SHUHUDA KUTOKANA NA MAFUNDISHO NA MAOMBI.

SHUHUDA KUTOKANA NA MAFUNDISHO NA MAOMBI.
Nakuletea shuhuda hizi kama nilivyotumiwa. Sifa, heshima na utukufu ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni.
1. Mtumishi Mabula, nashukukuru sana mafundisho yako, yamenijenga sana utu wangu wa ndani kuliko maelezo. Nimejua mambo mengi kwa kusoma jumbe zako.
Mi nilipenda sana miujiza zaidi kuliko kumjua Yesu. Lakini kupitia mafundisho yako, hasa kuna somo la BAADA YA NGUVU ZA GIZA KUTOKA KWA MTU ufalme, nguvu na wokovu vinaingia, nililirudia Mara nyingi sana
Ntakukumbuka Mtumishi niombee sitakusahau.
2. Bwana Apewe Sifa, Kweli Kaka Umegusa Maisha Yangu.
Somo Lako la OMBA MUNGU AKUFUTIE MOYONI MAMBO AMBAYO UKIYAKUMBUKA YANAKUUMIZA, hilo somo Limebeba Historia Ya Ndoa Yangu, Iliyovunjika Miaka 10, Iliyopita Nilisingiziwa Hadi Ndoa Ikavunjika, Kweli Niliumia Sana Hadi Leo Maumivu Yananitesa Sana
3. Maajabu baada ya somo la MAOMBI YA KUOMBEA AFYA KIROHO . Yaani hapa Mtumishi umeniongelea mimi kabisa kuhusu haya maroho ya mizimu kutufuatilia babu yangu alianguka kutokana na kuumwa kiuno na miguu alipofikisha miaka 40, Baba yangu ambae ni mwanae wa kwanza nae alipofikisha miaka40 nae akaanguka kwa ugonjwa uleule lakini hospital tatizo halijulikani, Na mm ni mtoto wa kwanza kwetu mwaka jana nimetimiza miaka 40 nilianguka kiuno na miguu nimelazwa muhimbili miezi 2 hakuna nafuu yeyote nikarudishwa nyumbani nikawa naenda kwenye maombi angalau naweza hata kuoga kwa sasa. Sasa mtumishi kwetu ni mpaka ukatambike na mm nimegoma kufanya hivyo ili kuwanusuru wanangu je nifanyeje ili niweze kulishinda hili.
4. Mungu apewe sifa mtumishi. Mtumishi wewe hakika ni mtumishi wa Mungu kabisa alikuita umtumikie. Sio kwa maajabu haya kila siku. Binafsi nashindwa kuacha kukushuhudia.
Usiku wa kuamkia juzi usiku wa manane nilipopata shida ya mumivu makali ya ajabu kama nilivyokuwa nimeota naumwa kushtuka nikakuta niko vilevile, siwezi kuelezea yale maumivu, mtumishi unakumbuka kwa kifupi nilivyokueleza. Nilishindwa kuomba nikamweleza mume wangu akaamka akaanza kuomba juu yangu. Mimi yale maumivu nilishindwa kuongea zaidi ya kusema "Yesu naomba uniokoe na hizi nguvu za giza, najifunika kwa damu ya Yesu, Mungu naomba uyakumbuke maombi yangu"
ndani ya saa na nusu nilipopata nafuu nikakutumia sms japo nikiamini hata kama usipojibu umeniombea, baadae nilipata nafuu na simu yako ikaingia meseji ikisema "Mungu anakuponya hakika".
Jana mchana saa nane nipo natembea naenda sehemu ugonjwa ukaanza japo si sana ghafla ikaingia sms yako inasema "Mungu anaenda kukuponya"!!!! Nilitabasamu kwanza nikasema kwa sauti hakika huyu kateuliwa na Mungu, muda mfupi maumivu yalipotea. Namshukuru Mungu sana kuniponya na kuniokoa na haya magumu yanayonijia. Mtumishi naamini maombi yako kuwa kila kitu unaweza kuomba na kikawa, kweli Mungu alikupa funguo nyingi, maana kwangu tu umefungua milango mingi hata la jana pia. Pamoja na uelewa wangu mdogo moja kwa moja hili la juzi niliamini ni nguvu za giza ndio maana sikuwaza kwanza kwenda hospitali, hakika Mungu alipendezwa na wewe kukupa kazi hiyo, ubarikiwe sana na Mungu namuomba azidi kukuongezea funguo. Naomba usinichoke nimejawa imani ya kuleta milango yote iliyofungwa uifungue. Asante sana mtumishi kwa kutoa muda wako kunisaidia, jana uliponiombea mpaka sasa sina shida kabisa. Bila kujizuia naweza kuandika kurasa 10 kutoa shukrani kwa Mungu . Barikiwa tu na familia yako.
5. Bwana Yesu apewe sifa Mtumishi wa Mungu acha Leo nimpe Mungu Utukufu kwa kukutumia wewe kunifanya mimi leo nilivyo maana najihisi mwenye furaha mno
Mungu alianza kunifundisha Neno lake pasipo mimi kujua tena maneno yaliyokuwa yananifunza niache dhambi, sikujua lakini ilifika hatua mpaka nikaanza kuhubiri injili pasipo mimi kujua ni wito wa Mungu lakini nikihubiri injili makanisani jumapili bado siliishi neno natenda dhambi tena siku hizo mabinti yananipenda sana kuona na hubiri, lakini namshukru Mungu kwa NEEMA yake ya ajabu mwaka Jana mwezi wa 5 nilipo maliza chuo, ufunuo wa Mungu ulinijia na kusema na baada ya Mungu kusema na mimi kupitia maandiko na kunipa kibali cha kuhubiri watu wanabadilika akaona sibadiliki akaona aseme nami tena ilikuwa asubuhi akaniulizi "hivi tangia uanze kutenda dhambi umeshapata Faida gani?"
Nilishangaa na nilikosa jibu na cha ajabu akataja dhambi zilezile zilizokuwa zikinitesa, tangia siku hiyo nikasema nimeacha dhambi, na ni kweli nikaacha lakini jibu likaja "nani atanifanyia sala ya Toba?"
Lakini Mungu huyu acha aitwe Mungu ndo maana nasema kwamba mimi siwezi kukwambia nilikuona wapi wewe Mtumishi P Mabula na sikuwai kuona page yako Fb,wala kuwa na namba yako ya WhatsApp lakini wakati najiuliza nani wa kunifanyia toba nikaona unanitumia maandiko WhatsApp ya Neno la Mungu kila wakati mpaka nikaijua page yako ndio roho yangu ikazidi kuwa na msukumo zaidi kwamba "ukimwambia huyu Mtumishi atakufanyia TOBA" na ndio mwaka Jana tu mwezi wa 12 karibu na sikukuu nikakupigia ukanifanyia sala ya Toba na kumbuka Niko wilaya ambayo sio kwetu japo mkoa ni mmoja na nilishaomba kuhubiri wakakataa, lakini uliponifanyia toba, sasa usiku wa mkesha wa mwaka mpya mwinjilisti akaniita nifungue sifa ikiwezekana nitoe ushuhuda basi nilifanya hivyo kwa Mara ya kwanza mkesha wa mwaka mpya unanikuta kanisani Mara nyingi ulikuwa unanikuta disko, basi siku hiyo nilifurahi mno, pamoja na kuwa mgeni sehem hiyo lakini Mungu alinipa kibali tena baada ya kutubu lakini nikasema moyoni kama mwaka nimeuanza hivi basi mwaka huu utakuwa wa kushangaza kwangu hasa kumtumikia Mungu, na ni kweli baada ya hapo pakatokea mwezi wa 2 mkutano wa injili kata jirani wa siku nne nikaenda kwa kweli pamoja na ugeni wangu sehemu hiyo niliruka sifa mpaka watu wengi wakabaki wananishangaa hata mimi binafsi, mkutano huo wa injili ulipoisha tukatoka lakini baada ya hapo nikawa na muomba Mungu mbona nina uwezo wa kuhubiri na karama hii ushanionyesh lakini mbona sikubaliwi huku kuhubiri kama sehemu zingine nilizopita? nikajaribu kuwaita vijana ili tuwe tunajifunza Biblia wakakubali lakini siku tulizo kuwa tumepanga hawakutokea mpaka nikagundua huenda Mungu hajanipa kibali ktk hili nimetumia akili zangu tu, lakn palikuwepo kikundi cha wana Maombi kikafa kwa sababu mbali lakini waliokuwa wamebaki wanatembea krb km 3 hadi 4 kwenda kanisani lingine kufjata mafundisho na Maombi sasa siku1 wakiwa wanachangia mada kanisani nikaamsha mkono kuhoji juu ya wana Maombi nao sikia wako wapi vichakani? au mbona huwaga siwaoni? Na watu walikuwa wameshaanza kunijua kuwa naijua biblia baada ya kutoka kanisani siku ile wana Maombi wakanifuata wakasema "ni sisi" wakanielezea lkn wakaniambia kwa sababu wewe unalifahamu neno la Mungu tunakuomba tupange siku uwe unakuja unatufundisha nikasema sawa tukapanga mwezi huo huo wa pili baada ya kutok ktk mkutano wa injili Mungu akiwa Juu yangu kwa kutumia Vichwa vya mafundisho yako mtumishi Mabula na summary ya vifungu vya Biblia vyako na nilivyo kuwa mimi najua nikachanganya basi watu wakawa wana barikiwa na wanabadilika namshukru Mungu sifa zangu zikaenea wakasema kijana yule yuko vizuri tukaitiwa mgonjwa alikuwa amefungwa na pepo kifuani linamzuia kula karibia siku tatu hajala akasema watuite tumuombee tukamuombea ndani ya siku tatu akapona kabisa mpaka Leo kwa kutumia somo lako la kuita Afya kwa wagonjwa na somo la kutoa pepo tena alikuwa muislamu huyo kijana tuliyemwombea sifa zikazidi kuenea na kumbuka Niko ugenini lakini Mungu alizidi kunipa kibali kwa hiyo kwa njia hiyo ikanifanya hata kanisani kupewa nafasi mbalimbal za huduma za kiroho kuwazidi wenyeji japo mimi ni mgeni na kuanzia krpind kile Mungu akanipa kibali cha kurejesha kikundr cha wana Maombi mpaka wa Leo kikundi kinazid kufanya vizuri kwa Neema ya Mungu na kuwaombea wagonjwa nao wanapona,lakini cha ajabu zaidi kuna mama mwenye maono ninayefanya nae sanr karz hii ya utumishi akiona kitu kunihusu au kutuhusu sisi wawili kuhusu huduma lazima tu kitokee na Mungu anatenda kwa hiyo ikazidi kunipa moyo zaidi sasa juzi nilikutumia mafunuo ya maandiko niliyo yaona kupitia mfungo wa kufunga ili kanisa langu kuwa na umoja kiroho maana weng hawajaokoka na wanatusimanga sana sisi tuliookoka, Kanisa letu sio la kiroho yaani sio makanisa ya Kilokole. Sasa juzi mwinjilisti kanisani wakawa wananizungumzia mwinjilisti mwingine akamwambia tunataka kijana huyu(Mimi) ikiwezekana awe anahubiri kila Jumapili. Mama mmoja ameniambia kwamba mwinjilisti Alisha nichukua mpaka kwa mchungaji ili anipe kibali cha kuhubir kila jumapili.
Kikubwa nasema mpaka saiv nawaza maajabu Mungu anayo yatenda nashindwa kuelewa
Lakini yote ya Yote ashukuriwe MUNGU muumba mbingu na nchi ktk jina la BWANA YESU KRISTO aliye nipa karama hii Sifa,Utukufu,Heshima na Uweza vina yeye Mungu ktk jina la Yesu Kristo, lkn nimshukru kwasababu ya kukuleta wewe Mtumishi Peter Mabula ktk maisha yangu ambayo wewe ndio ulikuwa na ufunguo huo kwangu wa kunifungulia Baraka na endelea kutuhudumia kwa uwezo wa Mungu ktk jina la Bwana wetu Yesu Kristo na kama huu ni mwezi tu wa tano tangia ni okoke rasmi acha zile nilizokuwa natumika huku bado Niko gizani je nikija kufika mwaka na zaidi Mungu akipenda aise Matendo ya Mungu yamenishangaza sn, naomb Mtumish wa Mungu zidi kuniombea mm mwnyw nawaza sana utukufu wa Mungu mpk naogopa sn, na hii nimetokan sijawahi funga siku 7 lkn tangia Jumatatu nilipo funga nilisikia msukumo wa kufunga siku hzo saba pamoja na mama yule wa maono na ndo siku hzo saba Mungu amenionesh Isaya 58:1_2 na mafunuo mengne na Leo kunipa kibali cha kuhubiri na ikawa gumzo sana mtaani
Lkn pia kupitia mfungo huo Bwana alisema nasi kupitia mazingira tuliyo nayo na kwa utu wetu wa ndani kuwazungukia wana Maombi walio anguka kipind kile sijaja kuwachukulia injili na wale wana Maombi wanao umwa na wagonjwa mbalimbal wa mtaa ninao kaa na tumefanya hvyo tangia wiki iliyo pita mpk Leo
Hakika tunaye Mungu Baba wa mbinguni asieshindwa Bali anaweza haijalishi wewe uko sehemu ambayo ni mgeni kama Mimi lakini Mungu akikupa kibali kama unamtumikia ktk Roho na Kweli atakupa kile unachokihitaji
Amen,Amen,Amen,Amen,Amen

Comments