SHUHUDA MBALIMBALI. 
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Hapa chini ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki zangu wamenitumia, shuhuda hizo zinatokana na maombi na zingine zinatokana na masomo ya Neno la MUNGU.
Nakuletea shuhuda hizo kama zilivyo, sifa, heshima na utukufu wote ni kwa MUNGU Baba Mwenyezi Muumba mbingu na dunia.
1. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Namshukuru sana Mungu hatimaye nimefunga ndoa takatifu.
Asante sana mtumishi kwa maombi yako.
Mungu akubariki sana.
2. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Napenda nitoe ushuhuda huu nilikuwa sioti ndoto kabisa lakini baada ya wewe kuniombea kwa sasa naota ndoto.
Ubarikiwe sana mtumishi.
3. Bwana asifiwe mtumishi Mabula.
Somo hili la MAOMBI YA KUFUTA VIFUNGO VINAVYOTOKANA NA NDUGU limeibariki sana hata nikajipata natokwa na machozi kwa kuwa limenikumbusha mambo mengi sana niliyowahi kunenewa na watu na sasa nimejua ndio yamenifunga, kuna kijana aliwahi niambia sitawai olewa, na kusema kweli kila nikipata mchumba huniacha bila sababu ilifika mahali nikajitamkia hiyo laana mimi mwenyewe kwamba sitaki kuolewa baada ya kuvunjika kwa kila uchumba ninaojaribu.
Naomba unikumbuke kwa maombi kwa sasa nina miaka 28 na sijisikii kuanza mahusiano na mtu yoyote kuna wanaume wawili wananiomba uchumba, mmoja tuliwahi kuwa kwa mahusiano tukaachana lakini kwa saa hizi ananiambia anataka kunioa na wa pili ni mwimbaji kutoka Tanzania tulipatana tu kwa mtandao akaniomba tuwe marafiki na sasa anasema anataka kunioa Naomba unisaidie maombi kwa ajili ya hilo Mungu azidi kukubariki.
4. Bwana Yesu Asifiwe Mtumishi. Nimetuma zaka na sadaka ya shukrani kwa Mungu kupitia kwa mwanae Yesu Kristu kwani nimefaulu evaluation iliyofanyika Ijumaa tarehe 06/09/2019 hapa chuoni Australia kama nilivyo kueleza. Asante pia kwa kuniombea kwa Mungu. Kwani hakika nimeona wema wake kwangu. Tafadhali naomba uendelee kuniombea. Asante na Mungu wa Ibrahim na Yakobo aendelee kukubariki.
5. Bwana Yesu asifiwe mtumishi
Nashukuru mnoo kwalile somo ulilofundshaga juu ya MAOMBI YA KUOMBEA SADAKA, nimemwona Mungu mnooo, nilifuata maelekezo ya somo na nikakupigia pia ukaniombeaa nilikuwa nateswa na ndoto ovu na mawazo Maovu, lakini tokea hapo nilipokea nguvu ya Roho Mtakatifu nipo huru sasa.
6. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI. POLE NA KAZI/MAJUKUMU.
MIMI NIKO ZANZIBAR NASUMBULIWA NA TATIZO LA MASIKIO MUDA MREFU SANA SISIKII VIZURI.
SIKUZALIWA HIVI ILA TATIZO LIMENIANZA NIKIWA KIDATO CHA 4. WAZAZI WANGU WAMEHANGAIKA SANA HADI SASA BADO. NAKUWA NASOMA POST ZAKO KWENYE FACEBOOK. JANA NIMESOMA POST YAKO INASEMA; KUSHAMBULIWA MIGUU NDOTONI.
MTUMISHI NIKIWA NASOMA KUNASEHEMU UMEANDIKA; KUNA MTU ANAENDA KUFUNGULIWA KWA DAMU YA YESU. NILIPOSOMA TU HAPO MWILI WOTE ULITETEMEKA SIMU ILIDONDOKA IKAZIMA NA SIJAMALIZA KUSOMA HIYO POST. SASA NAJIULIZA KWANINI AU NINGEMALIZA KUSOMA NINGEFUNGULIWA KUSIKIA?
NAOMBA MSAADA MTUMISHI.
7. Bwana Yesu asifiwe mtumishi Mabula.
Mungu ni mwema Mtumishi yaani yule mgonjwa uliyemuombea karuhusiwa na ameanza kutembea na kuongea wakati mwanzo alikuwa hawezi kutembea wala kuongea.
Mungu akubariki sana sana.
8. Mtumishi Bwana Yesu asifiwe. nashukuru kwa maombi yako miungurumo masikioni siisikii tena, yaani Mtumishi barikiwa kwa maombi yako miungurumo ya ng'ombe masikioni siiskii tena naomba tu zidi kuniombea yafunguke kabisa.
9. Shalom mtumishi.
Nashukuru kwa maombi yako ya amekuja mtu kwa nia ya kunioa.
Kwangu ni muujiza mkubwa mno, naomba tu endelea kuniombea zaidi.
10. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu naendelea vizur leo nimeweza kulala maana nilikuwa siwezi hata kulala sababu ya maumivu, sasa hivi naongea maumivu yamepungua kabisa nitatuma sadaka ya shukurani.
Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Leo nakuletea baadhi ya shuhuda kama nilivyotumiwa na baadhi ya marafiki zangu, sifa heshima na utukufu wote kama ulivyo ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni.
Shuhuda hizi zilitokana na maombi na zingine zilitokana Neno la MUNGU.
1. Shukrani Mtumishi.
Mimi niko Kenya na nimefaidishwa na mafundisho yako. Aidha maombi hujaninyima. Kwa maombi yako nilipata kitambulisho ambacho kimeniwezesha kupata mkopo wa kununua kipande cha shamba baada ya kuhangaishwa na kukoseshwa amani na mavyaa. Mtumishi nakusihi usichoke kuniombea kibali kwa Mungu niweze kujenga na pia mipaka yangu ipanuke. Shalom!
2. Bwana Yesu asifiwe mtumishi! Namshukuru Mungu kupitia maombi yako,nimepigiwa simu na mkuu wa shule ambayo nilienda kufanya usaili mwaka jana lakini sikuitwa.
Nilishakata tamaa lakin leo kanitafuta na kuniambia kesho atanipigia simu ili tuonane. Kwa kweli ni miujiza!
3. BWANA asifiwe mtumishi! napenda kumshukru MUNGU kwani amenikumbuka tangu kipindi nilikuomba unikumbuke kwenye maombi kuhusu kazi yangu nilipwe kwa wakati, naomba tujumuike kuomba ili nipandishwe mshahara nipate off pia nipate kibali pia niwe namtolea MUNGU zaka na zaka yangu ipokelewe kwa MUNGU.
Naona majibu tarehe 31 mwezi wa jana nimekumbukwa japo nimelipwa nusu lakini ninatangua nadhiri yangu kwa MUNGU.
Pia mtumishi naomba umuombee na mke wangu ana sumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu sasa naomba aponywe zaidi ya yote na mshukuru MUNGU kwa upendo wake.
4. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Namshukuru Mungu kwa maombi yako.
nilikuwa naumwa tumbo nilienda kupima jumanne wiki iliyopita hospitali nikakutwa nina vidonda vya tumbo, ila Mungu acha aitwe Mungu, tangia juma tano mpaka leo ninayasimulia matendo makuu ya Bwana. Maumivu ya vidonda siyasikii katika tumbo langu.
Ni muujiza kweli.
5. Asantee sana mtumishi wa Bwana na Mungu akubariki umekua msaada mkubwa katika maisha yangu nimemuona Mungu kwa njia ya ajabu saana naamini nitaendelea vizuri zaidi. Nashindwa hata niandikaje ila utukufu ni kwake Bwana aliezifanya mbingu na nchi kwa neno lake Mungu wa mbinguni akubariki saana akusaidie katika kufundisha kondoo zake.
6. Mtumishi Bwana Yesu asifiwe nilikua nafuatilia somo lako la mashambulizi kwenye mikono, miaka mitatu imepita sasa nilikua nikifanya maombi nikaota na pambana na ng,ombe mkono wangu wa kushoto uko kwenye kinywa cha huyo ng,ombe nilimpiga mangumi ya mdomoni mpaka akaachilia mkono wangu lakini bado uchumi uliondoka na bado nikafilisika kabisa mpaka sasa uchumi haujakaa sawa.
Nilikuwa sijui Maana ya kushambuliwa mkono wa kushoto ndotoni na madhara yake.
Lakini kupitia somo lako nimejua ni nini tatizo na ni nani nilikuwa napambana naye kuhusu uchumi wangu.
Naamini kwa maelekezo ya somo hilo ulilofundisha nitashinda.
7. BWANA YESU asifiwe mtumishi wa MUNGU. Nakushukuru sana kwa mawaidha uliyonipa, nimekuwa na maombi ya kufunga na kuomba kwa mwezi wote wa August
Na hatimaye BWANA amejibu jana ndio nimepeleka mizigo yangu DHL kuisafirisha kwetu Kenya imekaa hapa Saudia kwa miaka mitatu, nimekuwa nikishindana na tajiri vita katika ulimwengu wa roho kumbe alikua anazuia mizigo isiondoke hapo nami nilijiona nimefungwa miguu na mikono nina hung kwenye ndoto, kwa hakika nimeomba maombi mengi sana hata ukiuliza ulitumia mistari gani hadi kufikia ushindi huu siezi eleza. maombi ya mwisho juzi niliomba kumkumbusha BWANA yale nimetenda hapa nikimsihi MUNGU anikumbuke. baada ya hapo ROHO akaniongoza kuiteka nyumba hii KWA DAMU YA MWANA KONDOO KATIKA JINA LA YESU na kuwasha moto ndio nikafunuliwa jinsi moto unawaka mwekundu hadi vyombo vyangu vikiwa vimefungiwa kabisa, namshukuru BWANA kwa hili
SIFA ZOTE namrudishia yeye.
MUNGU akutegemeze mtumishi
8. MWALIMU, YESU ASIFIWE SANA. KWA HAKIKA NAMSHANGAA SANA MUNGU NI MWEMA LAKINI PIA NI MUAMINIFU SANA LAST TIME TULIKUWA VIBAYA SANA KIFEDHA NAKUMBUKA BINAFSI NILIKUWA NA MIA TU NA MME WANGU YEYE NI FUNDI HAKUWA NA HELA KABISA WALA KAZI. NILIKUSHIRIKISHA HILI SASA HIVI KAZI ZIMEMJIA MFULULIZO MPAKA ANALALA KAZINI. SIFA HESHIMA NA UTUKUFU NI KWA BWANA PEKEE. MUNGU AKUBARIKI SANA MWALIMU NA AKUKUMBUKE KATIKA KUKUZA HUDUMA YAKO.

Comments