SHUHUDA MBALIMBALI.

SHUHUDA MBALIMBALI.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Hizi hapa chini ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki zangu walinitumia baada kujifunza neno la MUNGU na baada ya kuwaombea.
Nakuletea shuhuda hizi kama zilivyo.
Katika shuhuda hizi sifa, heshima na utukufu wote ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni ambaye ndiye mtenda miujiza.
Karibuni.
1. Bwana Yesu asifiwe mtumishi Mabula.
Ninamshukuru Mungu sana tena sana maana jumapili iliyopita nilivalishwa pete ya uchumba Kanisani na picha nitakutumia. Sikujua kama ningekuja kupata mchumba maana nilifika hatua nikakata tamaa kabisa. Asante kwa maombi yako Maana uliniombea na kunitia moyo kwamba ni mwaka huu nitapata mume na kweli imetokea maana uchumba tayari na mahari tayari na sasa tarehe ya kufunga ndoa imeshatangazwa hivyo namshukuru sana Mungu kwa muujiza huu.
2. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI, MIMI YULE DADA MJAMZITO AMBAE ULIMUOMBEA KWA SIMU.
Nakumbuka nilikueleza hali ya uchumi si nzuri na suala la roho ya mauti na hali ya kufungika kimaombi mahali hapa ambapo nimepanga...
Kipekee namsukuru sana MUNGU naendelea vizuri nasikia utofauti mkubwa kwenye eneo la kuomba kwangu na ile hali ya mauti juu yangu na mtoto aliye tumboni inatoweka najisikia raha sana tofauti na mwanzo nilikuwa na msongo wa mawazo na unyonge ambao hata sababu sijui..
Eneo la uchumi nimepata hela kidogo nimenunua ubuyu ninaanza kuuza sasa nina amini MUNGU anakwenda kuinua uchumi wangu kupitia hiki kidogo nitainuka...ninajisikia ndani yangu hali ya kuthubutu ambayo awali nilikuwa muoga hata kulifanyia kazi wazo linalokuja ndani yangu sasa hv najisikia kuweka kwenye matendo na nikifanya naona nafanikiwa kwa mfano kutengeneza bites nimejifunza mtandaoni na nikaweza kuthubutu kuweka kwenye matendo na nikaona matokeo mazuri sikuwa naweza kusubutu kabisa HAPA NAMSHUKURU SANA MUNGU SANA.
ASANTE KWA MAOMBI YAKO MAANA NAAMINI NAENDA KUJIFUNGUA SALAMA PIA BIASHARA YANGU INAENDA KUSHANGAZA WENGI.
3. Bwana YESU KRISTO atukuzwe mtumishi! Napenda Kutoa ushuhuda Jana uliniombea na mke wangu juu ya nguvu za giza zinazotusumbua ili tupate watoto ktk ndoa yenu. sifa na utukufu kwa MUNGU BABA WA MBINGUNI. usiku wa Jana kuamkia Leo tuliamka kuomba saa 8 na nusu usiku wakati tunaomba katikati ya maombi tulisikia sauti ya paka akipga makelele Kisha akaanguka chini na baada ya kuanguka hatukusikia kelele tena tuliendelea na maombi Kisha tukarudi kulala hakika Bwana atatushindia maana sisi ni washindi kwa Damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO .
4. Bwana Yesu asifiwe ninapenda kumshukuru Mungu kwa maombi yako juu ya afya ya mama yangu na ya family yetu nzima tunaendelea vizuri kabisa kwa sasa.
5. Bwana YESU KRISTO asifiwe mtumishi napenda nitoe ushuhuda huu katika maisha yangu nilikuwa sijui kunena kwa lugha hutokeaje, Sasa Jana wakati tunafanya maombi na mke wangu kabla ya kulala usiku ghafla nilianza kuomba kwa sauti kubwa na Mara nikaanza kunena kwa lugha mdomo tu wenyewe nilishangaa nanena kwa lugha Hali iliyomshangaza hata mke wangu namshukuru Mungu wa Mbinguni kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU.
Asante kwa masomo yako na maombi yako hakika ninasogea hatua kwa hatua.
6. Habar ya uzima mtumishi,,,Ahsantee kwa maombi yako Nimepata sehemu ya kufanya kazi hata kama sio serikalini namshukuru sana Mungu.
Maana nilitafuta ajira kwa muda mrefu sana hivyo nashukuru kwa maombi yako maana matokeo nimeyaona kwa kupata kazi.
7. Bwana YESU asifiwe mtumishi! Napenda Kutoa ushuhuda kutokana na mafundisho yako niliwahi kukushirikisha juu ya nguvu za giza zinazotusumbua nikafunuliwa matendo10:5 ukaniambia nahitaji mtumishi ili anifungue na uliniombea pia sasa Jana mtumishi mmoja anaitwa Frolian alikuja kunifungua mimi na familia yangu tulikesha tunafanya maombi nimefunguliwa na Sasa nmepokea baraka zangu Ambazo adui alikuwa amezizuia walikuwa wanapitia kwa mke wangu maana walisema ana imani
ndogo ndio waliingia wakanifunga kizazi changu.
Pia walisema jina langu kuzimu hata kuzimu wanalijua.
Mimi ni kijana ambae nampenda Sana YESU KRISTO nafanya maombi Kila siku ninawachoma lakini pia waliingia kwangu mwaka 2016 baada ya Mimi kutenda dhambi ya uzinzi. Nilitupiwa jini na mtu mmoja ambaye Sasa yupo kahama anafanya biashara nilisoma naye shule ya msingi na sekondari huko Tabora lilikuwa uvunguni mwa kitanda.
walikuwa wakishirikiana pia na wachawi wawili wanaoishi huku Mutukula Kagera.
Lakini wakishirikiana na Mama yake rafiki yangu uliyesomatuliyesoma naye ambaye ndio amemrithisha uchawi huyo mwanaye tuliyesoma naye. Wamesema mke wangu asiposimama imara watarudi tena.
Namshukuru sana MUNGU BABA WA MBINGUNI sifa na utukufu anastahili yeye pekee Asante YESU kwa ROHO MTAKATIFU.
Vile vile wakati tunashukuru Nilinena kwa lugha Kisha nikawekwa wakfu kuwa hakuna Nguvu za giza ambazo zitashindana na Kuna maneno yalisema kazi ya mtumishi alikuwa ananiombea atazidi kukua zaidi .
Sasa napokea baraka zangu kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO. Amen amen amen.


SHUHUDA KUTOKANA NA MAFUNDISHO AU MAOMBI.
Hizi ni baadhi ya shuhuda walizonitumia baadhi ya marafiki zangu ambayo walijifunza mafundisho ya Neno la MUNGU na niliowaombea.
Nakuletea shuhuda hizo kama zilivyo.
Utukufu wote kwa MUNGU Baba wa mbinguni.
1. Shalom Pastor!!
Kuna kipindi nilikuomba uniombee nilipokua najipanga Kuanza ujenzi wa nyumba yangu.
Namshukur Mungu kwa maombi yako sasa Hivi nimefika level ya Rinta.
Nakushukuru Sana Pastor kwasababu umekua Mwombezi wangu, Mwalimu wangu na, Mshauri kwa Mambo ya kimwili na Kiroho.
Kiukweli nachelea kusema kwamba umekua msaada mkubwa sana kwenye maisha yangu.
Mungu aendelee kuinua maisha yako ya kiroho na kimwili uendelee kustawi na kunawiri daima.
2. Bwana asifiwe baba mchungaji nakushukuru sana maombi yako nimepona kabisa tatizo la kutokwa na damu Mungu akubariki sana.
Nikitokwa na damu mwezi mzima mfululizo lakini uliponiombea damu ilikata na tangu hapo nikapona.
3. Bwana Yesu asifiwe mtumishi. Mtumishi mimi nataka nikutumia sadaka yangu ya shukrani ya kumshukuru MUNGU Kwa matendo makuu aliyo nitendea, nakumbka mwaka jana ulikua unaniombea na ukawa unanitia moyo sana kuwa nitapata mchumba mzuri ambae ni sahihi. Baada ya kuachwa na yule wa kwanza nikitaka kujiua ndipo nikakupigia nikiwa nimekataa tamaa ya maisha, baada ya kuniombea uliniambia kwamba nitapata mchumba sahihi kabisa na atakuwa mzuri kuliko hata aliyeniacha. kiukweli nashukru Mungu sana sana maana kuna wakaka wanne wote wananitaka wawili ni niwapetekoste na wote wananiambia hawana nia mbaya na mimj bali wanattka tufunge ndoa takatifu na sio mengineo, bado sijajua nimkubali yupi. kiukweli namshukuru sana MUNGU pamja na wewe mtumish.
Nina amani sasa.
Mungu akubariki sana sana.
4. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Namshukuru Mungu maana tangu umeniombea naona mabadiliko makubwa.
Hakika wewe utanisaidia sana, hata wabaya wanijaribu vip hawataweza. Kwakweli sifa hizo za kweli kutoka kwenye sakafu ya moyo.
Na namuomba Mungu anisaidie nipate sadaka itakayompendeza yeye niitoe kupitia kwako ikithiirisha haya ninayoongea.
Ukoo wetu unayo magumu, mimi angalau nayashinda kupitia maombi, nikiamini ipo siku wakuu wa giza watachoka waachane nami.
Nafikiri kuna kitu unakumbuka maana ni mengi nilikwambia juu ya majaribu niliyopitia.
5. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi wa Mungu nashukuru sana kwa maombi yako ulinombea kuhusu kutoa jasho na kunuka kwapa kwa kweli Mungu ni mwema nimepona kabisa ile hali imeisha kabisa nipo huru sinuki wala kuvuja jasho Mungu akubariki sana uzidi kubarikiwa asante sana.
6. Bwana Yesu asifiwe mtumishi!
Barikiwa sana !!
Mtumishi kuhusu somo hili ulilofundisha la KUTOKUTOA UDHURU KWENYKWENYE KAZI YA MUNGU nina ushuhuda mkubwa mno lakini Mungu ni mwema hakika amenishindia na Nina amini sitakuwa na udhuru katika kazi yake maana nishajua alichoniitia na ninaona ukuu wake ninapo hubiri injili yake japo bado nakaza mwendo lakini najua kidogo alichonipa na kikubwa atanipa zaidi maana namwamini yeye kuwa anaweza
Juzi tu jumatatu nilikuwa nimefunga kwa ajili ya kanisani maana kanisa yetu haina kabisa umoja wa kiroho kuna Wakristo tuliookoka na kuna ambao ni wakristo lakini hawajaokoka yaani kama matukano kwao ni sawa, kulewa ni sawa n.k, Hivyo kanisa tunapigia pagumu sana.
Lakini ilipo fika jumatatu usiku nimelala ndoto ikanijia ya kwamba nipo nasoma Isaya 58:1-2 ila sikuelewa hili neno lilijirudiatena ilipofika saa 8 uck waga naamka kuomb, nilipokuw naomb nikaikumbuk hyo ndoto yangu, lkn wakt nikiendelea kuomba nikafunuliwa pia
Isaya 50:1-2 na Isaya 52:1-2 utasoma uelewe vzr Mtumishi ukiwa na cha kunishauri utanishaur sasa baada ya kumaliza kuomba ikabidi nisome maneno hayo maana nilikuwa siyajui lrbuda hii ya Isaya 58:1-2 nahisi nilikuwa nimesha isoma kwenye maeneo mengne nahisi ni kwenye mafundisho yako lakini nilikuwa siikumbuki inasemaje maana nahinahisis ni muda mrefu nimeisoma na nilipo isoma nikaona ni mojawapo ya majibu kutoka kwa akinijibu napaswa ni fanye nini japo wito wangu nilijua ni kuhubiri lakini nilizidi kumuuliza Mungu ni "kweli Nina kibali cha kuhubir machoni pako? "
Lakini kilicho kuja kunishangaza ni kuhusu Isaya 50:1-2
Nilipo itafakar nikagundua inanijibu kuhusu kanisa langu nililokuwu nimelifungua nikimuomba Mungu alete umoja wa kiroho kanisani na watu waokoke, Mungu akaonyesh bado yuko nasi pamoja na kanisa letu lakini cha kufanya ni kutubu, maana dhambi za kanisa letu ndo zimetutenga na Mungu nilivyoelewa Neno
Lakini bado naendelea kumuita Mungu anifundishe zaidi kuhusu maandiko haya na mafunuo mengne ambayo amewah kunifunulia.
7. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Nakumbuka nilikutumia ujumbe ya kwamba naumwa, nashkuru Mungu nilipona, ila tangu nipone afya yangu imepungua sana nashindwa shida ni nini mwili unazidi kupungua japo siumwi naomba unikumbuke katika maombi yako, hakika nimejipata kufunguliwa kwa fundisho la kuombea afya Mungu akubariki sana.

Comments