SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKANA NA MASOMO NA MAOMBEZI.

SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKANA NA MASOMO NA MAOMBEZI.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu!.
Hizi hapa chini ni baadhi ya shuhuda walizonitumia baadhi ya marafiki zangu kutokana na masomo yangu na kutokana na maombi. Nakuletea shuhuda hizi kama zilivyo.
Sifa zote, heshima yote na utukufu wote ni kwa MUNGU Baba katika KRISTO YESU Mwokozi wangu.
1. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi.
Bwana Mungu ashukuriwe lile tatizo la kuumwa tumbo umeniombea jana leo nimeamka nimepona kabisa tatizo hili limenisumbua karibu week lakini leo nimepona kabisa, Mungu akubariki baba mchungaji uendelee kutusaidia sisi wenye shida.. Amen
2. Mtumishi ubarikiwe mno , manake nimekuwa nikifuatilia michango yako mingi sana sana , umetenda vema sana hata mimi mwenyewe umenisogeza mahali kutokana na masomo yako, ni mengi umetoa ila mimi nimebahatika kuandika zaidi ya 20 na naendelea kuyatunza ili na wengine wafaidi , point nina shida kidogo naomba unipe maelekezo , kuhusu huyu mchawi aliyepandikiza mapepo kwa mdogo wangu , manake sitaki kwenda kichwa kichwa nataka nipate maarifa kwanza. "Barikiwaa .
3. SHALOM MTUMISHI BWANA ASIFIWE SANA
MIMI NI KUTOKA ARUSHA
NINA USHUHUDA NA HII AUDIO YA MAOMBI ULIYOITUMA.
MTUMISHI NIPO KWENYE MAOMBI YA TOBA YA SIKU SABA, ILIKUWA SAA TISA JIONI HUWA NAPENDA NIKIWA NAOMBA HUWA NAWASHA TV KWA SABABU ENEO NINALOISHI KUNA STUDIO KUEPUKA ULE MWINGILIANO WA SAUTI .
SASA NILIKUWA NIMEUNGANISHA KWA BROOTOTH NILIKUWA NIPO KATIKATI YA MAOMBI NDIYO IKAFIKIA HII AUDIO YAANI BAADHI YA MAHITAJI NILIYOKUWA NAOMBA KAMA HAYOHAYO ULIYOKUWA UNAOMBA.
YAANI YAMENIGUSA KWA KIASI KIKUBWA SANA.
Mungu akubariki sana akuinue viwango hadi viwango
4. Bwana Yesu asifiwe mtumishi. nashukuru Mungu aliniponya basi baada ya maombi yako, kwa sasa niko mzima kabisa napata haja kama kawaida, sifa nautukufu nazirudisha kwake Mungu.
Mungu akubariki sana kwa kuniombea
5. Mtumishi Mabula hongera kwa kazi nzuri ya kutuinjilisha, masomo yako yananisaidia sana. nakushukuru pia umesaidia watu zaidi ya 3 ambao walikuwa wagonjwa sana nilitoa namba zako nikiwambia kwako watapokea uponaji.
Wamepona muda mfupi toka umeomba. Sifa na utukufu tumrudishie Mungu. Dada mmoja alibaki kuwambia watu ohooo fulani namba aliyonipa ndio palikuwa dawa ya kumponya mwanangu.
Maneno mengi ya shukrani ambayo ananipa mpaka sasa nakujulisha mtumishi. Na namrudishia sifa Mungu.
Barikiwa sana Mungu azidi kukufunulia zaidi.
Amina! Nakumbuka upande wangu kwa ndugu umefanya vitu, nikiunganisha na haya na shuhuda ninazosoma fb namkubali Mungu kweli alikuteua umtumikie. Hongera sana.
6. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Ngoja nikupe ushuhuda unaotokana na historia yangu na jinsi nilivyokupata Facebook na juu ya somo la leo lisemalo MUNGU AKUFUMBUE MACHO ILI UZIONE BARAKA ZAKO.
Historia fupi juu ya haya uliyofundisha.
Kwangu kuanza kukutaka wewe uniombee
Nilikuwa FB nikakutana na maombi yako ukiwa umepost kwenye group la mtu mwingine,basi nikawa nayasoma mara kwa mara nikachukua namba zote mbili yako na mwenzako ,kila nikitaka kumpigia roho inasita nashtukia dakika zimeisha,siku moja nikaweka vocha ili nimpigie nikapiga mpaka nikachoka,nikaamua kumuacha nikafuta namba yake ,kesho yake kulikuwa na kijana mmoja mtumishi kutoka mwanza ,rafiki yangu mmoja akaniambia tumeanzisha kituo cha maombi twende kijana huyu anakuja kwetu,basi kesho yake nikaenda,walikuwa watu kama kumi tu ,akafundisha ili kumpata baba wa kiroho ,ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia neno hilo,nikamuuliza inawezekanaje huyo baba ???au ni baba wa ubatizo???Akaniambia Leo nitakufundisha na tutaomba mpaka utampata baba yako wa kiroho,nikaanza kumsikiliza,nikamwambia kuwa nina tatizo kubwa kuliko hilo la baba wa Kiroho,akaniambia mama yangu unashida gani ???nikamwambia ninaumwa pia kuna kitu kinanisukuma huku mgongoni,akasema Mimi ni Mtumishi wa Mungu usinishangae amini tu yote yataisha,Basi Mungu akanipa roho kumwamini nikamwamini tukaendelea na maombi,Siku hiyo ndo mwanangu ametolewa nje sijalipia kodi ya chumba chake huko chuoni akapiga simu analia nikatoka nje ,aliponielezea nikaanza na mimi kulia nikafuata Biblia yangu, mtumishi i huyo akaniuliza mama umekuwaje???
Kilio kikaongezeka akanisogelea akashika Biblia yangu,baada ya muda nikamweleza,akasikitika ,akasema ngoja nikuombee kwanza usiondoke ,basi akaanza maombi,nikachoka nikakaa,
Story ndefu ngoja nikueleze mafundisho haya uliyofundisha leo ni kweli.
Baada ya maombi nikamwambia naona sasa unaweza kuondoka.Nikamwambia sasa najisikia moyo amani,hapohapo simu ikaita nikaiangalia nikatoka nje mdogo wangu ananiambia nimemtumia mwanao shilingi laki mbili sijui atanunulia nini ,nilirudi kwa kicheko nikamshika mkono huyo mtumishi nikatoa na ushuhuda ,uwezi amini basi acha Mungu aitwe Mungu.
Tukiwa tunaendelea na mafundisho jinsi ya kumpata baba wa Kiroho ,tukaanza kuomba juu ya hilo jambo, sikuelewa kitu,baada ya maombi nikamwambia bado ujanisaidia hiki kitu kilichopo mgongoni mwangu huku mabegani??
Akaniita akanishika mkono tukiwa tumekaa kila mtu kiti chake akiwa ananiombea kikasinzia akafikiri nina mapepo ndani ya dakika chache tu nikashtuka, akaniulizia unajisikiaje nikamwambia ngoja nijinyooshe nimechoka,basi nikajinyoosha,hapo imefika saa kumi nikamwomba kuondoka akanipa mawasiliano ,nikaondoka,nilipofika nyumbani nikachukua simu yangu kama kawaida yangu kufuatilia maombi ,nilipofungua ukurasa wako Facebook simu ikazima,nikajaribu kuiwasha inagoma sikuwa na umeme kipindi hicho,kesho yake nikaipeleka chaji ,mchana nilipotoka shambani nikamtuma mtoto aniletee ,akakuta haijawekewa moto,nikamwambia apeleke kwingine akakimbia akaipeleka,jioni kuifuata wakasema hawaioni ,akaja akanibia,nikakosa la kufanya,wakanipatia ya kutumia kwa muda wakati wanaitafuta,ilikuwa ya kawaida haina FB,Baada ya wiki moja hivi nikiwa naendelea kusoma yale niliyoyatoa katkra FB kwenye ukurasa wako nikapata,nikapata simu nyingine ,nilisoma siku hiyo usiku mzima sikumaliza nikachoka nikalala,
"''Pazuri hapa sasa'"
Nikiwa nimelala zilitoka picha tatu machoni pangu,mmoja mama niliyekuwa nasali nae ni RC akiwa amekaa ila alikuwa anaonekana kwa mbali sana na kuna giza,
Baadae mwanga mkali ukatokeza mbele yangu ukatokea wewe Mtumishi Peter Mabula ukiwa na suti ya bluu na huyo mtumishi wa kwenye ile pale yeye amevaa suti nyeupe ukanyoosha mkono wako ukanisimamisha,
Kesho yake nilihangaika sana kutaka kujua nini nimeonyeshwa nikamwelezea yule mama akanijibu unawafahamu hao watu ,nikamwambia hapana ila huwa mawaona kwenye Facebook,tukafungua FB nikawatafuta ,kufunua ukurasa huo yule mtumishi alikuwa anahubiri na suti yake hiyo nyeupe,nikaenda kwako nikakuta umevaa suti ya bluu ndani shati nyeupe hiyo niliyoiona,yule mama akaniambia mtafute huyu aliyekushika mkono uongee nae,nikarudi nyumbani nikaweka vocha nikapiga simu inatumika tuu muda mrefu ,baadae ukanitumia msg nipigie nilipopiga nikakwelezee shida yangu ukaniombee na nikafunguliwa.
Tangu siku hiyo maombi yako na mafundisho yako vimeniponya na kunifikisha hapa nilipo .
Kweli hapa Mungu alinipa macho ya rohoni kweli kweli wala sikubahatisha.
Niombee na ipo siku nitakuja huko kanisani ulipo ili unishike kweli kweli mkono wangu na kuniombea ,
Somo hili limenikumbusha maisha yangu huko nilikotoka kilio kila siku
Leo nacheka kila kukicha ,
Nikulipe nini!!!??
niseme nini !!???
nashukuru Mungu kwa kila jambo
Asaaaanteeeee
Saaaaanaaaa
Mungu akubariki
Nitaomba nami juu yako kila itwapo leo
AMINAaaaaa
7. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Namshukuru Mungu kwa maombi yako naona mabadiliko makubwa ndani yangu ipo kiu ya kusoma neno la Mungu, kuomba na kusikiliza mafundisho ya neno la Mungu.
Lakin kabla ya maombi yako nilikua mkame kwenye kila eneo, Mungu akubariki sana

Comments