SHUHUDA CHACHE ZILIZOTOKANA NA MAOMBI NA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Hizi ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki walinitumia, nami nakuletea Kama zilivyo.
Sifa na heshima na utukufu wote ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni.
1. Habari za uzima mtumishi wa Mungu.
Napenda kukujulisha kwamba miezi mitano iliyopita nilikupigia simu saa moja usiku ili uniombee maana tangu mimi na mume wangu tufunge ndoa hatukuwahi kupata mtoto, na ndoa yetu ilivuka miaka kumi, kwa muda huu wote tulienda hospitali nyingi na kunywa dawa nyingi lakini bado haikuwezekana kushika mimba, watu walinisema sana na ndugu wa mume wangu ndio walizidi sana katika kunisema vibaya. Nilikata tamaa ya mwisho kabisa hadi nilioopata ujumbe wako Facebook nikapenda uniombee na siku hiyo ukanitamkia kwamba nitakapoingia katika siku za hatari mwezi unaofuata nitapata mimba, sijui kama unakumbuka mtumishi, ni kweli kabisa na ashukuriwe sana MUNGU maana kwa sasa niko mimba ya miezi minne, huu ni muujiza mkubwa niliousubiri miaka mingi. Asante Yesu mwokozi wangu na asante mtumishi kwa maombi yako.
2. Mtumishi Mabula nabarikiwa na masomo na maombi yako, tangu nimeanza kufuatilia masomo na mafundisho yako Mungu ameyabadili sana maisha yangu, nakumbuka somo la kwanza ni ile kusikiliza sauti kutoka ndani mwangu kumbe nilipokuwa mtii ni sauti ya Mungu.
ubarikiwe sana.
3. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Nashukuru sana kwa maombi haya, Mtumishi nilikuwa naumwa, nashukuru Mungu nimepona kabisa, maumivu yamebaki kwabali sana ,tatizo lilikuwa kubwa Nashukuru sana kwa maombi yako.
AMINA. Asante
4. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI.
MIMI MAMA FARAJI NAMSHUKURU MUNGU AMEMPONYA BABA YANGU KUTOKA KUTOKUONGEA NA SASA ANAONGEA KABISA.
MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI KWA MAOMBI YAKO.
5. Bwana asifiwe mtu.
Bwana ashukuriwe lile tatizo la kuumwa tumbo umeniombea jana leo nimeamka nimepona kabisa tatizo limenisumbua karibu week lakini leo nimepona kabisa Mungu akubariki baba mchungaji uendelee kutusaidia sisi wenye shida.
Amen
6. Shalom mtumishi wa Mungu.
Nakumbuka nilikushirikisha maombi ili niingiziwe pesa zangu ambazo ni haki yangu iliyopaswa kuongezwa katika mshahara wangu siku nyingi, uliniombea na kuniambia nitaingiziwa pesa hizo kwenye mshahara unaofuata na ukasema utaendelea kuniombea juu ya hilo, ni kweli kabisa kwenye mshahara wa mwezi huu pesa hiyo nzuri nimeipata na kuanzia mwezi huu nitakuwa naipata, tulioanza nao kazi wengi hawana hiyo pesa lakini Mungu amenitendea mimi muujiza, na nitazidi kutoa pesa zangu ili neno la Mungu liende mbele sana.
Mungu akubariki sana mtumishi, hakika nimemuona Mungu wa miujiza.

Comments