiimani. Kwa hiyo tujiweke imara kiimani ili hata tukijaribiwa tusianguke. Pia sehemu nyingine iliyonipa funzo kubwa Ni pale ulipoifananisha Safari ya wana wa Israel kutoka Misri kwenda Kaanani na Safari ya wateule wa MUNGU waliookolewa na Bwana YESU ya kutoka duniani kwenda uzima wa milele,,kwamba tusije tukaishia njiani.MUNGU atuongoze tufike Kaanani (uzima wa milele). Nashukuru Sana kwa mafunzo.
14. Bwana na Mwokozi Yesu asifiwe Mtumishi Mabula ,habari za uzima wako? Nami niko mzima nikimshukuru Mungu kwa kila jambo.
Naomba nikuambie leo hii nimepokea muujiza maana kile kifungo cha macho kilichokuwa kinanisumbua kimepotea.
Hivyo basi nakushukuru kwa maombi yako na ninaomba uendelee kunikumbuka. Pia ujumbe huu wa somo la KUREJEA KWENYE NAFASI haki ni wangu maana jana nilifunuliwa mafundisho na maombi yako yakifanya Mungu anibadilishe.
Pia nisaidie nawezaje kujua neno la Mungu sana kama wewe?
Barikiwa sana Mtumishi.

Comments